Profesa Janabi’s Diet: Njia rahisi ya Kupungua na ukaona matokeo ndani ya mwezi mmoja tu

Mung Chris

JF-Expert Member
Sep 12, 2017
3,367
3,778
Profesa Janabi’s Diet leo Katika Kipindi cha Clouds 360 Tarehe 25,April. Mkurugenzi wa Jakaya Kikwete Heart Institute.
Ametoa njia rahisi ya Kupungua na ukaona matokeo ndani ya Mwezi mmoja tu.
Kasema
1. Achana na Vyakula vyote vya ngano, Acha chapati, Mandazi,Mikate, Keki nk
2. Achana na vyakula vyote vya nafaka hata Ugali wa dona achana nao.
3. Acha juisi Hata za Kutengeneza Nyumbani Yaani juisi nachuro

Akaulizwa wewe unakula nini? Mfano kwa siku moja tueleze?
Professor akajibu

“Asubuhi amepiga kahawa akaenda kazini” Mchana ikifika anakula “Mboga za majani na samaki wa kuchoma”.
.
Bado amewaacha watangazaji Mdomo wazi wanamuuliza Umefanya hivyo kwa miaka mingapi?

Jibu lake: Professor janabi amewaambia watangazaji kwamba yeye binafsi hajanywa juisi ya matunda na vinywaji vyovyote vya baridi karibia miaka 10 sasa. Na amesema ni hatari sana unywaji wa juisi za matunda hata yakutengeneza nyumbani. Unamimina sukari ya Fructose nyingi kwa mkao mmoja. Pili hajala mkate na vyakuala vya ngano kwa miaka 3 sasa.

--------------------------------------------------------------------------------------------------
PART 2

Prof Janabi umesema kitu ambacho nimekuwa nikiwaimbia kwaya hapa kila siku na wengi wamekuwa “Wakicharuka sana na Kurusha Matusi”

Aonya Wanywaji wa juisi za Matunda kama Machungwa Maembe kwa kigezo ni NACHURO hawajaweka SUKARI ni Hatari kwa afya.

Mimi binafsi nikinywa juisi na soda nikapiga na wanga aisee nanenepa kwa kasi sana. Kuna kipindi mwili ulitaka kuniponyoka nikafanya tafiti kwa kina “Aina kuu tatu za Sukari duniani zinazopatikana kwenye vyakula asilia”
.
Nikagundua kwamba:
1. Unapokamua juisi ya matunda kama maembe machungwa unatengeneza Syrup ya sukari kama vile Juisi ya kiwandani.
2. Jinsi mwili unavyo chakata Sukari ya Juisi ya Embe nachuro na Juisi ya kiwandani ya embe mchakato (Biochemical pathways) kimwili ni uleule.
3. Duniani kuna aina Tatu za sukari Glukosi inapatikana kwenye Wanga na hata matunda pia, Sukari nyingine inaitwa Fructose ipo kwenye matunda asali, miwa na Tende na sukari nyingine ni Galactose ipo kwenye maziwa.
Sukari iliyo kwenye Tende,Miwa,Matunda huitwa Fructose hii ni Tamu zaidi ya mara mbili ya Glukosi. Ukiramba Fructose kijiko 1 utamu wake unalinganishwa na vijiko 2 vya Glukosi.
4. Sukari ni Sukari hakuna cha “Nachuro wala Kiwandani” Mchakato ni Uleule.
5. Sukari ya Matunda,Tende, Miwa, Unatakiwa Ule kwa kiwango kidogo. Kwa sababu mchakato wake ni kama Pombe Fructose hutumika na Kiungo kimoja tu mwilini INI. Na Unapozidisha Fructose INI huhifadhi sukari hio kama MAFUTA unapata Non Alcoholic Fatty Liver. Kuna wagonjwa wengi tu “Hawanywi Pombe wana Ini limetapakaa mafuta, Wengine Limedumaa mpaka wamepata kisukari “Hepatic insulin resistance” na Mwisho Linakufa kabisa “Liver cirrhosis Fructose induced”.
---------------------------------------------------------------------------------------------
PART 3

Professor Janabi’s Breakfast Lunch and Dinner Meal Plan Kwa siku Moja inakuwa hivi:
No Nafaka , No Ngano, No Sukari , No Juisi Nachuro ,No soda..! Zote hizo ni NO. Kinywaji baridi Chake ni MAJI.
.
1. Asubuhi : Amekunywa Kahawa (Coffee) glasi moja. Na salad ya Matunda Apple na Ndizi mbivu.

2. Lunch: Kipande cha samaki, Mboga za majani na salad hapo Pembeni.

3. DINNER (USIKU):Jioni Kuku, salad na Mboga za majani pia. .
Hajaanza Leo ameanza siku nyingi sana Kuishi hivyo Kwa mujibu wake.
.
Kwa Professor Anakula hivi? Je ina maana Profesa anajitesa?
1. Kwanza anaonekana kufurahia mfumo wake na anawashangaa ambao wana HOFIA kutoweza. Sky Eclat
2. Alianza Mfumo huu baada ya kuona Watu wengi wanavyo hangaika na magonjwa ya moyo huku wakiwa wana maisha mazuri na pesa. Sababu kubwa ni Kutokujua waleje ili kujikinga na magonjwa ya moyo.
3. Kutokana na Utafiti wake akaona Vyakula vya wanga na sukari ni adui namba moja akaacha kabisa na kwa miaka mingi anaishi na afya yake iko FITI. “Hataki na Yeye aje alazwe kitandani akizibuliwa Mishipa yake ya Moyo”.

Anauliza “Ipi gharama zaidi? Kuacha vyakula vya wanga upunguze uzito wako au Kuendelea kula upate unene uliokithiri magonjwa ya moyo tuje tukuzibue kwa milioni 8” ?.

1083213


JK1.jpg
 
Yeye ni Professor mkuu, unajua ni samaki wa ngapi wa kuchoma utakula kwa wiki?
prof hajatoa mbadala wa wanga ila ni hivi vyakula vya wanga na sukari ndivyo viletavyo uzito mkubwa ila vyakula vya protini, mafuta, matunda, mboga ndivyo vilivyo salama zaidi ila kwenye mafuta lazima yawe mafuta salama ambayo yanastahimili moto mkali wakati wa kupika
 
prof hajatoa mbadala wa wanga ila ni hivi vyakula vya wanga na sukari ndivyo viletavyo uzito mkubwa ila vyakula vya protini, mafuta, matunda, mboga ndivyo vilivyo salama zaidi ila kwenye mafuta lazima yawe mafuta salama ambayo yanastahimili moto mkali wakati wa kupika
Kuna mtu aliniambia mchanganyiko wa sukari, wanga na mafuta ni sumu kubwa ambayo ni tamu sana. Nilipiga taswira ya keki
 
alichozungumza kinaukweli kwa asilimia kubwa sana ila swala ambalo hakuliweka bayana ni kwavipi mtu utaweza kukaa bilakusikia njaa muda mrefuu, ni kwamba vyakula vingi vya mafuta na protini ukila usikii njaa kwa muda mrefu mfano ukila karanga,samaki, nyama unakuwa we ni mtu wa maji tuu na njaa inakuwa mbali, pia huwa havipandishi insulin kwa kiwango kikubwa
 
Kuna mtu aliniambia mchanganyiko wa sukari, wanga na mafuta ni sumu kubwa ambayo ni tamu sana. Nilipiga taswira ya keki
swadakta ila sijaelewa vile ameoanisha ila nafahamu sukari wanga ndio vitu vinatutesa sana na kuviacha vyakula vitamu na vyenyesukari huwa ni vigumu kuviacha kama vile teja kuacha unga pia vinatuaminisha hatuwezi ishi bila hivyo vilevile kwa watumia unga anaamini hawezi ishi bila unga, mafuta yanaongeza omega 6 mwwilini ka ni mafuta mabaya
 
swadakta ila sijaelewa vile ameoanisha ila nafahamu sukari wanga ndio vitu vinatutesa sana na kuviacha vyakula vitamu na vyenyesukari huwa ni vigumu kuviacha kama vile teja kuacha unga pia vinatuaminisha hatuwezi ishi bila hivyo vilevile kwa watumia unga anaamini hawezi ishi bila unga, mafuta yanaongeza omega 6 mwwilini ka ni mafuta mabaya
The starting point should be awareness of what carbohydrate does in your body and you get enough of it in your main meals, you don’t need sugar in your tea and coffee.
 
kwa wale ambao tumewahi kuangalia postmortem kitu kinachokuw akwenye mwili wa mtu ambaye ni mnene huwa hakiangaliki ni mafuta tumbo lote, kwenye moyo, kwenye figo. kwenye utumbo mkubwa na mdogo na madaktari wengi wakati wanafanya wanaanzaelezea chanzo cha kifo pia kama alikuwa na tatizo jingine wengi huonekana wanamoyo mkubwa, figo huanza kuwa na matatizo hata kama ilikuwa haijaripotiwa kama ugonjwa, pia maini huw ana kasoro kutokana na fat liver ambayo ni chanzo cha pombe kwahiyo ni swala lakuangalia vyema na kula kwa kulinda afya zetu si mpaka tupate matatizo ndo tuanze kimbizana na madaktari na hosipitali kukikinga ni rahisi ila matibabu ni ghali sana
 
Back
Top Bottom