Hakikwanza
JF-Expert Member
- Dec 11, 2010
- 4,049
- 1,022
Shida yetu Watanzania ni kuwa na kiwango kikubwa sana cha watu wenye uwezo kidogo sana wa kufikiri.Hivyo tuna kazi kubwa sana mbele yetu
Kukosa nguvu ya kuzuia hakukuzuii kujiondoa kwenye list ya wanayoyapitishaHuenda wakati huo hakuwa na nguvu ya kuzuia kama aliyonayo sasa
Tupe mifano hai ya advancement yoyote kijamii, kiuchumi au hata kisiasa iliyofikiwa na nchi kama Ghana, Zambia nk ktk Afrika baada ya mageuzi ya serikali zao.Hii ni Africa experience inaonyesha wazi hata ukibadili serikali kupitia vyama ni sawa tu na kimimina mvinyo wa zamani ktk chupa mpya ni mchakato wa kubadili rangi za mafisadi tu.Ndugu zangu,
Katika mambo yanayotugharimu watanzania ni msemo wa "yaliyopita si ndwele tugange yajao"
Kumekuwa na makosa mengi ya kuligharimu taifa yakifanywa na viongozi ambao tumekuwa tukiwapa dhamana ya kuongoza nchi yetu, lakini sijawahi kuona wakiwajibishwa.
Wanaingia, wanatawala wanaharibu wanaondoka anayekuja vilevile. Katika mambo ambayo nilimtegemea sana JPM katika ukweli wake ni kuwa mkweli kama ambavyo amejinadi toka wakati wa kampeni kuhusu kiini cha tatizo kuwa ni mikataba mibovu watangulizi wake kwa yote waliyoingia. Badala yake na yeye analalamika tu, fikiria kama ingekuwa wapinzani ndio walitawala miaka mitano ilopita, kama namuona Rais wangu ambavyo angewafanya.
Suala la mchanga wa dhahabu kwa mfano, hivi Rais wa awamu ya nne na tano wanachomokaje hapa? Gazeti la uhuru la leo limesema ukweli kama linavyojinadi "ukweli daima", kwamba makontena ya mchanga yameshauzwa nje kuanzia 2001 hadi 2016. Hii inamaana wakati wa utawala wa Rais Mkapa na Kikwete, maana yake kwa kipindi chote hiki tumeongozwa na ama na watu kwa maslahi yao binafsi au kwa kiburi cha "Tutawala milele" hivyo tuijitajirishe tu. Kama hadi kufikia gazeti la uhuru kuandika haya mangapi yanayopigiwa kelele za ukweli mfano escrow hayaandikwi?
Watanzania tunasubiri nini? Tubadilishe watu wa kutuongoza na kusimamia kodi zetu.
Nilikuwa na imani na JPM lakini simwelewi kabisa, analalamika kuhusu mchanga kwanini asiseme kweli kama lilivyoandika uhuru kwamba serikali za chama chake ndizo zilizotufikisha hapa yeye akiwa waziri? Cha ajabu hata alikuwa haoni wakti huo angetusaidia kutoa hoja binafsi labda.
Kama nguvu nyingi inatumika kuwashughulikia akina Mbowe anayedaiwa kutolipa kodi, Manji anayedaiwa kuajiri wageni bila vibali, wanaokosoa serikali na kuhoji mambo mbalimbali ya viongozi, wanaokwenda tofauti na chama tawala kwa nini tusitumie nguvu hiyo pia kuwawajibisha viongozi wetu hawa waliotutia hasara kwa miaka karibia 17 sasa ili hata yeye na wajao wajue wakiharibu watawajibishwa?
Jamani, tusiogope kubadilisha serikali na kuwapa wapinzani nchi tuwe kama Ghana, Zambia etc, sioni tofauti ya uwezo wa wanaotwala sasa na wapinzani, naweza sema wako watu makini zaidi upande wa upinzani, mfano Zitto, Tundu Lissu just to mention few. Kufanya hivi kutaleta discipline kwa kila tunaowapa dhamana, wataongoza kwa matakwa ya tuliowachagua wakijua hawana uhakika wa kutawala tena na pengine kushtakiwa kama wakiharibu na sio kwa fikra zao kama ilivyo sasa.
Wapenzi wa vyama msichafue hali ya hewa please.
View attachment 490550
Andika kizalendoumeandika kishabiki sana ,
JPM atatufanyia kazi nzuri tu madam ameshaianza kazi tumpe mudaHaya ndio matatizo ya kuchagua marais masikini. Wanawaza matumbo yao tu, ndio maana Marekani inabidi uwe na mkwanja wa maana ndo ugombee kwenda jumba jeupe.
Bunge la safari hii lina mambo km matatu hivi motomoto,
1. Bashite
2. Mchanga wa dhahabu
3. Bajeti
Lkn Ooooh bahati mbaya bunge haliko mubashara, kila kitu kitafanyika gizan,
Kwamba Indonesia wameamua kujenga mitambo wenyewe ni sawa lakini usisahau walitoa grace period... hawakumka tu na kusema from now; hakuna ku-export mchanga!!!Kupelekwa nje sio tatizo, South africa,Chile,Indonesia na na nchi nyingi duniani (exportation of cupper concentrate inaonekana ni grobal practice sio habari)zinapeleka japo nyingine kama Indonesia waliamua kuchukua uamuzi ambao kauchukua leo Rais wetu kuwa wachenjulie hapa ambao tunaupongeza.
Kitu kipya hapo kwenye hiyo habari ni kwamba WANAUUZA HUO MCHANGA HAWACHENJUI KAMA TULIVYOAMBIWA ILI WANACHOKIPATA NDIO WAUZE.
Ulimsikiliza ZZK au umeongea tu?! Kwenye suala hili ZZK ndo ameongea jambo la msingi sana!!! Alichosema ZZK ni:Kwanza, naanza kwa kusikitika kuwa muondoe kabisaaa ZZK, maana amesema mchanga tuendelee kuuzwa/ kusafirishwa nje na kusema wawekezaji wameanza kupata hasara.
Tatizo, Sasa la mchanga kupelekwa nje ni kuwa nchi kama japani ni visiwa hawana maeneo ya kupata mchanga na mawe ya kujengea barabara na majengo kwa hiyo Tanzania ikajitoa ufahamu kuwapa mchanga na mawe hayo kwa kisingizia vinu vya kuchembua/kuchakata dhahabu.
Pia,uchumi tumbo wa viongozi wote kuanzia 1995 hadi 2015.
Tena, bunge la wimbo wa ndiyoooooooo, na kibwagizo cha siyoo!
Katiba uchwara kwamba, wastaafu watarindwa na hakuna kushitakiwa .
Mwisho, wasomi vyeti na siyo akili na upeo kupanuka nao wanatutesa sana, mfano, huyu wa umeme, mwaka Jana alituaminisha kuwa umeme wa gesi nchi nzima hadi tutauza nje ya nchi, juzi wanakuja na ngojera bila kiitikio kuwa Ethiopia itatuuzia umeme wa maji.
Vilaza ni wengi sana.
halikueleweka sasa ilikuwaje mkaporomoka kutoka 84% 2005 mpaka 57% 2015 ?? na upinzani from 20% 2005 mpaka 40% 2015 (NEC)Hao ambao angalau walitegemewa kuwa ndio mbadala wa CCM wakaenda kubadilishia gia angani, wakamchukua mtu ambaye ni sehemu ya upigaji wa miaka mingi.
Tatizo lipo hapo kwenye ukweli kwamba hata wa nje ya CCM hawana mikakati sahihi ya kuweza kuja na wazo mbadala na likaeleweka kwa wananchi.
Unaposema mabadiliko huku ukirusha mikono hewani ni kazi bure kama huwezi kujielezea vyema na ukaeleweka, kwa kuionyesha jamii ni namna gani ulivyo na tofauti na kile kinachowakera baadhi ya watanzania.
lissu anaubongo mzuri kuliko phdeeWee mzima kweli !? Yaani nchi umpe Tundu Lissu !? Nenda katibiwe kwanza .