Kama huna ngozi nene usigombee urais!

Kama huna ngozi nene usigombee urais!

Kuna mambo yanayoendelea sasa hivi hapa nchini ambayo siyaelewi kabisa.

Inapotokea mtu maarufu anapomkosoa huyu rais wetu hadharani au inapotokea hata mtu tu wa kawaida akafanya au kusema kitu fulani ambacho kinaonekana kama kinamkosoa Rais Magufuli basi mtu huyo ataanza kuandamwa andamwa na hata kukamatwa.

Rejeeni habari za yule dogo wa UDSM alipokamatwa kwa sababu ya alichokifanya kuhusu majengo ya mabweni mapya ya wanafunzi chuoni hapo. Rejeeni suala na Nape kutishiwa na bastola mchana kweupe. Rejeeni suala la mbunge Bashe kusumbuliwa na polisi au sijui usalama wa taifa wale. Rejeeni suala la Lissu kukamatwa kamatwa na kuwekwa rumande kisa katumia lugha kali dhidi ya Magufuli.

Kwenye nchi za kidemokrasia, kama tunavodai na sisi nchi yetu iko hivyo, suala la viongozi kukosolewa, kudhihakiwa, kutukanwa, na kadhalika, ni jambo la kawaida sana.

Tazama kote duniani kwenye demokrasia na hayo mambo utayaona.

Sasa kwa nini hapa kwetu huyu rais wetu akisemwa vibaya huyo mtu aliyemsema vibaya anaanza kusumbuliwa?

Askofu Kakobe sasa hivi tumesikia habari kuwa eti atakamatwa kisa eti kadiriki kumkosoa rais.

Hivi kumkosoa rais au hata kumkebehi na kumdhihaki ni kosa kwenye nchi hii?

Kwani huyu rais wetu wakati anagombea huo urais alikuwa na matarajio gani labda? Kwamba akishatangazwa kuwa yeye ndo mshindi basi kila mtu ndo atakubaliana naye na kumuunga mkono kwenye kila kitu? Hilo kamwe haliwezekani na halitowezekana Tanzania hii.

Labda linawezekana tu huko Korea Kaskazini ingawa hata huko sidhani kama watu wote wanamuunga mkono huyo Kiduku.

Nawashauri CCM waunde kitengo cha ‘War room’ mahsusi kwa kujibu mapigo ki-hoja na kuacha kutumia vitisho vya vyombo vya dola kujibu mapigo kwa kutishia watu.

Wewe ndo uwambie ccm wenzio kuwa wanachofanya ni upumbavu!! Ni nani wewe usiepingwa Kwa hoja. Hata baba wa familia anaweza kupingwa kwa hoja nyumbani kwake na wanae anaowalisha kilasiku kama atafanya maamuzi ya hovyo; sembuse Mtu aliyechaguliwa kwa kura, tena sio na watanzania wote. Huu ni ujuha, ulimbukeni na ulevi wa madaraka.
 
Ndiyo hivyo. Hutakiwi kujitangaza jina halafu ukawa unabishana na watu ambao hawajulikani majina halafu ukajiona mjanja kwa sababu huna woga.

Kama vile ambavyo hutakiwi kufunga macho halafu ukavuka barabara yenye magari mengi huku umefunga macho halafu ukatamba eti huna woga.
Sawa Mkuu. Lakini, maongezi yetu yalikuwa more casual. Umepeleka hoja mbali
 
Vijana wa kitanzania bwana; tumejivika akili ya kutoelewa. Nani alikuambiwa atakamatwa. Kwanza kwenda kutoa maelezo ya kauli ulizozitoa ni kukamatwa. Mbona ni jambo la kawaida. Lowasa alienda kutoa maelezo juu ya kauli yake; Katibu wa chadema alienda kutoa maelezo juu ya kauli aliyoitoa. Je hili ni geni?. lazima ifikie wakati mtoke katika hayo matongotongo mliyojivika na mje na ajenda zenye tija.
Wewe hujiulizi hata swali LA kawaida kwamba kwa nini ukimkosoa raisi unapelekwa kwenda kuhojiwa kwanini?
 
Umetukana wote ambao hatujaweka majina yetu halisi hapa kwamba ni waoga.

Your casual insult is more insulting than a deliberate one.

It is more deeply rooted in your psyche.
Mkuu, I was joking. Please, do not take it seriously. My apology Sir/Madam!
 
Rais kukosolewa ni sawa. Kukosoa kuwe kwa staha na kunakotoa njia mbadala. Lakini, kumdhihaki, kumtukana na kumkejeli Rais hakutavumiliwa. Watakaofanya hivyo wote watashughulikiwa kwa mujibu wa Sheria.
Anayetafsiri kuwa Rais kakosolewa kwa staha au laa ni hao hao wanaccm wenzake.

Hebu nieleze wakili Mselewa, hivi Baba Askofu kumwambia Rais atubu dhambi yake ya kutaka kuigeuza nchi hii ya chama kimoja wakati Katiba ya nchi yetu inasema hii nchi ni ya vyama Vingi, hivi hilo nalo ni kosa hadi Polisi wajihangaishe kwenda kumkamata na kumhoji??

Mbona hao hao maaskofu wanapotamka kuwa Magufuli ni Zawadi toka kwa Mungu, Mbona mapolisi hawahangaiki kuwakamata watu wa aina hiyo??
 
Umetukana wote ambao hatujaweka majina yetu halisi hapa kwamba ni waoga.

Your casual insult is more insulting than a deliberate one.

It is more deeply rooted in your psyche.

Mazee unakaba hadi penati?

Utamfanya mtani wangu huyo akimbie hahahaaa.

Hapo alipo tu bado anaitafuta sheria inayokataza rais kudhihakiwa....
 
Rais kukosolewa ni sawa. Kukosoa kuwe kwa staha na kunakotoa njia mbadala. Lakini, kumdhihaki, kumtukana na kumkejeli Rais hakutavumiliwa. Watakaofanya hivyo wote watashughulikiwa kwa mujibu wa Sheria.

You are probably right. Lakini unasahau kwamba there is a fine line between kukosoa na kudhihaki au kukejeli au kutukana. Mtu anaweza kukosolewa lakini akatafsiri kuwa ametukanwa na hivyo kutoa adhabu. Ukianza kujifanya hutakubali kutukanwa au kukejeliwa, mara nyingi unasema hutaki kukosolewa. Na ndio msingi wa hoja ya Nyani Ngabu. As a lawyer (kama unavyodai) you should know better. Kwa kuwa kukosoa na kutukana are open to interpretation, na kwa kuwa lengo ni kutoa uhuru kamili kwa watu kutoa maoni yao, ni muhimu sana kuhakikisha kuwa hatuuzi uhuru wetu kwa watawala.
 
Kuna wakuati Nyani Ngabu ulikuwa umejitoa ufahamu kwa ajili ya huyu poyi wako. Naona umeanza kurejewa na akili zako nilizozizoea. Safi sana , karibu kwenye ulimwengu wa watu wenye kuelewa. Bado Mzee Mwanakijiji . huyu naye ameweka busara zake zote rehani , si yule tuliyemzoea wakati wa JK. Au tatizo ilikuwa JK, na siyo uongozi wake?
Huyo babu anavizia uteuzi ikiwa mungu wao akitoka madarakani pasipo kuteuliwa utamuona atakavyokuwa Mkali jinga huyo
 
Ac

heni kutengeneza maneno ni lini Rais alisema maneno hayo kuwa asikosolewe , lakini ukosoe kwa stahaa

Hukusikia alivyosema yeye hajaribiwi? Kukosoa kwa staha nani anayeku-define na ndiyo kukoje? Maana kusema ukweli tu, siku hizi kunaitwa uchochezi. Sasa kama kuambiwa aache kutumia vyombo vya dola, kujaribu kuua watu, kuteka watu, kukamata watu wanaomkosoa, ndiyo kukosa staha, basi sawa.
 
Una akili timamu kweli wewe?
Freedom of expression is recognized as a human right under article 19 of the Universal Declaration of Human Rights and recognized in international human rights law in the International Covenant on Civil and Political Rights (ICCPR). Article 19 of the UDHR states that "everyone shall have the right to hold opinions without interference" and "everyone shall have the right to freedom of expression; this right shall include freedom to seek, receive and impart information and ideas of all kinds, regardless of frontiers, either orally, in writing or in print, in the form of art, or through any other media of his choice". The version of Article 19 in the ICCPR later amends this by stating that the exercise of these rights carries "special duties and responsibilities" and may "therefore be subject to certain restrictions" when necessary "[f]or respect of the rights or reputation of others" or "[f]or the protection of national security or of public order (order public), or of public health or morals".[6]
 
Nakumbuka jirani zetu kenya kuna mama alimwambia uhuru kinyata kua ni mshenzi,tena hasharani.siku sikia watu wasiojulikana wakimpoteza.

Zawadi ya kadi ya Christmas ndo lilikua jibu la kinyata kwa mama yule,na maisha yalisonga na uhuru bado ni rais wa kenya.

Wasipoteze muda bure,nachotaka ni viwanda mia kila mkoa na sisi wa tabora tupate upendeleo ili viwe mia mbili.
Nahuko kwenu cccm inavyoendelea kuabudiwa kama mungu mtangoja sana
 
Back
Top Bottom