Kama Eva asingekula tunda la mti wa kati

Kama Eva asingekula tunda la mti wa kati

Ijumaa Khareem....!

Naandika haya Leo hii kwakuwa kwakuwa Eva alikula tunda la mti wa kati mti wa UJUZI wa MEMA na MABAYA.

Eva hakujilia tu hilo tunda bali ni kwa ushawishi wa nyoka.... Na kamwe hakuwahi kuhangaika nalo kwa kuwa Mungu mwenyenzi yote alikuwa keshakataza kabisa matumizi ya matunda ya huo mti wa kati mti wa Ujuzi wa mema na mabaya. Haya ndio maelezo ya kidini katika ukristo.

Kuna maswali mubashara ya kujiuliza hapa;

- Kwanini kiumbe nyoka? Na si kingine chochote?
- Kwanini kiumbe nyoka hakumfuata Adam?
- Kwanini Eva baada ya kula na kuliona lile tunda linafaa kwa chakula hakuhisi tofauti yoyote mpaka alipompa Adam akala ndio wakajihisi wako uchi?
- Ni nani aliwafunulia siri ya wao kuwa uchi?

Haya maswali yatachukua Karne nyingi kuja kupata majibu mubashara, lakini dunia ipo hapa ilipo Leo! Ipo hivi ilivyo leo kutokana na kile kilichotokea Eden. Nje ya hapo mambo yangekuwa tofauti kabisa.

Inawezekana kabisa Adam na Eva wangeishi pale milele na pengine RACE ya Africa na waafrika tusingekuwepo? Kutokana na picha za wazungu Adam na Eva hawakuwa weusi... Na dunia isingekuwa hivi ilivyo leo.

Kuna dhana zinazopingwa sana na hii pengine ni kutokana na kukosekana kwa ithibati japo za kimaandishi kwamba nje ya Eden huko mbali duniani kulikuwa na viumbe wengine waliofanana na wale wa Eden. Lakini hili linapingwa kwa nguvu na yale maneno ya kwenye Bible kuwa Mungu ndie aliyeumba dunia hii na vingine vyote vilivyomo.

Tunaitwa kizazi cha nyoka je ni sisi wote ama ni wale tu waliokuwa Eden na vizazi vyake? Lakini Kwanini kizazi cha nyoka?..

Ni mkanganyiko tupu lakini bado nazidi kujiuliza kama Eva kwa ushawishi wa nyoka asingekula lile tunda ingekuwaje! Leo hii??? Ama kama angekula peke yake bila kumgaia Adam ingekuwaje? Je story ya Lilieth ingejirudia?

Kuna mengi bado hatuyajui.

Sent from my INFINIX-X551 using JamiiForums mobile app
Hizi mambo bana kama una imani ndogo unaweza ukadhani ni story tu za vijiweni. Ukitumia akili yako zaidi na sio ya kuazimwa utafikia mahali tu uone hii story ina walakini. Sema sababu ndo maandiko yanasema hivyo bas wacha tukubaliane nayo tu.
 
Kwanini kiumbe nyoka? Na si kingine chochote?

::: Shetani aliamua kumtumia Nyoka kwa sababu alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote
-Mwanzo 3:1 Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya BWANA Mungu....

Nimesema Shetani alimtumia Nyoka kwa Sababu ;
- Ufunuo wa Yohana 12:9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.

Shetani angeweza kutumia kinywa cha Mnyama yoyote kupeleka maana yeye na Mungu wananguvu hiyo .

Ukisoma na Maandiko utaona kuna wakati Mwenyezi Mungu alitumia kinywa cha PUNDA kufikisha ujumbe kwa BAALAM
-
Hesabu 22:28 BWANA akakifunua kinywa cha yule punda, naye akamwambia Balaamu, Nimekutenda nini, hata ukanipiga mara tatu hizi?
Hesabu 22:29 Balaamu akamwambia punda; Kwa sababu umenidhihaki; laiti ningekuwa na upanga mkononi mwangu ningekuua sasa hivi.
Hesabu 22:30 Yule punda akamwambia Balaamu, Je! Mimi si punda wako, nawe umenipanda maisha yako yote hata leo? Nimezoea kukutenda hayo? Akasema, La!

- Kwanini kiumbe nyoka hakumfuata Adam?

::: Ni kweli nyoka hakumfuata Adamu, sababu ni kwamba ,Adamu ndiye aliyepewa maagizo kuhusu huo mti kabla hata ya kufanyiwa Msaidizi ( EVA)
Ujumbe kuhusu Mti wa kati aliopewa Adamu ni huu.

-
Ujumbe kuhusu Mti wa kati alipewa Adamu ni huu
- Mwanzo 2:17 walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.

Ukisoma hapo ni wazi kwamba Adamu ndio alipitisha huo ujumbe wa Mungu kuhusu mti kwa Eva, na kama Binadamu mwingine ujumbe unapopitia kwa mtu mwingine asie mlengwa anaufikisha kwa Mlengwa anaufikisha ukiwa na mapungufu au Chumvi. Kwa case hii Adamu alifikisha ujumbe pungufu kwa Eva na Shetani akamtumia Eva sababu alipewa ujumbe pungufu.

Ujumbe aliopewa Eva ni huu,

-Mwanzo 3:2 Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula;
Mwanzo 3:3 lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa.

NB: Hapo katika Mwanzo 3:3 unaona Eva anazungumzia maagizo ya Mungu kuhusu mti , anaongelea kufa tu lakini haongelei kama ni mti wa ujuzi wa mema na mabaya kama alivyoagizwa Adamu kwa mara ya kwanza , Mwanzo 2:17

Ni wazi Adamu hakumwambia Eva kuwa ni mti wa mema na mabaya shetani akatumia mwanya huo kumdanganya Eva kutumia kipengele hicho hicho.

Mwanzo 3:4 Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa,

Mwanzo 3:5 kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.

Kwa hiyo shetani alitumia weakness hio kupitia kwa Eva kwanza.

- Kwanini Eva baada ya kula na kuliona lile tunda linafaa kwa chakula hakuhisi tofauti yoyote mpaka alipompa Adam akala ndio wakajihisi wako uchi?

::: Yes, ni kweli Eva hakuhisi chochote alipokula mpaka Adamu alipokula sababu wao ni mwili mmoja; mpaka alipokula Adamu mwili ukakakamilika
-Mwanzo 1:27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.
Note: hapo ameongelea Mtu na si watu halafu mbele Ameongelea Me na Ke

Ndio maana pamoja na wote kula wakiwa wawili lakini bado Dhambi ililetwa na Mtu mmoja
- Warumi 5:12 Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi;

Mimi naamini angekula Eva tu bila kumshirikisha mkewe mambo yangekuwa tofauti .
Ni nani aliwafunulia siri ya wao kuwa uchi?

Mwanzo 3:10 Akasema, Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha.
-Mwanzo 3:11 Akasema, Ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je! Umekula wewe matunda ya mti niliyokuagiza usiyale?

Ni wazi baada ya kula lile tunda walitakuwa wawe uchi.. lakini kuna swali fikirishi hapa ukisoma
Mwanzo 3:7 Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajijua kuwa wa uchi, wakashona majani ya mtini, wakajifanyia nguo.

Hapo utaona walishajifanyia nguo, lakini ukienda mbele 3:10 wanamwambia Mungu wako uchi!!
Hiyo uchi ni kiroho au uchi, uchi!!
 
Back
Top Bottom