Kama kawaida wazee wa kudandia hoja wameshadandia issue ya mikopo kwa wanafunzi

DAT BOY SU

Member
Nov 15, 2017
29
30
Hili swala la wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam kucheleweshewa fedha zao za mikopo ni swala nyeti na mtambuka, busara inahitajika katika kuliendea jambo hili pasina kuleta sintafahamy yoyote kwa jamii. Cha kusikitisha hili swala baadhi ya viongozi wa upinzan wameshaona ndo agenda yao na kuanza kuropoka bila kujua kuwa wanawaingiza hawa vijana kwenye matatizo kwan hilo sio swala la kisiasa hata kidogo ni la kitaaluma waache wanataaluma wenyew watalimaliza.

Kumeibuka kundi la kudai wao ndio watetezi wa wanafunzi mala watawawekea wanasheria na kelele nyingi na vijana pasina kuchambua kilicho sahihi watajingiza kwenye mtego ambao badae utawaletea shida huko mbeleni,

Serikali kupitia wazir mwenye dhamana. alishatolea ufafanuzi kuhusu swala hili pia mkurugenz wa bodi nae ameshaliongelea tena kwa kina mpk kufikia jmos hwa vijana watapatiwa fedha zao lakin watu wanaojita watetez wameibuka gafla na kuanza kuwalubin wanafunz kufanya fujo bila kuangalia future yao huko mbele.

Hivi vyama ambavyo hata mvua ya juzi kunyesha kwao imekuwa ajenda tayar na,kuanza kuilaum serikali as if ndo imeleta hiyo,mvua hiv vyama twapasa kuviogopa kama ukoma maana havijui wanapigania nn na wanataka nn na kwa wakati gani.
 
Back
Top Bottom