Kama Crown FM imezinduliwa bila kuwa hewani, litakuwa ni kosa kubwa la kibiashara

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,016
9,885
Imagine watu wanataka kupata radha, ubunifu na vipindi tofauti. Uzinduzi umefanyika halafu kitu kisipatikane. Kwanza niseme nimetune channel hiyo zaidi ya mara sita ila sisikii kitu, kwenye kurasa za Crown FM sioni content, Inaonekana kama ilizundiliwa kuwaweka watu tayari wakati wenyewe wakiwa hawako tayari.

Nilitarajia siku ya uzinduzi mitambo iwashwe watu tuanze kusikiliza music wakati watangazaji wanajipanga kuleta vipindi. Anyway, inawezekana radio yangu mbovu, ila kama kweli hii crown FM ilizinduliwa bila kuwa tayari watakuwa wamefeli kwa kuwa wasikilizaji waliokuwa tayari kusikiliza watakuwa tayari wamechoka kuitafuta mara kwa mara na kuichoka.

Kifupi ni poor marketing strategy.
 
Upo sahihi Mkuu Kibiashara ni kitu kibaya

Ni kama vile unaenda duka flani Kila siku unakuta bidhaa hiyo haipo
Automatically utakata tamaa

Inshort inakuwa ni white elephant project
 
Ali Kiba sio mtu wa kumuamini sana, aliwahi kufanya promo ya kinywaji cha Mofaya na hakikuwahi kuuzwa sehemu yoyote Tz. Anyways kama nyuma yake kuna Kusaga sina wasiwasi soon radio itasikika
Kinywaji Cha mo faya aliingiza sokoni sema price yake ilikua kubwa soko likagoma....cartons of mofaya ziliozea pale store ya mikocheni alipokua amepanga Kwa mama simba.akazitelekeza pale pale..

Kiufupi uyo alikiba nje ya kuimba na kukata kiuno , biashara sio fungu lake..awaache tu kina mondi kidogo wanajitaidi ktk biashara..
 
92.1 hizi frequency hazishiki.
Binafsi amenikwaza, anyway anaejua Ratiba ya matangazo ya vifo Radio one atusaidie hiyo Ratiba
 
Mbona niliona mtandaoni picha za Studio ya hiyo Crown FM.

Ama ni picha za kubumba?
 
Ali Kiba bwana,akili zake sijui zikoje. Yeye kila kitu mpaka apushiwe na watu. Kumbe walizindua wazo la radio?
 
Back
Top Bottom