Kama gazeti la Uhuru limeandika, tunasubiri nini?

gillard

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
227
165
Ndugu zangu,
Katika mambo yanayotugharimu watanzania ni msemo wa "yaliyopita si ndwele tugange yajao"
Kumekuwa na makosa mengi ya kuligharimu taifa yakifanywa na viongozi ambao tumekuwa tukiwapa dhamana ya kuongoza nchi yetu, lakini sijawahi kuona wakiwajibishwa.

Wanaingia, wanatawala wanaharibu wanaondoka anayekuja vilevile. Katika mambo ambayo nilimtegemea sana JPM katika ukweli wake ni kuwa mkweli kama ambavyo amejinadi toka wakati wa kampeni kuhusu kiini cha tatizo kuwa ni mikataba mibovu watangulizi wake kwa yote waliyoingia. Badala yake na yeye analalamika tu, fikiria kama ingekuwa wapinzani ndio walitawala miaka mitano ilopita, kama namuona Rais wangu ambavyo angewafanya.

Suala la mchanga wa dhahabu kwa mfano, hivi Rais wa awamu ya nne na tano wanachomokaje hapa? Gazeti la uhuru la leo limesema ukweli kama linavyojinadi "ukweli daima", kwamba makontena ya mchanga yameshauzwa nje kuanzia 2001 hadi 2016. Hii inamaana wakati wa utawala wa Rais Mkapa na Kikwete, maana yake kwa kipindi chote hiki tumeongozwa na ama na watu kwa maslahi yao binafsi au kwa kiburi cha "Tutawala milele" hivyo tuijitajirishe tu. Kama hadi kufikia gazeti la uhuru kuandika haya mangapi yanayopigiwa kelele za ukweli mfano escrow hayaandikwi?

Watanzania tunasubiri nini? Tubadilishe watu wa kutuongoza na kusimamia kodi zetu.
Nilikuwa na imani na JPM lakini simwelewi kabisa, analalamika kuhusu mchanga kwanini asiseme kweli kama lilivyoandika uhuru kwamba serikali za chama chake ndizo zilizotufikisha hapa yeye akiwa waziri? Cha ajabu hata alikuwa haoni wakti huo angetusaidia kutoa hoja binafsi labda.

Kama nguvu nyingi inatumika kuwashughulikia akina Mbowe anayedaiwa kutolipa kodi, Manji anayedaiwa kuajiri wageni bila vibali, wanaokosoa serikali na kuhoji mambo mbalimbali ya viongozi, wanaokwenda tofauti na chama tawala kwa nini tusitumie nguvu hiyo pia kuwawajibisha viongozi wetu hawa waliotutia hasara kwa miaka karibia 17 sasa ili hata yeye na wajao wajue wakiharibu watawajibishwa?

Jamani, tusiogope kubadilisha serikali na kuwapa wapinzani nchi tuwe kama Ghana, Zambia etc, sioni tofauti ya uwezo wa wanaotwala sasa na wapinzani, naweza sema wako watu makini zaidi upande wa upinzani, mfano Zitto, Tundu Lissu just to mention few. Kufanya hivi kutaleta discipline kwa kila tunaowapa dhamana, wataongoza kwa matakwa ya tuliowachagua wakijua hawana uhakika wa kutawala tena na pengine kushtakiwa kama wakiharibu na sio kwa fikra zao kama ilivyo sasa.

Wapenzi wa vyama msichafue hali ya hewa please.
uhuru-Leo-03-04-2017.jpg
 
Kupelekwa nje sio tatizo, South africa,Chile,Indonesia na na nchi nyingi duniani (exportation of cupper concentrate inaonekana ni grobal practice sio habari)zinapeleka japo nyingine kama Indonesia waliamua kuchukua uamuzi ambao kauchukua leo Rais wetu kuwa wachenjulie hapa ambao tunaupongeza.
Kitu kipya hapo kwenye hiyo habari ni kwamba WANAUUZA HUO MCHANGA HAWACHENJUI KAMA TULIVYOAMBIWA ILI WANACHOKIPATA NDIO WAUZE.
 
Aliyelishikia bango apewe mawazo ya namna ya kulimalimaliza hili, na sio kulia lia na kubadili serikali. kwasaa tuangalie lililo mbele yetu hilo la reform tusubiri muda ufike. Masuala ya nchanga sikuyajua mwanzo mpaka mzee alipozuia makontena, so sion kakosea wapi kwenye hili
 
Bunge la safari hii lina mambo km matatu hivi motomoto,

1. Bashite
2. Mchanga wa dhahabu
3. Bajeti

Lkn Ooooh bahati mbaya bunge haliko mubashara, kila kitu kitafanyika gizan,
Bro na swala la Lugumi limepita hivi hivi kwa kweli sioni jipya ndani ya CCM.Ni kila anaekuja anakuja kula na kuondoka.Akija mwengine analinda mwenzake aliyeondoka.Ndiyo maana wanatumia nguvu kubwa kurudi madarakani.Kumbuka kauli ya Rais Magufuli kwa Kikwete kapumzike nitakulinda,je atamlinda kwa nini,anashida gani hadi ampe ahadi ya kumlinda mtu ambaye ni safi?
 
Wewe ndio hukuyajua, yeye aliyajua na alikuwa sehemu ya cabinet iliyofikia maamuzi haya. Au wewe ndio nani?
 
Ndugu zangu,
Katika mambo yanayotugharimu watanzania ni msemo wa "yaliyopita si ndwele tugange yajao"
Kumekuwa na makosa mengi ya kuligharimu taifa yakifanywa na viongozi ambao tumekuwa tukiwapa dhamana ya kuongoza nchi yetu, lakini sijawahi kuona wakiwajibishwa.

Wanaingia, wanatawala wanaharibu wanaondoka anayekuja vilevile. Katika mambo ambayo nilimtegemea sana JPM katika ukweli wake ni kuwa mkweli kama ambavyo amejinadi toka wakati wa kampeni kuhusu kiini cha tatizo kuwa ni mikataba mibovu watangulizi wake kwa yote waliyoingia. Badala yake na yeye analalamika tu, fikiria kama ingekuwa wapinzani ndio walitawala miaka mitano ilopita, kama namuona Rais wangu ambavyo angewafanya.

Suala la mchanga wa dhahabu kwa mfano, hivi Rais wa awamu ya nne na tano wanachomokaje hapa? Gazeti la uhuru la leo limesema ukweli kama linavyojinadi "ukweli daima", kwamba makontena ya mchanga yameshauzwa nje kuanzia 2001 hadi 2016. Hii inamaana wakati wa utawala wa Rais Mkapa na Kikwete, maana yake kwa kipindi chote hiki tumeongozwa na ama na watu kwa maslahi yao binafsi au kwa kiburi cha "Tutawala milele" hivyo tuijitajirishe tu. Kama hadi kufikia gazeti la uhuru kuandika haya mangapi yanayopigiwa kelele za ukweli mfano escrow hayaandikwi?

Watanzania tunasubiri nini? Tubadilishe watu wa kutuongoza na kusimamia kodi zetu.
Nilikuwa na imani na JPM lakini simwelewi kabisa, analalamika kuhusu mchanga kwanini asiseme kweli kama lilivyoandika uhuru kwamba serikali za chama chake ndizo zilizotufikisha hapa yeye akiwa waziri? Cha ajabu hata alikuwa haoni wakti huo angetusaidia kutoa hoja binafsi labda.

Kama nguvu nyingi inatumika kuwashughulikia akina Mbowe anayedaiwa kutolipa kodi, Manji anayedaiwa kuajiri wageni bila vibali, wanaokosoa serikali na kuhoji mambo mbalimbali ya viongozi, wanaokwenda tofauti na chama tawala kwa nini tusitumie nguvu hiyo pia kuwawajibisha viongozi wetu hawa waliotutia hasara kwa miaka karibia 17 sasa ili hata yeye na wajao wajue wakiharibu watawajibishwa?

Jamani, tusiogope kubadilisha serikali na kuwapa wapinzani nchi tuwe kama Ghana, Zambia etc, sioni tofauti ya uwezo wa wanaotwala sasa na wapinzani, naweza sema wako watu makini zaidi upande wa upinzani, mfano Zitto, Tundu Lissu just to mention few. Kufanya hivi kutaleta discipline kwa kila tunaowapa dhamana, wataongoza kwa matakwa ya tuliowachagua wakijua hawana uhakika wa kutawala tena na pengine kushtakiwa kama wakiharibu na sio kwa fikra zao kama ilivyo sasa.

Wapenzi wa vyama msichafue hali ya hewa please.
View attachment 490550
Wee mzima kweli !? Yaani nchi umpe Tundu Lissu !? Nenda katibiwe kwanza .
 
Bunge la safari hii lina mambo km matatu hivi motomoto,

1. Bashite
2. Mchanga wa dhahabu
3. Bajeti

Lkn Ooooh bahati mbaya bunge haliko mubashara, kila kitu kitafanyika gizan,
Nenda pale bungeni kuna spika wameweka nje ukasikilize yote
 
Bro na swala la Lugumi limepita hivi hivi kwa kweli sioni jipya ndani ya CCM.Ni kila anaekuja anakuja kula na kuondoka.Akija mwengine analinda mwenzake aliyeondoka.Ndiyo maana wanatumia nguvu kubwa kurudi madarakani.Kumbuka kauli ya Rais Magufuli kwa Kikwete kapumzike nitakulinda,je atamlinda kwa nini,anashida gani hadi ampe ahadi ya kumlinda mtu ambaye ni safi?
Mkuu sahau kuhusu Lugumi,

Alishasema hajaja kufukua makaburi,

Na hapangiwi cha kufanya, vumilia tu
 
Hao ambao angalau walitegemewa kuwa ndio mbadala wa CCM wakaenda kubadilishia gia angani, wakamchukua mtu ambaye ni sehemu ya upigaji wa miaka mingi.

Tatizo lipo hapo kwenye ukweli kwamba hata wa nje ya CCM hawana mikakati sahihi ya kuweza kuja na wazo mbadala na likaeleweka kwa wananchi.

Unaposema mabadiliko huku ukirusha mikono hewani ni kazi bure kama huwezi kujielezea vyema na ukaeleweka, kwa kuionyesha jamii ni namna gani ulivyo na tofauti na kile kinachowakera baadhi ya watanzania.
 
Back
Top Bottom