Ni propaganda mfu. Imemezwa na kutamkwa bila ya utafiti. Dr.Wilbrod Slaa wa CHADEMA amezaliwa tarehe 29/10/1948. Eti anaitwa babu. Huku ni kuishiwa kwa hoja. CCM hatukufika hapo. Tazama baadhi ya waandamizi wa kwetu wa CCM ambao wengine wanatajwa kuwa wagombea Urais na uone Dr.Slaa alivyo kijana:
-Wasira (amezaliwa 1945. Ni miaka mitatu kabla ya Dr Slaa)
-Mangula (mwaka wake wa kuzaliwa hauko wazi lakini ni mkubwamnokwa Dr. Slaa)
- Sitta (amezaliwa tarehe 18/12/1942 miaka zaidi ya mitano kabla ya kuzaliwa kwa Dr. Slaa)
-Pinda (amezaliwa tarehe 12/8/1948 akimzidi miezi miwili Dr. Slaa)
-Kinana (mwaka wake wa kuzaliwa hauko wazi ingawa kuna habari kuwa amelitumikia Jeshi la Wananchi kwa miaka takribani 20 hadi alipong'atuka 1972. Kimahesabu, naye umri umekwenda)
Kuna orodha ndefu ya waandamizi chamani ambao ni wakubwa wa Dr. Slaa wa CHADEMA lakini hawaitwi 'babu'. Ni propaganda za kitoto sana. Niwaase wanachama wenzangu wa CCM na wakereketwa wetu kuachana na jina dhafu hilo kwa Dr.Slaa. Sisi tuna kaka na dada zake wengi tu ndani ya CCM. Nasi tuwaitaje?
Mzee Tupatupa wa Lumumba (sasa Dodoma)