Kama kweli hawa wazee wawili wamejitoa chamani

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
375,677
Reaction score
870,373
Taarifa hizi zilianza kama minong'ono siku ya tarehe 7 feb.. Zikapuuzwa na wengi.. Baadae ikawa si minong'ono tena bali tetesi.... Tetesi zinapaswa kukanushwa chini ya masaa 24... Zikipita saa 72 bila kanusho kifuatacho ni ithibati.. Habari ikishathibitishwa hukoma kuwa tetesi na kuwa BREAKING NEWS.... HABARI MPASUKO!

Pengine sasa kinachosubiriwa ni taarifa rasmi mbaya za makatibu wawili wastaafu kujitoa toka chama tawala.. Mzee Yusuph Makamba na Mzee Abulhaman Kinana... Hii inawezekana ikawa habari mbaya na kubwa kuwahi kutokea kwenye awamu hii.. Lakini je ni nani wa kuumia?
Ni nani wa kushangilia?
Ni nani wa kupata?
Ni nani wa kukosa?
Tuwe makini tusije tukaingizwa kwenye mtego wa vita ya propaganda kati ya ndugu wanafamilia wawili
Sitaki nizungumzie sana kuhusu ccm kwakuwa ndani ya hicho chama hakuna msafi hata mmoja.. Wanachotofautiana ni viwango tuu
Ni lazima turejee nyuma 2015 kwenye uchaguzi uliojaa ghiliba, dhuluma, rushwa na wizi wa wazi kabisa wa kura.. Wazee hawa kwa nafasi zao hawana jinsi ya kuikwepa hii lawama na laana...
Kiuhalisia kwa hali ilipokuwa imefikia kipindi kile kama Taifa tulihitaji mabadiliko.. Mabadiliko ambayo yangeusafisha uchafu wote wa ccm kwa dodoki la chuma

Rais mstaafu JK kwa usikivu wake na kusoma alama za danger zone kwenye chama chake yalifanyika maamuzi yaliyokuja kuleta matokeo tuliyo nayo sasa..! Wazee hawa ni makada kindakindaki walioiva kiitikadi wakitokea jeshini walikohudumu sehemu kubwa ya maisha yao tena kwa nafasi za juu.. Hawa ni waumini na zao la siasa za kijamaa za chama kimoja
Ni sehemu ya wafaidikaji wakubwa waliokula vizuri fungate ya uhuru..maisha yao na familia zao na ndugu zao na jamaa zao hayajui dhiki ni kitu gani... Nyakati zao hakukuwa na ugumu.. Connection zilikuwa kila mahali
Kazi zilipatikana kwa vimemo tu... Tenda hasa ndani ya chama kwa simu moja tu.. Hawa walihubiri wasichofanya kwa vitendo na walitenda wasichohubiri kwa maneno...

Mzee Makamba akiwa ni mtuhumiwa wa ufisadi na upugaji wa wanae.. Mzee Kinana yeye ni ishu za biashara na tuhuma za pembe za ndovu.. Yote juu ya yote walikuwa wachezaji muhimu kwenye vilinge vya rushwa ndani ya ccm na Taifa katika ujumla wake..

Rais aliyepokea kijiti ana msaada mkubwa sana wa wawili hawa.. Lakini kutokana na hali ilivyokuwa ilikuwa ni lazima afanye jambo litakaloleta complete overhaul ili wananchi waweze kurudisha imani yao kwa chama tawala
Amejaribu kulifanya hili kwa mkono wa chuma na mwangwi wa maumivu yake ulifika mbali.. Pamoja na mengine yote kukatwa kwa mirija ya ulaji na kuishi kwa mazoea ndani ya ccm ndio vimekuja kutupa matokeo haya ya sasa...
Kuna wakati Magufuli anaona anafanya kitu sahihi kabisa as per kilio cha wananchi way back 2015 lakini anapata mshangao na kubaki na taharuki kubwa kuona kwamba hapewi ushirikiano walioahidiana?
Hawa wazee walihitaji heshima na kutambuliwa huduma yao katika utumishi wao kwenye Taifa hili lakini pamoja na hili ni kutoguswa kwa maslahi yao na ya washirika wao... Magufuli anataka kusafisha chama ms kurudisha imani kwa wananchi.. Kila upande hapa una supporters
Sasa kwenye hiki kizungumkuti kuna
CCM asili vs CCM makinikia
Kuna CCM maslahi na kuna CCM wafia chama
Kuna CCM wenye chama na kuna CCM wakuja
Wote hawa katika ujumla wao wanaunda makundi mawili muhimu
1. CCM awamu ya tano
2.CCM awamu zilizopita
Ukweli na uhalisia wa hizi habari pamoja na uimara wa mwenyekiti wa sasa wa chama ndio vitatoa picha kamili ya ccm 2020
Kila kundi linatafuta kuungwa mkono.. Kwahiyo propaganda zitakuwa nyingi kama hapo nyuma... Na tutegemee wanachama prominent zaidi kujitoa chamani kama karata zikichangwa vema la sivyo wataishia kuwa hawa wawili tuu

Jr[emoji769]
Zaidi soma Rais Magufuli anaiua CCM kifo cha mateso makubwa
 
MAKATIBU wakuu wastaafu wawili wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana na Yusuf Makamba, wamejivua uanachama wa chama hicho.

Habari zilizoifikia SAUTI KUBWA zinasema Kinana na Makamba walijiondoa rasmi CCM kwa maandishi. Barua zao, kila mmoja na ya kwake, zilifikishwa ofisini kwa Katibu Mkuu wa CCM tarehe 7 Februari 2020.

Chanzo kinachoaminika kutoka CCM Makao Makuu kimeiambia SAUTI KUBWA: “Barua zao zimefika kwa nyakati tofauti, zimepokelewa. Lakini inaonekana kama walikuwa wameziandika muda mrefu baada ya kushauriana, maana zinafanana na zimewasilishwa siku moja. Taarifa hizi zilipofikishwa kwa Mzee (Rais John Magufuli) zilimvuruga kwa kweli.”

Kwa mujibu wa chanzo hicho, ambacho hakitatajwa hapa, Rais Magufuli, baada ya kupokea ujumbe wa Kinana na Makamba kujivua uanachama, aliwaomba wazee wawili waandamizi – Rais Mstaafu Benjamin Mkapa na Spika Mstaafu Pius Msekwa – wamsaidie kuzungumza na akina Kinana ili kuwashawishi wabadili msimamo wao.

Hata hivyo, Kinana na Makamba wamegoma kusikiliza ushawishi wa mtu yeyote. Katika barua zao za kujiondoa CCM, kwa mujibu wa chanzo chetu, Kinana na Makamba waliambatanisha pia kadi zao za uanachama.

“Tayari wameturudishia kadi zetu, maana yake wao si wanachama wetu tena,” kimesema chanzo hicho.

Kinana na Makamba ni miongoni mwa makatibu wakuu wanaoheshimika katika CCM, wenye ushawishi, na ambao wametumikia nchi katika nyadhifa mbalimbali kuanzia jeshini hadi serikalini na kwenye chama.

Siku ambayo walikabidhi barua na kadi zao na kutangaza rasmi kujiondoa CCM, ndiyo siku walipotarajiwa kuhojiwa na Kamati ya Maadili ya CCM iliyoagizwa na Rais Magufuli katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), ili wajieleze kuhusu waraka walioanidika kwa Baraza la Wazee la chama hicho wakilalamikia kubezwa na kudhalilishwa na mhuni mmoja anayetumia jina la rais kudhihaki na kushambulia wakosoaji wa rais na serikali.

Mbali na Kinana na Makamba, mwingine aliyeitwa kuhojiwa na kamati hiyo ni Bernard Membe, waziri wa zamani wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ambaye aliunga mkono waraka wa wazee hao, na pia alidukuliwa akizungumza katika simu mambo ambayo hayakumfurahisha Rais Magufuli.

Yeye alikutana na kamati hiyo Mjini Dodoma Ijumaa tarehe 7, Februari 2020; na baada ya mahojiano alionekana mwenye kujiamini na mwenye furaha. Mmoja wa wajumbe walioshiriki mahojiano hayo amezungumza na SAUTI KUBWA kwa sharti la kutotajwa, akisema: “Tulijuta kumuita Membe. Kuna maswali amehoji na masuala amezungumza nasi hadi tukahisi yeye ndiye anayetuhoji. Ukweli ni kwamba chama chetu kinahitaji mabadiliko makubwa ya kimsingi, maana kuna shida mahali. Bwana mkubwa anatupelekesha, na watu jasiri wa kumwambia ukweli hawapo, tunaishia kuagizwa tu, hata kutenda mambo yaliyo kinyume cha misingi ya CCM. Membe ametukumbusha yote haya. Kwa kweli, sijui kinachoofuata.”

Hata hivyo, SAUTI KUBWA iliambiwa wiki iliyopita kuwa agizo la kamati kuwahoji wakongwe hao lilikuwa kama igizo tu, kwani Rais Magufuli na watu wake walishaamua kuwa Membe na Kinana wavuliwe uanachama, na Mzee Makamba apewe onyo kali.

Kwa Kinana na Makamba kujivua uanachama na kugoma kuhojiwa, wamewaza hatua mbili mbele ya Magufuli. Chama hakiwezi kuwahoji kwa kuwa wao hawafungwi tena na nidhamu wala maadili ya CCM kwa kuwa si wanachama CCM.

Ingawa barua zao zilipelekewa kimya kimya, na uongozi wa juu wa CCM umekuwa unahangaika kuzuia taarifa hizi kuvuja, zilivuja mapema mno; na kitendo chao cha kutofika mbele ya kamati kuhojiwa kimezua maswali na mjadala mpana ndani nanje ya CCM.

Baadhi ya wadau wa siasa za Tanzania wanasema inawezekana kitendo hiki kikawaingiza wote wawili, au mmoja wao, kwenye matata makubwa, kwani uongozi wa CCM ni wa visasi, unaweza kutaka kuwakomoa na kuwadhalilisha.

Profesa mmoja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amesema: “Tusishangae sasa kusikia siku moja Kinana au Makamba wametiwa mbaroni na wanashitakiwa kwa utakatishaji fedha, maana hii ndiyo fimbo mpya ambayo inatumika kuumiza wanaotofautiana na watawala. Lakini iwapo watashitakiwa umma utajua kuwa sababu hasa si uhalifu wao bali ni hii barua yao na uamuzi wao.”

Kiongozo mmoja mwandamizi wa CCM ameiambia SAUTI KUBWA: “Kiukweli, Mzee Kinana na Mzee Makamba hawana cha kupoteza. Nadhani sisi ndio tuna cha kupoteza, maana ukisoma waraka unaowasababishia haya yote utagundua kuwa wao ni watetezi wa misingi ya chama chetu. Wanachotetea ndicho wanaCCM wote tunapaswa kutetea, lakini sasa tofauti iliyopo kati yetu na wao ni kwamba wao wameonyesha ujasiri ambao sisi hatuna. Wengi wetu tumebaki kutii maagizo ya bwana mkubwa, huku chama kinaporomoka!”

SAUTI KUBWA inatambua kuwa kuna mtifuano mkubwa ndani ya CCM ambao haujawahi kutokea tangu uwepo wa chama hicho, ingawa wanafanikiwa kuufunika kwa kutishana – kwa kutumia vuombo vya dola.
 
Wamewawahi...!!!

tapatalk_1581214471052.jpeg

Jr[emoji769]
 
Hizi ni porojo kama zilivyokua zile porojo zingine za mama kuongoza nchi kwa muda. Tetesi na porojo zile zilienea na si serikali wala chama zilizojitokeza na kukanusha hata baada ya hizo saa 72 anazosema mleta uzi. Ni kama walizipiuza tu tetesi zenyewe maana kwa vyovyote vile walizisikia

Serikali ilijibu kwa vitendo baada ya aliyekua kazushiwa kifo kujitokeza hadharani mbele ya luninga, live akifanya majukumu yake aliyokabidhiwa kikatiba. Ilikua ni aibu kwa wazushi
 
Niliona siasa ni upuuzi mwaka 2015 watu walipounga mkono mabadiko yanayoongozwa na lowassa. Naona upuuzi Tena Kama huo ukiongozwa na membe kwa kuungwa mkono na upinzani. Alafu eti Leo watu wanawasgangilia kinana na makamba kwamba ni ni majasiri kwa kujitoa ccm kiss maslahi yao kiuchumi yapo mashakani.
Kiukweli Kama hauna maslahi ya moja kwa moja kwenye siasa ni Bora kukaa pembeni tu vinginevyo akili yako ina walakini.
 
waacha waondoke ili siasa nazo zilete utamu mwingine kama soka sio kila siku matokeo yaleyale licha ya hiyo hawana kasi ya kuendana na kizazi hiki waache wapumzike tu.
 
Hao wazee wawili Kinana na Makamba ni wanafiki, kwanini wameshindwa kumpa ushirikiano Magufuli? na kama wana hoja zao kwanini wasingezipeleka kwenye kamati ya mahojiano kama alivyofanya Membe? wameamua kujitoa kwenye chama chao kwa misingi ipi, kwamba utawala wa Magufuli unawaonea? au hasira ya mtoto kupigwa chini kwenye uwaziri? na kusema kweli January alikuwa weak, Magufuli alimlea sana kwenye ile nafasi, alistahili kutumbuliwa mapema zaidi, na vile vikatuni vyake alivyokuwa anamchora Magufuli hovyo bado akavumiliwa!

Hao jamaa wawili ni corrupt, wanapewa heshima tu yakuitwa wazee wa chama but they don't deserve it, huu ndio ulikuwa wakati wao kuungana na Magufuli kumpa ushirikiano wa mawazo na vitendo kurekebisha matatizo ndani ya chama chao, na nchi kwa ujumla, but surprisingly wameamua kumsusia Magufuli, bila kusema walikosewa wapi, then waone chama cha kingefanya nini, coz kweli Musiba nae ni mropokaji sana, but hata wao nao sio wasafi kiivyo. Walimpa Magufuli urais wakidhani angeendelea kuwa chini yao, afuate watakavyo, sasa kawageuka nao wameamua kumgeuka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi ni porojo kama zilivyokua zile porojo zingine za mama kuongoza nchi kwa muda. Tetesi na porojo zile zilienea na si serikali wala chama zilizojitokeza na kukanusha hata baada ya hizo saa 72 anazosema mleta uzi. Ni kama walizipiuza tu tetesi zenyewe maana kwa vyovyote vile walizisikia

Serikali ilijibu kwa vitendo baada ya aliyekua kazushiwa kifo kujitokeza hadharani mbele ya luninga, live akifanya majukumu yake aliyokabidhiwa kikatiba. Ilikua ni aibu kwa wazushi
Ila ni kweli kabisa aliugua na alikuwa hoi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom