Kama huna ngozi nene usigombee urais!

Kama huna ngozi nene usigombee urais!

Hao wanaolalama JPM hataki kushauriwa kama ingewezekana tuwape ikulu wiki tu mngeona! Wengine njia zao kutafuta ikulu kila aliyekuwa kizingiti alishughulikiwa directly au indirectly ....wangefanya hayo hayo kama tungewapa nchi. Kukosoa tukosoe lakini staha muhimu pia ....yule ni Rais wa Tanzania ....ndio alama ya nchi ....lazima mipaka iwepo kidogo ....msifikiri uhuru uliopo Marekani uliibuka tu ....walipitia safari ndefu .....hii ni Africa lazima ujue mipaka yako (hapa sizungumzii uoga bali kujenga hoja kwa staha) .....akina Prof Shivji wanakosoa kila siku, Generali Ulimwengu anakosoa, wengi wanakosoa lakini wakijua mipaka .....hakuna atakayekufundisha mipaka ....ni wewe kujua staha inaanza na kuishia wapi ....mtu akikamatwa kwa hoja zake zenye staha umma utanyanyuka ....mfano ni Askofu wa jimbo la Karangwe ....tuwe na staha ...

Kakobe alimkosea staha rais?
 
[emoji216][emoji216][emoji216][emoji216][emoji216][emoji216][emoji216][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125]
 
878f6387a1e0c410dd3269053243602c.jpg


Mkuu umenishangaza sana eti sheria gani inakataza kumkejeli Rais au kumdhihaki.Punguza ushabiki maandazi

Hicho ulichoweka ndo sheria inayokataza kumkejeli rais?
 
Rais kukosolewa ni sawa. Kukosoa kuwe kwa staha na kunakotoa njia mbadala. Lakini, kumdhihaki, kumtukana na kumkejeli Rais hakutavumiliwa. Watakaofanya hivyo wote watashughulikiwa kwa mujibu wa Sheria.
Hata Yesu alikosolewa huyu wenu ye ni nani, kumwambia atubu tena kanisani ni kosa gani au si staha? Wekeni maneno mliyotaka aambiwe basi mtukufu wenu.
 
Kuna mambo yanayoendelea sasa hivi hapa nchini ambayo siyaelewi kabisa.

Inapotokea mtu maarufu anapomkosoa huyu rais wetu hadharani au inapotokea hata mtu tu wa kawaida akafanya au kusema kitu fulani ambacho kinaonekana kama kinamkosoa Rais Magufuli basi mtu huyo ataanza kuandamwa andamwa na hata kukamatwa.

Rejeeni habari za yule dogo wa UDSM alipokamatwa kwa sababu ya alichokifanya kuhusu majengo ya mabweni mapya ya wanafunzi chuoni hapo. Rejeeni suala na Nape kutishiwa na bastola mchana kweupe. Rejeeni suala la mbunge Bashe kusumbuliwa na polisi au sijui usalama wa taifa wale. Rejeeni suala la Lissu kukamatwa kamatwa na kuwekwa rumande kisa katumia lugha kali dhidi ya Magufuli.

Kwenye nchi za kidemokrasia, kama tunavodai na sisi nchi yetu iko hivyo, suala la viongozi kukosolewa, kudhihakiwa, kutukanwa, na kadhalika, ni jambo la kawaida sana.

Tazama kote duniani kwenye demokrasia na hayo mambo utayaona.

Sasa kwa nini hapa kwetu huyu rais wetu akisemwa vibaya huyo mtu aliyemsema vibaya anaanza kusumbuliwa?

Askofu Kakobe sasa hivi tumesikia habari kuwa eti atakamatwa kisa eti kadiriki kumkosoa rais.

Hivi kumkosoa rais au hata kumkebehi na kumdhihaki ni kosa kwenye nchi hii?

Kwani huyu rais wetu wakati anagombea huo urais alikuwa na matarajio gani labda? Kwamba akishatangazwa kuwa yeye ndo mshindi basi kila mtu ndo atakubaliana naye na kumuunga mkono kwenye kila kitu? Hilo kamwe haliwezekani na halitowezekana Tanzania hii.

Labda linawezekana tu huko Korea Kaskazini ingawa hata huko sidhani kama watu wote wanamuunga mkono huyo Kiduku.

Nawashauri CCM waunde kitengo cha ‘War room’ mahsusi kwa kujibu mapigo ki-hoja na kuacha kutumia vitisho vya vyombo vya dola kujibu mapigo kwa kutishia watu.
Kuna wakuati Nyani Ngabu ulikuwa umejitoa ufahamu kwa ajili ya huyu poyi wako. Naona umeanza kurejewa na akili zako nilizozizoea. Safi sana , karibu kwenye ulimwengu wa watu wenye kuelewa. Bado Mzee Mwanakijiji . huyu naye ameweka busara zake zote rehani , si yule tuliyemzoea wakati wa JK. Au tatizo ilikuwa JK, na siyo uongozi wake?
 
Nakumbuka jirani zetu kenya kuna mama alimwambia uhuru kinyata kua ni mshenzi,tena hasharani.siku sikia watu wasiojulikana wakimpoteza.

Zawadi ya kadi ya Christmas ndo lilikua jibu la kinyata kwa mama yule,na maisha yalisonga na uhuru bado ni rais wa kenya.

Wasipoteze muda bure,nachotaka ni viwanda mia kila mkoa na sisi wa tabora tupate upendeleo ili viwe mia mbili.
 
Kuna wakuati Nyani Ngabu ulikuwa umejitoa ufahamu kwa ajili ya huyu poyi wako. Naona umeanza kurejewa na akili zako nilizozizoea. Safi sana , karibu kwenye ulimwengu wa watu wenye kuelewa. Bado Mzee Mwanakijiji . huyu naye ameweka busara zake zote rehani , si yule tuliyemzoea wakati wa JK. Au tatizo ilikuwa JK, na siyo uongozi wake?

Wewe huna akili ya kuweza kunielewa mtu kama mimi.
 
Rais kukosolewa ni sawa. Kukosoa kuwe kwa staha na kunakotoa njia mbadala. Lakini, kumdhihaki, kumtukana na kumkejeli Rais hakutavumiliwa. Watakaofanya hivyo wote watashughulikiwa kwa mujibu wa Sheria.
Mbona unajitoa ufahamu ndugu? Kakobe kaongea lipi Baya
 
Back
Top Bottom