Kakobe apinga nyaraka za viongozi wa dini; akemea kauli ya Pengo

Kakobe apinga nyaraka za viongozi wa dini; akemea kauli ya Pengo

Samahani jamani,

Kama huwawezi basi jiunge nao. Ndio mbinu yangu ya "kutoka" hiyo!
 
Kakobe alichokisema ni ukweli mtupu, hata kama wanajitokeza wanaojaribu kumkebehi. Amewachoma wana ccm hata kama huwa anajumuika nao. Kuhusu pongezi kwa Kibaki, ile ni lugha ya kisiasa, ili aweze kudroo attention kwa umma kumsikiliza, vinginevyo watu wasinge droo attention naye. Lakini ujumbe wake ni kuwataka watanganyika kusisimama imara kutetea maslahi yao na si kusubiri kuangalia wanayofanya wengine na kujifanya wadadisi wakati ya kwao yamewashinda.
 
Zalendo halisi,

Samahani mkuu, hii ya kusomea Nigeria una uhakika nalo?

Maana mimi nafikiria kuwa fisadi mkuu hapa nchini na jamaa yangu mmoja anasema ukitaka kuwa fisadi either uibe BOT, Richmonduli, Ndege, IPTL, Kiwira etc, au uwe jambazi sugu na kuibia mabenki na kuuwa watu au uwe MCHAWI.

Sasa mimi nataka niwe MCHAWI ili mafisadi wakishaiba wawe wanakuja kwangu kuwafanyia mambo flani flani kisha nawadhulumu hela zote!

Halafu naanzisha miradi ya kuwasaidia wananchi!

Unaonaje hilo? nipe chuo na mahali huko Nigeria. Nitumie kwenye PM ikiwezekana.

Mie nimekusoma(nimekuelewa mtatzamo wako),Na nina kuunga mkono,
Lazima uyatazame mambo pande zote ,sawa...?
 
Wakuu nimekuwa nikitafakari sana press release ya Zakaria Kakobe na insticts zangu zimekuwa zikinishawishi kwa kiasi kikubwa nikiamini kwamba ama anatumiwa na CCM (divide et impera) au anajipendekeza kusafisha uhusiano wake mbaya na CCM tangu mwaka 2000 (kama sikosei) wakati akimuunga mkono ALM (mzee wa Kiraracha.
Katika kuperuzi kwangu nikakutana na bandiko moja la Faustin S. Munishi (maarufu kwenye nyimbo za injili) akielezea sura halisi ya Zakaria Kakobe (bandiko ni refu kidogo but its worth reading):

Askofu Kakobe msiyemjua

kakobendogo.jpg
[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif]Taja jina ASKOFU KAKOBE popote Tanzania na utashangaa kujua kwamba karibu kila mtu anamfahamu. Wengi walimfahamu pale alipoweka historia ya kujitosa katika ulingo wa siasa na kumpigia debe Augustino Lyatonga Mrema. Hiyo ilikuwa ni mwaka 2000 wakati wa uchaguzi mkuu. Mengi yalisemwa kumhusu, lakini mimi naheshimu uhuru wake kama mtanzania kutangaza msimamo wake kisiasa katika nchi yake. Tena kama Askofu anaeongoza kanisa la Full Gospel Bible Felloship alikuwa na haki kuwatangazia washirika wake ambao pia ni wanachama wa vyama tofauti vya kisiasa msimamo wake kisiasa kama kiongozi wao kidini. Kwangu kama kuna wakati niliwahi kumheshimu Kakobe basi ni wakati huo. Aliwakemea waziwazi bila woga CCM Chama Cha Majambazi na kuvumilia vishindo na matisho yao. Japo kwa sasa hana misimamo mikali kuihusu CCM hiyo inaeleweka. Nani aipinge CCM aishi salama Tanzania? Kama hawatakuua, basi watakufuatilia kila ufanyalo na kabla ujue kila kitu kwako kitakuwa kichungu. Nasikia Kakobe walimfuatilia kiasi cha kulisambaratisha kanisa lake. Kila neno baya waliloweza kulisema kumhusu basi walilisema. Kila mbinu chafu ya kisiasa CCM waliyoweza kuitumia kinyume cha Mtumishi wa Mungu Kakobe basi waliitumia mradi tu waone kwamba walimharibia katika kila jambo. Hata kama Kakobe leo amepunguza misimamo mikali kuhusu CCM, lakini mimi namwita shujaa alieandika historia ya watumishi wa Mungu walioipinga CCM mchana jua linawaka. Kwa hilo Kakobe ni mfano wa kuigwa. [/FONT]

[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif]Lakini Kakobe ni nani hasa? Je tunamfahamu kweli KAKOBE? Nini kinachomfanya awe alivyo? Mimi mwinjilisti na mwimbaji wa nyimbo za injili, Faustin S. Munishi nakuletea Kakobe ambaye hukuwahi kumfahamu. Tulifahamiana naye kwenye miaka ya themanini hadi mwaka 84 nilipohamia Kenya na kumwacha Kakobe Tanzania. Kwa miaka niliyomfahamu, huyu ndiye Kakobe Zakaria Mokovu jeuri anayejiamini katika kila afanyalo. Wengi huchanganya bidii ya mtu katika kile akifanyacho na upako wa kiungu. Cocacola imafanikiwa kuuzwa duniani kote siyo kwamba wenye kampuni wameokoka, bali ni juhudi zao katika kutangaza bidhaa yao. Biashara nyingi duniani zimefanikiwa kwa wenye biashara hizo kufuata kanuni za biashara. Mengi hajawahi kusema kama ameokoka au la, lakini kibiashara bado anaongoza. Je Kakobe huendesha kanisa akitumia kanuni za kibiashara? au anatumia kanuni za neno la Mungu? [/FONT]
[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif]Alianza kama mmachinga wa kunakili nyimbo za wasanii mbali mbali bila kibali kutoka wasanii hao. Ingekuwa ni wakati wa sasa angekamatwa na kufikishwa mahakamani kwa kosa la kunakili nyimbo bila kibali cha wasanii, lakini wakati huo alipewa leseni ya kufanya kazi hiyo. Cha ajabu aliitangaza kazi hiyo haramu kwenye vyombo vya habari. Jina la kampuni yake lilijulikana kama MULANGA EDITION. Hiyo ilikuwa kwenye miaka ya themanini. Bidii yake ya kujitangaza, na kuamini alichokifanya hata kama ni kazi haramu, zilimfanya ajulikane Tanzania nzima kama mnakili kanda maarufu. Sishangai watu wanaposema kwamba kanisa analoliongoza la Full Gospel Bible Felloship ndilo linaloongoza makanisa ya Kipentekoste kwa idadi ya watu. Lakini hiyo haimaanishi kwamba kanisa hilo ndilo kipimo cha makanisa Tanzania kwani hata wengi mara nyingi hukosea. Ila nisieleweke kama ninayesema kwamba kanisa la Kakobe siyo la kweli, lakini siwezi pia mia kwa mia kusema kinyume chake. Mungu pekee ndiye mwenye kipimo cha kuhukumu kanisa gani la kweli. ILa siyo vibaya watumishi wa Mungu wakitoa tadhimini yao kuhusu yale wanayoyaona na kuyasikia, na kwa sababu wana roho wa Mungu ndani yao, mara nyingi hawatakosea sana. Nisemayo nayasema kama mtumishi wa Mungu. Pengine niseme kwamba mimi ni mtumishi wa Mungu. Ninajiamini hivyo. ila simzuii mwingine kuniona vinginevyo kwani hata ninayemsema hapa pengine naye anajiamini ni mtumishi wa Mungu. [/FONT]

[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif]Pengine Askofu Kakobe atakuwa amesahau, lakini mimi siwezi sahau. Nyakati hizo tulikuwa tukikutana mara nyingi na kujadili mengi yanayohusu wokovu na kukua kwa kanisa la Mungu kwa ujumla. Kwa muda wote tuliowahi kujadili mambo na Kakobe, nilimchukulia kama mtu aliyekuwa na upeo mkubwa wa kuchambua mambo na hakuwa mtu rahisi wa kufuata mambo kama bendera ifuatavyo upepo. Mara nyingi alihoji kuhusu pesa walizokuwa wakichanga kwa maandalizi ya mikutano ya Mwinjilisti Kulola, aliwahi kuniambia kwamba mikutano hiyo inaanza kukosa maana na inaelekea kugeuzwa kama sherehe za kila mwaka. Kwa mtazamo wake wakati huo, Lengo zima la kuwaleta wenye dhambi kwa Yesu lilikuwa linasahaulika na badala yake washirika wa makanisa ambao tayari walikuwa wamemwamini Yesu, ndio waliokuwa wakija kusheherekea injili. Wakati huo nilikubaliana naye mia kwa mia japo nilikuwa nikizunguka mikoa yote Tanzania na mwinjilisti Kulola. Kama Kakobe angeitisha mapinduzi wakati huo, tungeungana kumpindua Kulola. Lakini yale aliyokuwa akimlaumu Kulola kwayo, sijui kama wengine wakimlaumu yeye sasa atasemaje. Lakini Kakobe hakosi la kusema kama nimjuavyo. Pamoja na kwamba hakuwa tajiri wa kutisha kama alivyo sasa, Kakobe Alijiamini, alijipenda sana. Isingekuwa ajabu kumuona Kakobe na mke wake pamoja na mtoto wao wa kwanza wakitembea kwa miguu katika barabara ya Samora siku ya Jumapili baada ya ibada. Mara nyingi tulikutana mjini bila taarifa wala kujiandikisha na tulijadili mengi mimi na Kakobe. Miaka imepita na mengi yamebadilika. Sitarajii sasa kumpata Kakobe akila mhogo wa kuchoma pale Kariakoo, Lakini asishangae akinipata pale Kariakoo kwa mama ntilie nikila wali nusu sahani na kisamvu. Ndiyo maisha yangu. Bado niko huru kama alivyokuwa Kakobe miaka ya themanini. [/FONT]
[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif]Alikuwa mtu huru. Watu waliijua MULANGA EDITION kuliko mmiliki wake ambaye alikuwa Kakobe, Jambo lililomfanya huru kutembea kona zote Dar bila watu kuanza kuonyeshana Kakobe ndiye yuleee. Nina mashaka kama sasa akiwa askofu mkuu anaweza kudhubutu kutembea huru kwenye barabara za Dar. Kwa sasa watu wanamjua Kakobe kuliko kanisa la Full Gospel Bible Felloship, analoliongoza kama askofu mkuu. Pia mwenyewe sidhani kama atapenda kuonekana mjini akiwa bila gari kubwa, itakuwa kujidhalilisha. Lakini mimi bado niko huru kutembea kona zile tulizokuwa tukikutana miaka ya themanini, na sitokubali chochote kininyanganye uhuru huo. Siyo umaarufu au sifa za wanadamu zinazoweza kuninyanganya uhuru wa kukutana na watu, na kwenda nitakako kwa wakati nitakao. Kama cheo ndicho kinachoweza kusimama kati ya mimi na uhuru wangu, basi najua nitakavyofanya. Tuache hayo ya mimi, tuendelee na yake Kakobe. [/FONT]

[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif]Pamoja na biashara yake ya MULANGA EDITION ambayo ilikuwa inashamiri kila kukicha, Kakobe alikuwa mshirika mtegemewa wa kanisa la TAG Temeke. Alitegemewa sana kanisani hapo kwa michango ya kila aina kanisani. Kama ilivyokuwa kawaida ya makanisa mengi ya Kipentekoste nyakati hizo, wengi kati ya washirika walikuwa hoi kimaisha, jambo lililowafanya wachache waliojiweza kubeba mzigo wote wa mahitaji ya kanisa. Kakobe wakati huo alikuwa anajiweza kimaisha jambo lililomfanya awe na uhusiano wa karibu sana na Mchungaji. Mchungaji wa kanisa la Temeke wakati huo alikuwa ni Masalu. Kakobe mara nyingi alikuwa akilalamika kuhusu michango isiyoisha kanisani, na hasa akitilia maanani kwamba yeye na wenzake wachache ndio waliokuwa wakibeba mzigo huo. Siku moja aliwahi kunihoji wakati wa moja ya mikutano ya Mwinjilisti Moses Kulola, na ilikuwa kuhusu mahali nilipopangiwa kulala na aina ya chakula nilichokuwa nikipewa wakati wote wa mkutano huo. Nilipomweleza kwamba nilikuwa nakula chakula cha kawaida yaani maharagwe na ugali au na wali, alionyesha kutolifurahia hilo. Japo hakuwa na cheo chochote kanisani, aliniahidi kwamba ataongea na mchungaji na watanihudumia kama mtumishi wa Mungu mwalikwa. Kweli jioni iliyofuatia chakula changu kilibadilishwa na nikawa nakula sawa na Mwinjilisti Moses Kulola tena kwenye meza moja. Itakumbukwa kwamba kwenye mkutano huo nilikuwa mhudumu kwa njia ya uimbaji. Kwamba Kakobe alikuwa akirekodi nyimbo zangu na kuwauzia washirika huo ni ukweli usiopingika. Lakini heshima aliyoionyesha kwangu wakati huo ilikuwa siyo ya kawaida. Pengine ilikuwa ni kutokana na biashara yake ya kunakili nyimbo za waimbaji mbalimbali, ndiyo iliyomfanya awaheshimu wasanii wote kwa ujumla sijui. Lakini bila kuongeza chumvi Kakobe alikuwa mtu pekee kuwahi kuipa heshima ya hali ya juu huduma yangu ya uinjilisti kwa njia ya uimbaji, wakati waimbaji walichukuliwa si lolote kanisani. Ila siwezi kujua kama bado anawaheshimu wasanii wakati huu akiwa Askofu mkuu. [/FONT]

[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif]Majuzi nilipata nafasi ya kulitembelea kanisa lake la Full Gospel Bible Felloship jijini Dar es Salaam. Kulikuwa na kongamano la wachungaji zaidi ya 8000 wa makanisa mbali mbali ya kipentekoste. Ni kitambo kidogo tangu tukutane na Kakobe uso kwa uso. Tangu miaka ya themanini hadi themanini na nne sikumbuki kama tumewahi kukutana. Ukizingatia kwamba miaka mingi hatujaonana na mtumishi wa Mungu Kakobe, halafu uchanganye na Mengi tuliyowahi kujadili na Kakobe kuhusu Kanisa la kipentekoste Tanzania na Hatma yake, Tena uongeze na Askofu Kulola ambaye miaka hiyo alikuwa na vita kali kati yake na Askofu Emanuel Lazaro, na wote wako kwenye kongamano, Kwa nini mimi Munishi nisiwepo? Hata kama siyo kuhudumu kama mwimbaji, nikae nisikilize wasemavyo wengine. Kwa kuwa ilitokea kwamba niko Dar kwa kipindi hicho, na kuna mkutano wa kihistoria kama huo, ningeukosa basi sijui mimi ningekuwa mhubiri wa jinsi gani nisiyefuatilia matukio ya kiinjili katika nchi yangu Tanzania. [/FONT]

[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif]Sikuruhusiwa kuingia kwenye mkutano huo kwa kile walichokiita kukosa kadi maalum kuniwezesha kuingia. Pamoja na jitihada zangu kutaka nipelekwe mahali pa kujiandikisha niipate kadi hiyo, lakini walinzi baada kwenda jukwaa kuu kupeleka suala langu walirudi na kunibeba juu kwa juu kunitoa kwenye mlango wa kuingilia mkutanoni na mlango kufungwa. Nilipojaribu kujieleza kwamba lengo langu ni kumsikiliza Askofu Kulola ambaye alikuwa anahubiri kwa wakati huo, majibu yalikuwa kwamba "Hii siyo injili ya kawaida. Ingekuwa hivyo tungeiweka viwanja vya JANGWANI." Siwezi kuwalaumu walinzi mlangoni kwa maswahibu yaliyonikuta, kama kulaumu nitamlaumu Kakobe mwenyewe. Ila kimahusiano mema, Kakobe atawalaumu walinzi kwa kunitimua mkutanoni. Lakini mimi najua walinzi walikuwa wakitimiza maagizo ya BOSS wao Kakobe. Ila sina kinyongo, Kanisa ni la Kakobe, walionizuia kuingia ni walinzi wa Kakobe, sasa wa kulaumu lazima awe Kakobe. Ingekuwa Kanisa ni la Yesu kama inavyostahili kuwa, basi hakuna mwenye mamlaka ya kunitimua hapo. Tena kanisa la Yesu linapaswa kuwa la jumuia na siyo mali ya mtu. Katika nyakati tulizo nazo ambapo makanisa yanabinafsishwa na kuwa mali za watu binafsi, basi wengi watatimuliwa kama mimi. Wananicheka kwa sababu nimeanza kutimuliwa, lakini ukimuona mwenzio ananyolewa, kichwa weka maji kwani wakimaliza na huyo itakuja zamu ni yako.[/FONT]
[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif]Baadaye ndipo nilipokuja kuelewa kwamba Lengo la mkutano lilikuwa ni kuweka mikakati ya kujenga mahusiano mazuri kati ya kanisa na serikali. Akizungumza wakati wa ufunguzi, Mwenyekiti wa umoja huo Askofu Sylvester Gamanywa alisema, wakati umefika kwa serikali kutowapuuza wapentekoste. Alidai kwamba wapentekoste hawapewi nafasi katika vyombo vya habari vya kitaifa jambo ambalo alisema limechangiwa na dhana potovu kwamba walokole ni watu waliochanganyikiwa kimaisha na hawana lolote la kuweza kuisaidia serikali kiutawala. Naye Askofu Kitonga wa kanisa la Redeemed Kenya alisema anaunga mkono kongamano hilo na akasema anafurahi kuona askofu Kakobe akiufuata ushauri wake wa kutoipinga serikali iliyoko madarakani. Aliongeza kwamba nchini Kenya serikali iliyokuwa madarakani ilitambua umuhimu wa wapentekoste na iliwatumia sana katika kuwasilisha sera za serikali kwa wananchi ambao wengi ni washirika wa makanisa hayo. Lakini wale wanaopinga wazo la kanisa kununuliwa na serikali wanasema, Kanisa ni chombo cha kukemea maovu katika jamii na serikali ikiwa mojawapo. Waliongeza kwamba Kanisa linapokubali kununuliwa na serikali, hiyo ni hatari kubwa. Walisisitiza kwamba Inasikitisha kuona kwamba kanisa la Tanzania limekubali kununuliwa na serikali ya CCM ambayo sifa yake ni kuwaua raia wasiokubaliana na sera zao mbovu za wizi , Ukandamizaji, na uonevu wa kila namna kwa raia wa Tanzania. Mungu lisaidie kanisa lako Tanzania. [/FONT]​
 
Mara mwisho aliambiwa na ccm kuwa akiendelea kumuunga mkono mrema kanisa lake lipo barabarani hivyo litabomolewa.Akafyata mkia akanywea.Huyu bwana ni kama ana pepo maana makanisa mengine hayana imani na kazi yake.Hivyo ni wakati mwafaka na kuna kila sababu ya kuamini kuwa anatumiwa na chukua chako mapema(ccm).Katumwa na kingunge.....
 
Nimesoma katika mtandao kuwa Kakobe kamkemea Kikwete kuwa ni mpole mno kwa kutokemea nyaraka za Katoliki na waislamu kuwa waziache.

Namshangaa Kakobe kweli ni mnafiki.Mbona hakumkemea Kikwete na serikali yake ilipopeleka mjadala wa kadhi bungeni? Kwa nini hakumuuliza kIngunge kwa nini hakukemea suala la KAdhi kuingia bungeni na mchakato wake kuingizwa serikalini wizara ya mambo ya sheria na katiba? Mnafiki mkubwa.

Nilichogundua ni kuwa anajikomba kwa serikali na kingunge Ikumbukwe kuwa ASkofu hutu alikuwa mwanasiasa mkubwa aliyetelekeza dini na kuwa mpiga debe wa Mrema aliyetoa unabii wa uongo kuwa Mrema angemshinda Mkapa.Huo unabii wake ukawa wa Uongo mkubwa Mkapa akashinda na mwamawe Mrema aliyempigia madogoli ya unabii wa uganga wa kienyeji wa uongo uwa angeshinda uchaguzi wa 1995 akashindwa vibaya na Mkapa.
Serikali wakati ule ilimlaaani ajkajifanya kichwa maji na unabii wake wa uongo.

Kingunge kampongeza kwa Sababu mwaka wa Uchaguzi 1995 mwenyekiti wa vijana wakati ulle NCHIMBI ambaye sasa ni naibu waziri wa Ulinzi aliamua kumkabili Kakobe na kubishana na Kakobe kuwa ni MWONGO na atashangaa mgombea wake Mrema Hatatashinda Kingunge akaingilia kati akamkemea Nchimbi akamwambia Nchimbi acha kubishana na Kakobe.Nchimbi akanyamaza.Sasa Kakobe analipa fadhili kwa Kingunge kwa kumsifia na kujifanya rafiki kwa Kikwete ili serikali imwone kama katubu mnafiki mkubwa.Kachagua kumpongeza Kingunge kwani Kingunge aliamua kumkemea mshabiki Nchimbi aliyekuwa kaamua kumvalia njuga Kakobe.Mashambulizi ya NChimbi yalikuwa makali kiasi kuwa kosa Kingunge kuingilia kati kumyamazisha nchimbi KAKOBE angekiona cha mtema kuni.Hata hivyo Mashambulizi ya Nchimbi yalikuwa makali kuwa pamoja na Kingunge kumnyamazisha Kakobe aliumia akakimbilia mafichoni akijifanya eti yuko katika maombi ya nguvu ya kumuomba huyo mungu wake kama yupo kweli aliyempa unabii wa uongo kuwa Mrema ATASHINDA UCHAGUZI lakini ukweli wa mambo ni kuwa aliingia mafichoni kwa aibu kwa kuwa unabii wake wa uongo kuwa Mrema angeshinda haukutimia.

Alikuwa wapi kuikemea serikali kuwa iachane na suala la kadhi kuwa suala lile ni hatarri kwa usalama wa nchi?alikaa kimya huyu.

NABII uongo aliyetabiri Mrema kushinda na hakushinda eti anaibuka kuwakemea wale waliokemea Suala la Kadhi hivi huyu kama si mnafiki ni nini? Asiye upande wetu kwa suala la kukemea mambo ya Kadhi yu kinyume chetu.MUNGU NA SHETANI UNAOWATAJA KILA SIKU KAMA WAPO NA WAKULAANI MNAFIKI NA MWOGA WEWE KAKOBE.

Kakobe umechelewa ulikuwa wapi suala la kukemea kadhi? Hatuna cha kukuheshimu you are too late ndio maana waumini wengi wamekukimbia unabaki unajikomba kwa wapagani akina KIngunge kwa kuwasifu kwa sifa wasiokuwa nazo.

Mimi ni mpagani na huwa nawalaani sana wakatoliki hata kwenye maandiko yangu nikipata mwanya lakini kwa suala la Kukataa suala la kadhi kulikataa mlikuwa sahihi na mlionyesha ujasiri mkubwa kusema wazi tofauti na Kakobe aliyejifanya hana cha kusema.Kwa suala la kukemea suala la kadhi kuingizwa bungeni na katika serikali wakatoliki nawapa hoyeeee Kakobe nampa Ziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.
 
Ndio Viongozi wote wa Dini tulionao Tanzania. Hivyo Sisi Wananchi ndio wenye kuwalea watu hawa
 
Kakobe ashambuliwa
• Wadai anajipendekeza kwa Rais Jakaya Kikwete

na Joseph Sabinus na Sauli Giliard

amka2.gif

SIKU moja baada ya Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zacharia Kakobe kuupinga Waraka wa Kanisa Katoliki na Mwongozo wa Waislamu, Kanisa Katoliki limemgeuzia kibao kiongozi huyo wa kiroho na kumweleza kuwa ni kigeugeu na anajikomba kwa watawala.
Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana, Askofu wa Jimbo Katoliki la Mbeya, Mhashamu Evaristo Chengula, alisema endapo serikali inalipangia kanisa lake jambo gani la kuandikwa na kuhubiriwa, basi aendelee kufanya hivyo na si Kanisa Katoliki.
"Mambo ya dini hatuwezi kwenda kuiuliza serikali, lakini kama yeye anaomba kupangiwa mahubiri, afanye hivyo," alisema Mhashamu Chengula.
Alisema Askofu Kakobe ana tabia ya kujipendekeza kwa watawala kiasi cha kushindwa kujua mahitaji ya wafuasi wake kiroho na kimwili.
Alisisitiza kuwa, kamwe Kanisa Katoliki haliwezi kupangiwa na serikali mambo ya kuhubiri na kuongeza kuwa, kama kanisa lake linafanyiwa hivyo, basi atekeleze hayo kanisani mwake.
Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Walei, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Joseph Selasini alisema, Askofu Kakobe hana budi kutambua kuwa Kanisa Katoliki halijipendekezi kwa watawala, bali linazingatia maslahi ya umma.
"Kanisa halijipendekezi wala kutafuta Cheap Popularity (umaarufu kirahisi) kama Kakobe, hivyo kusema maaskofu wamekosa nidhamu, ni kuonyesha upeo mdogo wa kazi yake ya uaskofu anayoifanya," alisema Selasini.
Alihoji: "Kakobe huyo anayesema nidhamu, aliwahi kuipigia kampeni TLP alipoona haikuingia madarakani, akahamia CCM, sasa anatapatapa, mara CCM mara TLP. Hiyo ndiyo nidhamu anayopaswa kuwa nayo mtu anayejiita Askofu Mkuu?"
Selasini alimtaka Askofu Kakobe kuachana na mambo hayo kwa sasa ili akomae kiimani kwanza kabla ya kufanya jaribio la kujilinganisha na Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo, ambaye ni Askofu Mkuu Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam.
"Kakobe asijilinganishe na Kardinali Pengo kwa kuwa uaskofu wao ni kama mlima na kichuguu, hivyo asitumie heshima wanayompa waandishi kumsikiliza kwa kuchanganya watu, maana uaskofu wake ni kigeugeu wa kutafuta maslahi ya kidunia," alisema.
Naye mmoja wa waamini wa Askofu Kakobe ambaye jina lake limehifadhiwa, alisema hakutegemea kuona kiongozi huyo wa kiroho akipinga msimamo wa viongozi wa dini kutochaguliwa mambo ya kuhubiri.
Kwa upande mwingine, Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Shura ya Maimamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda, alisema hata kama Rais Jakaya Kikwete ataliingilia suala hilo kama alivyoshauri Askofu Kakobe juzi, hakuna litakalosaidia kwa sasa.
Akizungumza kwa ufupi na waandishi wa habari jana, jijini Dar es Salaam mara baada ya kutoka msikitini, Sheikh Ponda alisema sababu ya kusema hivyo ni kwamba, waraka uliotolewa na Kanisa Katoliki ndiyo umelenga kuwagawa Watanzania na si ule wa Waislamu.
Sheikh Ponda alimgeuzia kibao askofu huyo kwa kumtaka akausome vizuri mwongozo wa Shura ya Maimamu anayoiongoza, na endapo hatauelewa, basi arudi kwa Waislamu wamweleweshe.
Aliusifu mwongozo wa Waislamu kwa kusema kuwa ndiyo pekee unaofaa kwa mustakabali wa taifa na kwamba, tofauti na ule wa Wakatoliki, wa kwao waliuandaa wakiwa wamejiamini.
Nao baadhi ya viongozi wa makanisa ya uamsho wa kiroho jijini Dar es Salaam, wamemjia juu Askofu Kakobe kwa kuushambulia waraka wa Kanisa Katoliki na kumtuhumu kuwa, anatumiwa na mafisadi.
Wachungaji hao pia walishangazwa na hatua ya askofu huyo kumshambulia Kardinali Pengo, na kusema lengo la kiongozi huyo ni kutaka kulitangaza kanisa lake upya baada ya kubaini kuwa limepoteza mwelekeo.
Wakizungumza na gazeti hili, wachungaji hao walitetea kauli ya hivi karibuni ya Askofu Pengo, aliyoitoa mbele ya Rais Kikwete katika ibada ya mazishi ya aliyekuwa Askofu wa Jimbo la Mwanza, Anthony Mayalla, na kusema kuwa kiongozi wa Kanisa Katoliki hakuwa na nia ya kumdhalilisha kiongozi huyo wa nchi.
"Tunavyoona sisi katika suala hili ni kwamba, Askofu Pengo hakuwa na nia ya kumdhalilisha Rais Jakaya Kikwete, bali alikuwa akitoa mawazo yake na kumweleza rais kilicho ndani ya moyo wake kulingana na maandiko ya Kitume," alisema Mchungaji Huruma Choya wa Kanisa la Living God la Mwenge.
Mchungaji huyo alieleza kusikitishwa kwake na kauli hiyo aliyoiita isiyo na baraka za Mungu, ikitolewa na kiongozi huyo wa kanisa, anayeheshimika nchini na kubashiri mwisho wa kanisa lake umekaribia.
Mchungaji wa Kanisa la Glory Tample la Kimara lililopo jijini Dar es Salaam, Andrea Kwayu alisema kilichofanywa na Askofu Kakobe kuchukua hatua hiyo ni chuki dhidi ya Kanisa Katoliki na kwamba anatafuta huruma ya Ikulu kwa maslahi yake binafsi.
Aliongeza kuwa, mazingira ya sasa yanaonyesha wazi kuwa suala la ufisadi na kukosekana kwa uadilifu katika serikali ni matokeo ya kupatikana kwa viongozi wabovu ambao huchaguliwa katika uchaguzi unaoshirikisha wananchi walio wengi.
"Kimsingi Kakobe miaka yote amekuwa na chuki binafsi na Kanisa Katoliki, sasa ameamua kusema hovyo mambo ambayo ni kama analazimisha wananchi waanze kulichukia kanisa hilo," alisema Mchungaji Kwayu.
Kwa mujibu wa Kwayu, jamii imeanza kutambua uongo na ukweli bila kujali jambo analosema kiongozi yeyote yule, ikiwa ni pamoja na wa dini, mwanasiasa ama msomi.
Mchungaji William Mwamalanga wa Kanisa la Pentekoste lenye makao yake makuu mkoani Mbeya, alieleza kusikitishwa kwake na kitendo cha Kakobe kuungana na viongozi wa Shura ya Maimamu katika kuendeleza chuki dhidi ya kanisa hilo la Katoliki.
"Kama kiongozi wa kanisa, alipaswa kutoa msimamo au maoni yake kuhusu waraka wa kanisa na si kuonyesha chuki za wazi kwa Pengo, na kwa kweli ameamua kutumia vibaya sakata la waraka huu, na si kuchangia maoni," alisema Mchungaji Mwamalanga.
Wakati huohuo, Shirika lisilo la Kiserikali la Peace Building and Human Development (PHD), limemtahadharisha Askofu Kakobe kuepuka njama za kutumiwa na mafisadi kwa lengo la kuupinga waraka wa Kanisa Katoliki. Mkurugenzi wa PHD, Philoteus Lissanga alisema, amesikitikishwa kuona hata wananchi wakifuatilia maelezo yake, kwani kwa kufanya hivyo watu waovu katika jamii nao wanapata wafuasi wa kuwaunga mkono.
 
kuna mtu alimuuliza msimamo wake kuhusu Kikwete kabla ya uchaguzi wa 2005 na baadaye... watu wanakumbuka.. Kama ni unafiki ni ule nilioandika kwenye "Barua kwa wachungaji".. baada ya kondoo kutawanyika kama wasio na mchungaji leo wanasimama na kujifanya wananyosha fimbo ya uongozi!!? Ashindwe na kulegea....

Nilimuona mwenyewe siku akimpigia kampeni Mrema, baada ya kuwashutumu CCM kumwita yeye Kibwetere, alisema wazi kuwa CCM si nzuri na aliwapinga sana. I wonder whether what he says today is what he really mean or anataka kuvuna kitu fulani toka CCM. Haaminiki.
 
Huyu Kakobe naye kuna watu bado wanamsikiliza? Hata hapo kanisani kwake anadumaza tu waumini wake kufikiria na kuwaacha waendelee kuwa masikini huku yeye ana magari ya thamani na sadaka anapokea kila siku.
 
Kimsingi Kakobe amekosa dira na sio mtu wa kujadiliwa, maisha yake kwa ujumla ni ya kitapeli na hiyo kofia ya uaskofu amejivisha kwa lengo la kufunika uovu wake mbele ya jamii. Katika medani zote, Kakobe hawezi kujilinganisha wala kupambanishwa na Kadinali Pengo ama askofu yeyote ndani ya Kanisa Katoliki.
 
Mtu asiye wa Mungu huongea kiwafurahichasho wanadamu ili apewe ujira wake hapa hapa. I meandikwa, mtawatambua kwa matunda yao, Naam!
 
Mtu asiye wa Mungu huongea kiwafurahichasho wanadamu ili apewe ujira wake hapa hapa. I meandikwa, mtawatambua kwa matunda yao, Naam!

Kama Kakobe miaka ya nyuma aliishutumu CCM kwa matendo yake ni jambo lipi jema CCM ilmefanya sasa lililomfanya apige U-turn na kuanza kuifagilia CCM? Ni vitisho toka CCM? Kama ni vitisho na yeye akatishika basi kuna walakini katika kanisa la "Yesu" analolijenga. Kanisa la Yesu aliogopi vitisho na haliwezi kujengeka kwa misingi ya woga. Kuanzia kwa Yesu mwenyewe kwa kutundikwa Msalabani, Mtume Pero naye alitundikwa kicha chini, miguu juu. Mtume Paulo alinyongwa huko Roma, Stephano aliyepigwa mawe mpaka akafa na Mtume Yakobo (ndugu yake Mt.Yohana) aliyenyongwa na Herode Agripa na wengine wengi. Wote hawa walikufa katika kusimamia kile wanachokiamini.

Kimsingi kanisa sio "one man show". Kanisa lazima liwe na uongozi wa pamoja ( hata haya ya Pentecoste) kwa sababu wanasema "two heads are better than one". Kakobe angekuwa na mshauri pengine angesita kusema aliyoyasema juzi. Hivi amesahau kwamba wiki tatu zilizopita alisema kwamba Watanazania tususie uchaguzi wa serikali za mitaa na ule mkuu wa 2010? Kwa nchi nyigine huu ungekuwa ni uchochezi kama sio uhaini! Ni jambo baya sana kuwa Ndumila-kuwili hasa ukiwa kiongozi wa kiroho kama Kakobe.
 
Last edited:
kakobe is just a stupid fellow, without vision.
 
Mimi nakubaliana na Kakobe kwa kiasi fulani. Ni kweli tumeshindwa kufanya lolote wakati CCM wanaiba waziwazi. Lakini kuandamana kuhusu Kenya siyo jambo baya maana inawezekana ndiyo ukawa mwanzo wa waTZ kuamka hivyo 2010 wakiibiwa CCM wajue wanategemea nini. Vilevile CCM kutokumtambua Kibaki wanajipalia makaa, kwani 2010 Kibaki atajibu mapigo, unafikiri M7 mjinga mpaka kajitanguliza kumpongeza? Anajua wizi ndiyo deal la viongozi wote Africa wakiongozwa na CCM nambari wani (No. 1)

mitanzania bana sijui mtapata akili lini..mi ni mkenya lakini mke wangu ni mtanzania na ninaish hapa kwenu..na juzi juzi nami nimepata uraia..kwahiyo saivi ni mtanzania sasa..lkn nawaambieni msije fikiria itafika siku wakenya wataandamana kwa maovu ambayo yatafanyika tanzania..kamwe hata siku moja..hawako interested..na hawana time hiyo..nyie angalieni mambo yenu tu..hata siku 1 huwezi jidai wampenda mtoto wa jirani yako na ukamlipia ada wkt wa kwako amefikuzwa shule yuko nyumbani..huo ni upumbavu..peleka shule mwanao kwanza..kama kuna ziada ndiyo mfikirie wa jirani yako..wakenya hawawafikirii nyie hata kidogo..kwnain nyie mjipendekeze wabongo fumbueni macho...anzeni kupigania haki zenu wenyewe..achaneni na mambo ya wa kenya..nyie mna matatizo mengi zaidi tu..chaguzi zenu kura zaibwa kila siku hamfanyi lolote mwacheka cheka na kuishia kuyaongelea kwe JF humu kama mazuzu halafu basi..haiwasaidii hiyo..maana tangu muongelee ccm haijaacha kuiba kura na kufanya ufisadi...u shld do smthng more..more efforts are needed guys...tatueni matatizo ya kwenu bongo ndiyo mkae mumfikirie mkenya...nyerere alipoipatia uhuru nchi hii..ndiyo akaanza ifikiria msumbiji na zimbabwe...
kakobe yuko sahihi kabisa..
 
Mkuu,

Napenda kutokubariana na wewe hapa.

Nadhani Mchungaji yupo right kwa hili,ingawa sikatai nini anaweza kua alifanya na kunena huko nyuma.Kutokana na siasa za kitanzania mabadiliko kama haya ni ya kuyategemea kwa yoyote (mfano Tambwe Hiza wa Cuf aliyeenda CCM).

But honestly how can you compare Kakobe and Tambwe Hiza? Tambwe Hiza ni mwanasiasa ambao hulka yao ni kubadilibadilika. Mtu wa Mungu kama Kakobe anapaswa kuwa na msimamo usiokuwa kwa kinyonga nyonga hivi. Baada ya hili la juzi what next?
 
• Wadai anajipendekeza kwa Rais Jakaya Kikwete

na Joseph Sabinus na Sauli Giliard (Tanzania Daima 4.9.09)

SIKU moja baada ya Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zacharia Kakobe kuupinga Waraka wa Kanisa Katoliki na Mwongozo wa Waislamu, Kanisa Katoliki limemgeuzia kibao kiongozi huyo wa kiroho na kumweleza kuwa ni kigeugeu na anajikomba kwa watawala.

Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana, Askofu wa Jimbo Katoliki la Mbeya, Mhashamu Evaristo Chengula, alisema endapo serikali inalipangia kanisa lake jambo gani la kuandikwa na kuhubiriwa, basi aendelee kufanya hivyo na si Kanisa Katoliki.

“Mambo ya dini hatuwezi kwenda kuiuliza serikali, lakini kama yeye anaomba kupangiwa mahubiri, afanye hivyo,” alisema Mhashamu Chengula.

Alisema Askofu Kakobe ana tabia ya kujipendekeza kwa watawala kiasi cha kushindwa kujua mahitaji ya wafuasi wake kiroho na kimwili.

Alisisitiza kuwa, kamwe Kanisa Katoliki haliwezi kupangiwa na serikali mambo ya kuhubiri na kuongeza kuwa, kama kanisa lake linafanyiwa hivyo, basi atekeleze hayo kanisani mwake.

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Walei, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Joseph Selasini alisema, Askofu Kakobe hana budi kutambua kuwa Kanisa Katoliki halijipendekezi kwa watawala, bali linazingatia maslahi ya umma.

“Kanisa halijipendekezi wala kutafuta Cheap Popularity (umaarufu kirahisi) kama Kakobe, hivyo kusema maaskofu wamekosa nidhamu, ni kuonyesha upeo mdogo wa kazi yake ya uaskofu anayoifanya,” alisema Selasini.

Alihoji: “Kakobe huyo anayesema nidhamu, aliwahi kuipigia kampeni TLP alipoona haikuingia madarakani, akahamia CCM, sasa anatapatapa, mara CCM mara TLP. Hiyo ndiyo nidhamu anayopaswa kuwa nayo mtu anayejiita Askofu Mkuu?”

Selasini alimtaka Askofu Kakobe kuachana na mambo hayo kwa sasa ili akomae kiimani kwanza kabla ya kufanya jaribio la kujilinganisha na Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo, ambaye ni Askofu Mkuu Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam.

“Kakobe asijilinganishe na Kardinali Pengo kwa kuwa uaskofu wao ni kama mlima na kichuguu, hivyo asitumie heshima wanayompa waandishi kumsikiliza kwa kuchanganya watu, maana uaskofu wake ni kigeugeu wa kutafuta maslahi ya kidunia,” alisema.

Naye mmoja wa waamini wa Askofu Kakobe ambaye jina lake limehifadhiwa, alisema hakutegemea kuona kiongozi huyo wa kiroho akipinga msimamo wa viongozi wa dini kutochaguliwa mambo ya kuhubiri.

Kwa upande mwingine, Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Shura ya Maimamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda, alisema hata kama Rais Jakaya Kikwete ataliingilia suala hilo kama alivyoshauri Askofu Kakobe juzi, hakuna litakalosaidia kwa sasa.

Akizungumza kwa ufupi na waandishi wa habari jana, jijini Dar es Salaam mara baada ya kutoka msikitini, Sheikh Ponda alisema sababu ya kusema hivyo ni kwamba, waraka uliotolewa na Kanisa Katoliki ndiyo umelenga kuwagawa Watanzania na si ule wa Waislamu.

Sheikh Ponda alimgeuzia kibao askofu huyo kwa kumtaka akausome vizuri mwongozo wa Shura ya Maimamu anayoiongoza, na endapo hatauelewa, basi arudi kwa Waislamu wamweleweshe.

Aliusifu mwongozo wa Waislamu kwa kusema kuwa ndiyo pekee unaofaa kwa mustakabali wa taifa na kwamba, tofauti na ule wa Wakatoliki, wa kwao waliuandaa wakiwa wamejiamini.

Nao baadhi ya viongozi wa makanisa ya uamsho wa kiroho jijini Dar es Salaam, wamemjia juu Askofu Kakobe kwa kuushambulia waraka wa Kanisa Katoliki na kumtuhumu kuwa, anatumiwa na mafisadi.

Wachungaji hao pia walishangazwa na hatua ya askofu huyo kumshambulia Kardinali Pengo, na kusema lengo la kiongozi huyo ni kutaka kulitangaza kanisa lake upya baada ya kubaini kuwa limepoteza mwelekeo.

Wakizungumza na gazeti hili, wachungaji hao walitetea kauli ya hivi karibuni ya Askofu Pengo, aliyoitoa mbele ya Rais Kikwete katika ibada ya mazishi ya aliyekuwa Askofu wa Jimbo la Mwanza, Anthony Mayalla, na kusema kuwa kiongozi wa Kanisa Katoliki hakuwa na nia ya kumdhalilisha kiongozi huyo wa nchi.

“Tunavyoona sisi katika suala hili ni kwamba, Askofu Pengo hakuwa na nia ya kumdhalilisha Rais Jakaya Kikwete, bali alikuwa akitoa mawazo yake na kumweleza rais kilicho ndani ya moyo wake kulingana na maandiko ya Kitume,” alisema Mchungaji Huruma Choya wa Kanisa la Living God la Mwenge.

Mchungaji huyo alieleza kusikitishwa kwake na kauli hiyo aliyoiita isiyo na baraka za Mungu, ikitolewa na kiongozi huyo wa kanisa, anayeheshimika nchini na kubashiri mwisho wa kanisa lake umekaribia.

Mchungaji wa Kanisa la Glory Tample la Kimara lililopo jijini Dar es Salaam, Andrea Kwayu alisema kilichofanywa na Askofu Kakobe kuchukua hatua hiyo ni chuki dhidi ya Kanisa Katoliki na kwamba anatafuta huruma ya Ikulu kwa maslahi yake binafsi.

Aliongeza kuwa, mazingira ya sasa yanaonyesha wazi kuwa suala la ufisadi na kukosekana kwa uadilifu katika serikali ni matokeo ya kupatikana kwa viongozi wabovu ambao huchaguliwa katika uchaguzi unaoshirikisha wananchi walio wengi.

“Kimsingi Kakobe miaka yote amekuwa na chuki binafsi na Kanisa Katoliki, sasa ameamua kusema hovyo mambo ambayo ni kama analazimisha wananchi waanze kulichukia kanisa hilo,” alisema Mchungaji Kwayu.

Kwa mujibu wa Kwayu, jamii imeanza kutambua uongo na ukweli bila kujali jambo analosema kiongozi yeyote yule, ikiwa ni pamoja na wa dini, mwanasiasa ama msomi.

Mchungaji William Mwamalanga wa Kanisa la Pentekoste lenye makao yake makuu mkoani Mbeya, alieleza kusikitishwa kwake na kitendo cha Kakobe kuungana na viongozi wa Shura ya Maimamu katika kuendeleza chuki dhidi ya kanisa hilo la Katoliki.

“Kama kiongozi wa kanisa, alipaswa kutoa msimamo au maoni yake kuhusu waraka wa kanisa na si kuonyesha chuki za wazi kwa Pengo, na kwa kweli ameamua kutumia vibaya sakata la waraka huu, na si kuchangia maoni,” alisema Mchungaji Mwamalanga.

Wakati huohuo, Shirika lisilo la Kiserikali la Peace Building and Human Development (PHD), limemtahadharisha Askofu Kakobe kuepuka njama za kutumiwa na mafisadi kwa lengo la kuupinga waraka wa Kanisa Katoliki.
Mkurugenzi wa PHD, Philoteus Lissanga alisema, amesikitikishwa kuona hata wananchi wakifuatilia maelezo yake, kwani kwa kufanya hivyo watu waovu katika jamii nao wanapata wafuasi wa kuwaunga mkono.
 
Kila ngoma ina mchezaji wake
Ila nawaambieni watanzania kwamba huko tuendako siko kwema kabisaaaa.

hii inaonesha kwamba siasa siyo safi kwani haiaminiki tena kama itaweza kuwakomboa watu kutoka katika ufukara wao hivyo watu wa dini wanataka kuingia na kujaribu. Tatizo hapa ni kwamba kila mmoja anajiona ana hekima mbele ya macho yake na hataki kusahihishwa......
 
Back
Top Bottom