tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 24,290
- 22,792
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Nabii Mkuu na maarufu Afrika Mashariki na Kati, Nabii GeoDavie, kwa mara ya kwanza ameipinga biblia hadharani kama unavyoweza kumsikiliza kwenye video ifuatayo. Nabii Mkuu ametanabahisha hilo baada ya kukerwa na watu wanaomuandama kila kukicha kuwa hatumii maandiko yaliyomo kwenye biblia katika mahubiri yake. Hebu msikilize wewe mwenyewe hapa mkuu.
MAONI YANGU
Kwa muda mrefu nimekuwa siyaamini mahubiri ya Nabii GeoDavie lakini kwa hili la biblia ni kama vile namuelewa kwa mbaaali! Nasimama na Nabii kwani hata mimi kuna baadhi ya maandiko katika biblia yananipa shida kuamini kama kweli yaliandikwa na Mungu au ni maneno tu ya wanadamu.
Baadhi ya maandiko tata yaliyomo kwenye biblia na ambayo yanawashangaza wengi ni kuhusu kuumbwa kwa mwanadamu pale bustanini Eden na kisha mwanadamu akadanganywa na nyoka na kujikuta akiadhibiwa na Mungu. Adhabu ambazo mwanadamu aliadhibiwa na Mungu zinasimama hadi leo.
Kwanza, huyo nyoka aliyemdanganya Eva akala tunda la ujuzi wa mema na mabaya alitoka wapi mbona uumbaji wa nyoka haukutajwa kwenye hadithi ya uumbaji? Au kuna mpinzani wa Mungu aliyemuumba huyo nyoka ili kuharibu mipango ya Mungu?
Pili, Mungu alikuwa na malengo gani kumuumba mwanadamu mwenye akili pungufu ukilinganisha na akili za nyoka huku akijua kuwa nyoka angemdanganya kwa urahisi na kumlisha matunda kutoka mti uliokatazwa na Mungu?
Tatu, kwanini Mungu aliumba huo mti wa matunda huko Eden huku akijua kuwa matunda yale yangetumiwa na nyoka kumlisha mwanadamu aliyemuumba? Inawezekana Mungu alifanya makusudi ili mwanadamu ale matunda kisha amuadhibu adhabu ya milele?
Utata mwingine ni kuhusu kuoa kwa Cain na Abel. Adam na Hawa walifanikiwa kuzaa watoto wawili tu wa kiume, ambao ni Cain na Abel. Lakini ukisoma katika kitabu cha Mwanzo 4:17, imeandikwa kwamba Cain alimjua mke wake, na akapata mimba na kumzaa Enoch. Huu mstari unazua utata kuhusu ni wapi mke wa Cain alipatikana ikichukuliwa kuwa Adam na Eva walikuwa ndio viumbe pekee waliokuwepo duniani wakati huo. Hata jina la huyo mke wa Cain halijatajwa mahali popote pale kwenye biblia.
Kwa mifano hii ya utata (contradictions), na mingine mingi iliyojaa kwenye biblia, kuna uwezekano mkubwa kuwa biblia ni mradi wa wanadamu, hasa wazungu, iliyotungwa kwa manufaa yao binafsi, hasa maslahi ya kikoloni.
Nawasilisha.