Taarifa hizi zilianza kama minong'ono siku ya tarehe 7 feb.. Zikapuuzwa na wengi.. Baadae ikawa si minong'ono tena bali tetesi.... Tetesi zinapaswa kukanushwa chini ya masaa 24... Zikipita saa 72 bila kanusho kifuatacho ni ithibati.. Habari ikishathibitishwa hukoma kuwa tetesi na kuwa BREAKING NEWS.... HABARI MPASUKO!!!
Pengine sasa kinachosubiriwa ni taarifa rasmi mbaya za makatibu wawili wastaafu kujitoa toka chama tawala.. Mzee Yusuph Makamba na Mzee Abulhaman Kinana... Hii inawezekana ikawa habari mbaya na kubwa kuwahi kutokea kwenye awamu hii.. Lakini je ni nani wa kuumia?
Ni nani wa kushangilia?
Ni nani wa kupata?
Ni nani wa kukosa?
Tuwe makini tusije tukaingizwa kwenye mtego wa vita ya propaganda kati ya ndugu wanafamilia wawili
Sitaki nizungumzie sana kuhusu ccm kwakuwa ndani ya hicho chama hakuna msafi hata mmoja.. Wanachotofautiana ni viwango tuu
Ni lazima turejee nyuma 2015 kwenye uchaguzi uliojaa ghiliba, dhuluma, rushwa na wizi wa wazi kabisa wa kura.. Wazee hawa kwa nafasi zao hawana jinsi ya kuikwepa hii lawama na laana...
Kiuhalisia kwa hali ilipokuwa imefikia kipindi kile kama Taifa tulihitaji mabadiliko.. Mabadiliko ambayo yangeusafisha uchafu wote wa ccm kwa dodoki la chuma
Rais mstaafu JK kwa usikivu wake na kusoma alama za danger zone kwenye chama chake yalifanyika maamuzi yaliyokuja kuleta matokeo tuliyo nayo sasa..! Wazee hawa ni makada kindakindaki walioiva kiitikadi wakitokea jeshini walikohudumu sehemu kubwa ya maisha yao tena kwa nafasi za juu.. Hawa ni waumini na zao la siasa za kijamaa za chama kimoja
Ni sehemu ya wafaidikaji wakubwa waliokula vizuri fungate ya uhuru..maisha yao na familia zao na ndugu zao na jamaa zao hayajui dhiki ni kitu gani... Nyakati zao hakukuwa na ugumu.. Connection zilikuwa kila mahali
Kazi zilipatikana kwa vimemo tu... Tenda hasa ndani ya chama kwa simu moja tu.. Hawa walihubiri wasichofanya kwa vitendo na walitenda wasichohubiri kwa maneno...
Mzee Makamba akiwa ni mtuhumiwa wa ufisadi na upugaji wa wanae.. Mzee Kinana yeye ni ishu za biashara na tuhuma za pembe za ndovu.. Yote juu ya yote walikuwa wachezaji muhimu kwenye vilinge vya rushwa ndani ya ccm na Taifa katika ujumla wake..
Rais aliyepokea kijiti ana msaada mkubwa sana wa wawili hawa.. Lakini kutokana na hali ilivyokuwa ilikuwa ni lazima afanye jambo litakaloleta complete overhaul ili wananchi waweze kurudisha imani yao kwa chama tawala
Amejaribu kulifanya hili kwa mkono wa chuma na mwangwi wa maumivu yake ulifika mbali.. Pamoja na mengine yote kukatwa kwa mirija ya ulaji na kuishi kwa mazoea ndani ya ccm ndio vimekuja kutupa matokeo haya ya sasa...
Kuna wakati Magufuli anaona anafanya kitu sahihi kabisa as per kilio cha wananchi way back 2015 lakini anapata mshangao na kubaki na taharuki kubwa kuona kwamba hapewi ushirikiano walioahidiana?
Hawa wazee walihitaji heshima na kutambuliwa huduma yao katika utumishi wao kwenye Taifa hili lakini pamoja na hili ni kutoguswa kwa maslahi yao na ya washirika wao... Magufuli anataka kusafisha chama ms kurudisha imani kwa wananchi.. Kila upande hapa una supporters
Sasa kwenye hiki kizungumkuti kuna
CCM asili vs CCM makinikia
Kuna CCM maslahi na kuna CCM wafia chama
Kuna CCM wenye chama na kuna CCM wakuja
Wote hawa katika ujumla wao wanaunda makundi mawili muhimu
1. CCM awamu ya tano
2.CCM awamu zilizopita
Ukweli na uhalisia wa hizi habari pamoja na uimara wa mwenyekiti wa sasa wa chama ndio vitatoa picha kamili ya ccm 2020
Kila kundi linatafuta kuungwa mkono.. Kwahiyo propaganda zitakuwa nyingi kama hapo nyuma... Na tutegemee wanachama prominent zaidi kujitoa chamani kama karata zikichangwa vema la sivyo wataishia kuwa hawa wawili tuu
Jr[emoji769]
Zaidi soma
Rais Magufuli anaiua CCM kifo cha mateso makubwa