Kitila Mkumbo
JF-Expert Member
- Feb 25, 2006
- 3,355
- 1,952
Kakobe amempongeza Rais Kibaki kwa kuchaguliwa tena. Mwanzoni niliposoma mstari wa kwanza nilishtuka na nikaanza kusema huyu Askofu kapatwa na nini tena. Hata hivyo kadri nilivyoendelea kusoma nikajiridhisha kwamba huyu bwana anaweza akawa yupo sawa na sisi wengine wote wakiwemo wale waliandamana juzi tukawa tupo on the wrong side wakati wote wa hili sakata la Kenya.
Anachosema Kakobe ni kwamba kilichotokea Kenya ndicho hicho ambacho kimekuwa kikitokea kwetu siku zote tangu mfumo wa vyama vingi uanze na kwamba tume yetu ya uchaguzi ni mbovu kuliko ya Kenya. Anasema tuache unafiki na tutoe kwanza boriti kwenye jicho letu kabla ya kuwanyooshea wengine vidole. OK, hebu na wewe endelea kumsoma na lete maoni yako.
______________________________________________________________
Kakobe atoa mpya
na Mwandishi Wetu (Tanzania Daima)
ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Full Bible Gospel Fellowship (FBGF), Zakaria Kakobe, amesema anampongeza Rais Mwai Kibaki wa Kenya kwa ushindi alioupata katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana.
Mbali ya hilo, Askofu Kakobe amemtaka Rais Jakaya Kikwete kuchukua uamuzi wa kumpongeza rais huyo wa Kenya, akisema uamuzi huo utafuta aibu ya unafiki wa Tanzania.
"Nina ujasiri wa kumpongeza Kibaki kwa kushinda uchaguzi mkuu nchini Kenya. Kwa sababu hiyo basi, iwapo kina Raila Odinga na wenzake wana manung'uniko yoyote na matokeo ya uchaguzi, hawana budi kufuata mkondo wa sheria kwa kwenda mahakamani kupinga ushindi huo," alisema Kakobe aliyezungumza na Tanzania Daima katika mahojiano maalumu ya njia ya simu.
Askofu huyo ambaye kwa miaka kadhaa sasa amejiweka kando na masuala ya kisiasa tangu mwaka 2000, alieleza kuwashangaa Watanzania wanaotoa maneno makali ya kejeli dhidi ya ushindi wa Kibaki.
Kwa mujibu wa Askofu Kakobe, Watanzania hawana ubavu wala jeuri ya kumnyoshea mkono Kibaki au kuwakejeli Wakenya wakati ukweli ukionyesha wazi kwamba uchaguzi Tanzania uhusisha wizi mkubwa.
Akitumia neno kutoka katika Biblia, Askofu Kakobe aliwataka Watanzania wenzake kutoa boriti iliyo ndani ya jicho lao kwanza kabla ya kuanza kukiona kibanzi kilicho katika jicho la mwingine.
Katika hili, Kakobe alieleza kushangazwa na makundi ya watu wakiwamo wasomi na wanasiasa wanaofikia hatua ya kupanga maandamano na kuandamana ili kupinga kile wanachokiita wizi wa kura uliofanywa na Kibaki.
"Watanzania hatuna mamlaka ya kuwanyoshea kidole Wakenya, wakati tukijua kuwa hapa kwetu hali ni mbaya zaidi... ni afadhali tuwaache wengine waseme badala yetu ambao kimsingi ni wanafiki," alisema Kakobe.
Askofu huyo ambaye mwaka 2000 alimuunga mkono Augustine Mrema aliyekuwa akigombea urais kwa tiketi ya TLP, alisema Tume ya Uchaguzi ya Kenya iliyokuwa ikiongozwa na Kivuitu ni bora kuliko ilivyo ile ya Tanzania.
Akitoa mfano alisema, angalau tume hiyo ya Kivuitu miaka mitano iliyopita ilikuwa na jeuri ya kutangaza kushindwa katika uchaguzi kwa Chama cha KANU kilichokuwa madarakani nchini Kenya tangu uhuru wa nchi hiyo mwaka 1963, hatua ambayo anaamini haiwezi kufanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania.
"Hivi wewe unaamini kwamba Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi wa hapa kwetu anaweza akatangaza matokeo kwamba CCM imeshindwa? Angalau Kivuitu huyu tunayemnyoshea kidole alitangaza kushindwa kwa Moi (Rais wa zamani wa Kenya) na KANU," alisema Askofu Kakobe.
Alisema kuna matukio mengi ya ushahidi yanayoonyesha kuwa katika chaguzi mbalimbali hapa nchini kumekuwa na matukio mbalimbali yanayoonyesha kuwapo kwa vitendo vya wizi wa kura.
" Tumepata kumsikia Cheyo (John) akilalamikia kuibiwa kura kwenye uchaguzi wa ubunge kule kwao, hivyo hivyo kule Zanzibar CUF wamekuwa wakilalamikia wizi wa kura. Mbona hatujaona maandamano ya kupinga wizi huo.
"Ni jambo la ajabu kwamba watu hawa wanataka kuandamana kuhusu Kenya na hawajapata kutaka kuandamana kuhusu Tanzania. Tunajifanya ni wasafi sana wakati ukweli ni kwamba sisi ni wanafiki," alisema Kakobe ambaye tangu kuanza kwa mahojiano hayo alikiri kuchukua uamuzi unaotofautiana na watu na makundi mbalimbali.
Mbali ya hilo, Kakobe alieleza kushangazwa na ukimya wa Watanzania wa kutozungumza lolote kuhusu ubaya wa katiba ambao umekuwa ni tatizo kubwa kabisa na kwa miaka mingi.
Alisema ni ukweli ulio wazi kwamba, katiba inayosimamia mfumo wa vyama vingi leo hii ni ya chama kimoja lakini hakuna mtu aliye tayari kulisimamia hilo na kulipigania.
Askofu Kakobe anatoa kauli hiyo siku chache tu baada ya makanisa mengine nchini likiwamo Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) kutoa tamko linaloonyesha wazi kutomuunga mkono Kibaki.
Aidha, kauli hiyo ya Kakobe inakuja siku chache tu baada ya wasomi wa vyuo vikuu kuandamana wakimpinga Kibaki na kumtaka Rais Kikwete kutoitambua serikali yake.
Kabla ya uamuzi huo wa wasomi, juhudi za wanasiasa kadhaa wa vyama vya upinzani kutaka kuandamana wakipinga ushindi wa Kibaki zilikwama kutokana na uamuzi wa Jeshi la Polisi kuzuia maandamano yao hayo.
Tangu kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi Kenya, vurugu zilizozuka katika maeneo mbalimbali nchini humo zimesababisha zaidi ya watu 700 kupoteza maisha yao huku mamia wengine wakiwa hawana makazi.

Last edited by a moderator: