Kama kweli hawa wazee wawili wamejitoa chamani

Kama kweli hawa wazee wawili wamejitoa chamani

"Kazi zilipatikana kwa vimemo tu... Tenda hasa ndani ya chama kwa simu moja tu.. Hawa walihubiri wasichofanya kwa vitendo na walitenda wasichohubiri kwa maneno..."

Uzi wako wote uliuhitimishwa hapa, ila ninalojiuliza ni Kama washirika wao watajitoa au watasubiri kutolewa na chuma?
Je hii Ina maanisha nini, iwapo watu Hawa hawakuwa wema kwa muda mrefu na chama kilishindwa kuwatema?

= mifumo inayoendesha chama ni mibovu, na Kama chama hicho kitaendesha nchi mifumo yake itakuwa mibovu pia.
 
Mheshimiwa Mshana Jr, ukiona nyani mzee ujue kakwepa mishale mingi. Misukosuko ambayo CCM imewahi kupitia ingekua ni chama kingine tayari tungekua tumeshakizika.

Kwa taarifa yako tu nikwambie CCM sio chama dola kusema kwamba kinasaidiwa saidiwa uwepo wake(its existence). Nakuhakikishia kua CCM NDIO DOLA YENYEWE. Fungua akili yako na uone mambo kwa uhalisia. Acha niishie hapo
 
Mshana Jr, Mkuu huwa napitia sana maandiko yako. Huwa zaidi unapendelea kuandika mambo yanayohusu uchawi na siasa ukigusia kwa mbaali. Leo umeitafasili vzr sana CCM.

Lakini ninavyofahamu mimi watanzania tunafanana sana kwa tabia zetu. Hii ndiyo inayopelekea vyama vya upinzania kuwachukua wanachama toka CCM ambao wanafahamika fika kuwa hawana maadili hata tone na kuwapa vyeo/madaraka makubwa. Na kwa sababu sisi ni wapenda vyama na siyo wapenda sera au misimamo na tabia za kiongozi, inatubidi kuwashadadia watu hao hao wasiyofaa.

Mfano ni hawa watu Lowasa, Sumaye na Nyarandu. Hakuna mtz asijua tabia za wa2 hawa. Lakini ajabu upinzani waliwapokea na kuwapa madaraka makubwa. Na sisi wanachama tukawapamba na kuwapa kura za kutosha. Matokeo yake ni kushusha ukuaji wa CDM.

Ni imani yangu kuwa CDM wangekuwa na msimamo thabiti na wakakataa kuwapokea viongozi hao, kwa ukuaji wa CDM iliyokuwa ikikuwa, kwa sasa ingekuwa mbali sana. Lakini kwa kuwapokea viongozi hao CDM ni kweli ilisonga hatua 80 mbele lakini kwa sasa imerudi hatua 40 nyuma. Ingewakataa ingetuimanisha kwamba ni chama kilicho na msimamo thabiti. Lakini kwa kuwapokea huku ikijua tabia zao imeonyesha ni chama chenye tabia ya popo.

Si hivyo tu lakini tujue wazi kuwa CCM wana watu wana elimu nzuri ya siasa nao kati yao wakiwa ni Makamba na Kinana. Si ajabu hii ni mbinu imepangwa maalum kuvivuruga vyama vya upinzani na hasa kwa mwaka huu wa uchaguzi. Kwanini iwe 2020?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niliona siasa ni upuuzi mwaka 2015 watu walipounga mkono mabadiko yanayoongozwa na lowassa. Naona upuuzi Tena Kama huo ukiongozwa na membe kwa kuungwa mkono na upinzani. Alafu eti Leo watu wanawasgangilia kinana na makamba kwamba ni ni majasiri kwa kujitoa ccm kiss maslahi yao kiuchumi yapo mashakani.
Kiukweli Kama hauna maslahi ya moja kwa moja kwenye siasa ni Bora kukaa pembeni tu vinginevyo akili yako ina walakini.

Ni upuuzi sana.. Baada ya miaka michache mbele mzee baba aliyepo sasa naye ataungwa mkono na wapinzani. Polytrics
 
Nakuhakikishia kua CCM NDIO DOLA YENYEWE. Fungua akili yako na uone mambo kwa uhalisia. Acha niishie hapo [emoji848][emoji848][emoji848][emoji144][emoji144][emoji144][emoji144][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124]
Mheshimiwa Mshana Jr, ukiona nyani mzee ujue kakwepa mishale mingi. Misukosuko ambayo CCM imewahi kupitia ingekua ni chama kingine tayari tungekua tumeshakizika.

Kwa taarifa yako tu nikwambie CCM sio chama dola kusema kwamba kinasaidiwa saidiwa uwepo wake(its existence). Nakuhakikishia kua CCM NDIO DOLA YENYEWE. Fungua akili yako na uone mambo kwa uhalisia. Acha niishie hapo

Jr[emoji769]
 
Tetesi hazikusema amekufa, ila zilisema yuko mahtuti. Sasa mtu akiwa mahtuti si kuna kupona au kufa?

Sent using Jamii Forums mobile app
Khantwe ndugu yangu, kuna watu walikua wanasema "Bi Mkubwa aapishwe kwanini wenye mamlaka wanataka kupindisha katiba wamteue mwingine?". Maana yake walisha "thibitisha" kifo.

Na kama mtu alikua "mahututi" kama ilivosemekana iliwezekanaje akaibuka baada ya siku tatu akiwa kazini japo alionekana akiwa na uchovu? Au sielewi labda maana ya mahututi
 
Hii mada iachwe kama ilivyo.. Kilichotokea zile siku tatu za tarahuki hakiwezi kusemwa sasa ila kuna siku kitasemwa... Sijui ninini kilitokea lakini speculations zilikuwa nyingi na nyingine zilitoka ndani kabisa... Hili halipaswi kujadiliwa sasa.. Si salama sana... LIACHWE...!!!

goggles, Labda hujui nchi iko wapi au hauishi Tanzania, chadema au chama chochote cha siasa Tanzania kwa awamu hii ya tano vilipaswa viwe vimeishakufa kutokana na nguvu kubwa iliyotumika kuvikandamiza Kwa kipindi chote cha awamu ya tano imetumia nguvu kubwa Sana kutaka kuviua, imetumia majeshi, polisi, watu binafsi Kwa kupewa hela imetumwa usalama wa taifa, imetumia fedha za walipa kodi kununua wabunge na madiwani Lakini cha ajabu vyama vyote vya kisiasa ukiondoa cuf vimeimalika zaid, katika hali ya kawaida kungekuwa Hakuna chama kinaitwa chadema, nguvu iliyotumika itakuwa hauko Tanzania Mkuu

Kuchukua watu toka Ccm ndio necha ya chama chochote cha kisiasa, ukiona chama kinamkataa mtu eti ni mchafu ujue hao hawafanyi siasa hiyo ni kampuni maaana siasa watu ndio mtaji wa chama Kama unavyosema kuwa lowasa alipelekea chadema kupata wabunge wengi, ndio maaana unaona hata Ccm mtu akiondoka Ccm watashangilia na kusema maneno meeengi na akirud wanashangilia na kumsafisha tena

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii mada iachwe kama ilivyo.. Kilichotokea zile siku tatu za tarahuki hakiwezi kusemwa sasa ila kuna siku kitasemwa... Sijui ninini kilitokea lakini speculations zilikuwa nyingi na nyingine zilitoka ndani kabisa... Hili halipaswi kujadiliwa sasa.. Si salama sana... LIACHWE...!!!

Jr[emoji769]
Nakubaliana nawe kaka Mshana Jr
 
Ni kweli
Hii mada iachwe kama ilivyo.. Kilichotokea zile siku tatu za tarahuki hakiwezi kusemwa sasa ila kuna siku kitasemwa... Sijui ninini kilitokea lakini speculations zilikuwa nyingi na nyingine zilitoka ndani kabisa... Hili halipaswi kujadiliwa sasa.. Si salama sana... LIACHWE...!!!

Jr[emoji769]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Hawana ushawishi tena chamani acha wajing'atue tu", alisikika mwanachama mmoja wa chama kikongwe akisema
 
Bado kuna kizungumkuti kwenye hili

Jr[emoji769]
 
Hakuna wakuwasindikiza, watz hatuna utamaduni huo wa kufuata upepo km Bendera, refer yaliyotokea 2015 yaliyomkuta Lowasa.
 
Back
Top Bottom