Barua ya Wazi kwa Rais Samia Suluhu; Pendekezo la Kuanzishwa kwa Benki ya Wahitimu wa Elimu ya Juu (HEGB)

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,331
8,254
Barua ya Wazi kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh.Dkt. Samia Suluhu Hassan; Pendekezo la Kuanzishwa kwa Benki ya Wahitimu wa Elimu ya Juu (HEGB).

Mpendwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan,

Ni imani yangu kuwa barua hii inakufikia ukiwa na afya njema na mwenye nguvu. Naandika barua hii kukujulisha juu ya jambo muhimu sana linaloweza kuleta athari chanya kwa taifa letu kuhusiana na wimbi kubwa la ukosefu wa ajira kwa vijana, hasa wale wanaohitimu elimu ya juu (vyuo). Pamoja na ufaulu mkubwa, bado vijana hao wamekuwa wakitaabika mno kupata ajira kutokana na uhaba wa fursa na ukosefu wa mitaji ya kuanzisha biashara mbalimbali.

Kutokana na changamoto hii, napendekeza kuundwa kwa Benki ya Wahitimu wa Elimu ya Juu (HEGB). Benki hii itakuwa suluhisho la kiuchumi kwa wahitimu wanaotamani kuanzisha biashara lakini wanapata wakati mgumu kupata mitaji kutoka katika benki mbalimbali hapa nchini. Benki hii itawawezesha wahitimu hao kuwa wajasiriamali kwa kuwanufaisha kwa mikopo inayolingana na ubunifu na ufanisi wa mawazo yao ya kibiashara. Benki hiyo itaendeshwa kutokana na michango watakayokuwa wakichangia wanafunzi wa elimu ya juu watakapokuwa masomoni kwa kila muhula.

Kutokana na kuundwa kwa benki hii, tunaweza kuchochea uvumbuzi na ujasiriamali miongoni mwa wahitimu wengi wanaomaliza elimu ya juu, na hivyo kupunguza wimbi la ukosefu wa ajira hapa nchini. Sio tu kutoa mikopo, Benki hii pia italenga katika kueneza dhana ya kujiajiri na ubunifu, ambavyo ni muhimu katika ukuaji endelevu na maendeleo ya nchi yetu kwa ujumla.

Naamini sambamba na msaada wako tunaweza kulipa pendekezo hili uhai na kuleta mabadiliko makubwa katika taifa letu. Nitafurahia mjadala endelevu kuhusiana na swala hili na nitayajibu kwa furaha maswali yoyote unayoweza kuwa nayo kuhusiana na swala hili.

Nashukuru kwa muda wako.

Wako mtiifu,
Bright and Genius Editors
Barua pepe: bandg.editors@gmail.com
Namba za simu: 0747744895/0687746471/0612607426
 
Back
Top Bottom