Ukweli kuhusu Njia sahihi na Salama za kupunguza Uzito.

zootopia

Member
May 29, 2016
74
76
Habari za saa hii wapenda afya,

Kabla hatujaanza unatakiwa kujua kuongezeka uzito ni nini pia ni wastani upi sahihi wa uzito (body weight) katika mwili wa binadamu kulingana na urefu wake (BMI).
Kuongezeka uzito ni hali ya mwili kuwa na uzito mkubwa kuliko wastani/ kiwango kinachotakiwa.Wataalamu wengi wa afya na chakula wanasema urefu wako ndo tathmini ya uzito wako. Body mass index (BMI) ni wastani wa uzito wa mtu kwa kilogramu (kg) na urefu wake katika mita za mraba.

*Hapa chini ni viwango vya BMI;
Adult BMI Calculator - Results
BMI Weight Status
Below 18.5 Underweight
18.5—24.9 Normal
25.0—29.9 Overweight
30.0 and Above Obese
*Nakushauri msomaji nenda kwa daktari ukapime urefu na uzito wako then utafute wastani ili ujijue upo kwenye kundi gani.

Kumekuwa na upotoshaji mkubwa kuhusu njia mbali mbali za kupunguza uzito hususani kwenye mitandao ya kijamii, hiyo inatokana na ukweli kwamba watu wengi hapa nchini wanakabiliwa na tatizo kubwa na sugu la kuongezeka uzito. Watu wengi kwenye mitandao ya kijamii wamegeuka kuwa madaktari bila hata kusomea fani hyo. Wamekuja na madawa mengi wenyewe wanayaita ya asili na hayana madhara yeyote katika mwili wa binadamu, mwanaafya mwenzangu kumbuka hakuna kitu ambacho utakula/kunywa hakina madhara katika mwili wa mwanadamu, isipokuwa ni viwango vya madhara vinatofautiana. Ningependa kuwashauri msishawishike kutumia madawa ya asili ovyo ovyo maana hayana vipimo sahihi na viwango/aina za kemilali humo ndani hazijulikani pia hujui zimetengenwa katika mazingira gani.

SABABU ZA KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KUPUNGUZA UZITO.
  • Dawa nyingi za kupunguza uzito haziweki wazi madhara yake baada ya kutumia.Hakuna kitu kizuri kama kujua chakula/ kinywaji unachotumia kina madhara gani, hii itakupa wewe mwenyewe uchaguzi kwamba utumie au usitumie. Madawa haya hayaelekezi wazi kemikali zilizomo ndani.
  • Wafanyabiashara wa haya madawa wengi hawana taaluma za ufamasia, na hii ni kitu mbaya sana, maana hata ukipata tatizo hawawezi kukusaidia kwa lolote, wao wanchojali ni pesa yao tu.
  • Unaweza kujua umetatua tatizo la kuongezeka uzito kumbe umeongeza tatizo lingine mwilini. Kweli unaweza kupungua kwa muda mfupi bila hata kutumia nguvu wala kuchoka lakini kitaalamu mwili wa binadamu hautakiwi kupungua ghala kwani haukuongezeka ghafla. Hii inaweza kuathiri mfumo wa ufanyaji kazi katika mwili wako (metabolic activity) kwenye organ mbali mbali kama vile figo, ini, na hata moyo, kwahyo kuwa makini na jali afya yako.
  • Dawa za kupunguza uzito hazitoi suluhisho la kudumu katika mwili wako. Watu wengi wanaotumia haya madawa huwa wanapungua kwa muda mfupi na kurudia tena hali ya mwanzo na hata zaidi. Hii inasababishwa na watumiaji wengi hawafundishwi kubadilisha mitindo ya maisha.
ZIFUATAZO NI NJIA SALAMA NA SAHIHI ZA KUPUNGUZA UZITO.
  • Kula chakula unachokipenda kwa kiwango kidogo (balance diet). Watu wengi wanene wanadhani njia sahihi ya kupunguza uzito ni kujinyima kula chakula unachopenda. Usiache kula kwani unaweza ukanenepa zaidi.
    18581817_10154464013356835_2593990822836116940_n.jpg
  • Usiache kula breakfast kila siku asubuhi.Watu wengi hasa wafanyakazi hawapendi kula breakfast kwa kisingizio cha kuwahi kazini. Hakikisha asubuhi unapata breakfast nzuri ( matunda/tunda, maziwa mboga za majani n.k)
breakfast-benefits.jpg

  • Punguza kula sana (overeating). Unajua kwanini watu wengi wanashindwa kupunguza kula chakula? Ni kwasababu chakula ni kitamu. Ukiweza kujifunza kula kwa wakati na kiasi huwezi kunenepa sana. Usipende kula kila saa kama nguruwe kwasababu umejisikia tu kula, panga ratiba yako ya kula na kwa wakati sahihi, hiyo itakusaidia kutokula ovyo. Kama huwezi kuvumilia bandika vikaratasi kwa ukuta wako/ desk ofisini kwako kama hii;
great-WeightLossMotivation_.jpg

  • Kunywa maji ya kutosha kila siku. Kwa kawaida unatakiwa kunywa maji kwa ujazo wa glass 8 - 12 kwa siku ( 1 -3 lita). Maji yanasaidia sana katika umeng'enyaji wa chakula pia hata tishu, organi na seli za mwili zinatumia maji ili zifanye kazi vizuri.
  • Punguza vinywaji vyenye caffeine kama vile coca na energy drinks, majani ya chai na kahawa. Ceffeine inamadhara makubwa sana mwilini ni pamoja na mfumo wa chakula, inaathiri sana ini. Pia inazuia mwili kutumia virutubisho vingi mwilini.
    18528002_10154461082096835_2753106405794049669_n.jpg
Hakikisha unafanya mazoezi ya kutosha kila siku na siyo kila jumamosi ya mwezi l.o.l . Mazoezi ni njia kubwa na muhimu ya kupunguza uzito. Watanzania wengi hususani wa mijini hawafanyi mazozezi na ndo maana wengi wanavitambi wake kwa waume, hii inasababishwa na mfumo wao wa maisha kutowashawishi kufanya mazoezi japo kuna centre nyingi za mazoezi mijini, Wanapanda magari na vyombo vingine vya usafiri, pia wanakula sana junk foods ( chpsi, mishkaki pizza n.k ), hii hupelekea kuongezeka uzito kutokana na mwili kutopata virutubisho muhimu na kwa wakati. Chips na vyakula vingne kama hvyo vina wanga nyingi na mafuta hivyo kufanya mwili utumie kiasi kidogo cha virutubish hvyo na kuhfadhi hvyo vingne kwa mfumo wa fat/ mafuta.
Ni muhimu kujipa angalau dk 15 za mazoezi asubuhi na dk 15 nyingne jioni, hii itakusaidia kuchoma mafuta yaliyozidi mwilini. Ndyo maana unaona wanamichezo wengi hata wakila kwa kiwango kikubwa hawanenepi ovyo kwasababu wanaunguza calorie nyingi wanazokula kwakufanya mazoezi kila siku.
18402617_10154446499741835_2486436487150853896_n.jpg
18275182_10154434515216835_1514080718833180516_n.jpg


N.B, Mazoezi si jambo la hiyari katika maisha, kila mtu anatakiwa kufanya mazoezi kwa ajili ya afya na muonekano mzuri. Badilisha mtindo wako kuanzia sasa, amua na ufanye kweli.Dawa za kupunguza uzito zinakusaidia kwa muda mfupi na haziwezi kubadili mtindo wako wa maisha.
12360207_10153225687076835_6266222406222571359_n.jpg


*FUATA DONDOO HIZI ILI UISHI KIAFYA.
12647102_10153296861571835_4879907367409611068_n.jpg


*
Kama unaushauri/maoni mengine tofauti na haya tafadhali changia hapa hili tujifunze kuishi kiafya, ASANTENI kwa umakini wenu.
 

Attachments

  • 18581817_10154464013356835_2593990822836116940_n.jpg
    18581817_10154464013356835_2593990822836116940_n.jpg
    132.2 KB · Views: 108
Back
Top Bottom