Kaka Cyprian huu sio utamaduni wa wastaarabu

Nao na makonda kama kwa gear ya kuonya endeleeni tu kutukana mukidhani muna Mjenga anayewatuma
 
Unaweza kudai unampenda sana Rais na hutaki kwa namna yoyote ile atukanwe au akosolewe. Hayo mapenzi yako unayoyasema mbele ya kamera, hakuna anayeweza kuyapima wala kuyathibitisha.

Unatengeneza aina fulani za siasa ambazo kwa bahati mbaya hujui madhara yake yanaweza kuwa makubwa kiasi gani.

Kwa taarifa yako ni kwamba ile radio ya kule Rwanda ambayo ilichochea maasi, haikuwa ikiendeshwa kwa gharama kubwa. Sawa sawa na gharama za utoaji wako wa habari.

Gharama za kufikisha ujumbe ni ndogo lakini madhara ya ujumbe wa radio ile yalikuwa ni vifo vya watu zaidi ya watu laki nane wasio na hatia yoyote ile. Kaka mkubwa Cyprian wenye mapenzi na ufanisi wa kazi anazofanya mheshimiwa JPM ni wengi.

Bahati mbaya kati ya hao hao team JPM wapo ambao wanakwazika na ujumbe wako, wapo ambao wanawaheshimu wazee ambao unapowataja majina ni kama vile unawazungumzia wanafunzi mliomaliza la saba au kidato cha sita pamoja.

Haipendezi kukuona kila baada ya siku chache ukijibizana na watu, huku mkiwa mnakejeliana na kutukanana, hii ni cheap politic, haiwezi kuwa na tija itakayodumu kwa miaka mingi kuanzia leo.

Nakutakia mwaka 2019 wenye mafanikio, lakini anza kwanza kwa kubadili approach ambayo inakufanya utengeneze maadui kumi na rafiki moja kila unaporusha hewani video clip mpya.
Ebwana na hivi..mkitaka huyo jamaa anyamaze kimya basi waambieni wazee wenu waache fitina na propaganda za chini chini za kisiasa..waache
 
Fitina za chini chini zipo mpaka huko Marekani na Russia, zimekuwepo kabla hata huyo bro hajazaliwa.

Hauujibu moto kwa kuwasha moto mwingine, busara ni kitu cha muhimu kuwa nacho.
 
Musiba anawadharau watu kwa kuwaandika vibaya,hajui kesho hao anaowadharau watakuwa nani,shauri yake ajue kila lenye mwanzo huwa na mwisho wake.
 
Kalewa ushawishi alionao katika awamu ya tano. Historia ipo kwa ajili ya kila mtu kujifunza kitu fulani.

Wako wapi wajanja wa awamu ya Mzee Mwinyi?. Wako wapi wajanja wa awamu ya Mkapa?. Wako wapi wajanja wa awamu ya JK?.

Anatukana wazee ambao wanao ushawishi wa miaka mingi, wanaweza wao wasishughulike nae, akaja kushughulikiwa na vijana wa wazee hao ambao siku zote wanakumbuka fadhila zao.
 
Unaweza kudai unampenda sana Rais na hutaki kwa namna yoyote ile atukanwe au akosolewe. Hayo mapenzi yako unayoyasema mbele ya kamera, hakuna anayeweza kuyapima wala kuyathibitisha.

Unatengeneza aina fulani za siasa ambazo kwa bahati mbaya hujui madhara yake yanaweza kuwa makubwa kiasi gani.

Kwa taarifa yako ni kwamba ile radio ya kule Rwanda ambayo ilichochea maasi, haikuwa ikiendeshwa kwa gharama kubwa. Sawa sawa na gharama za utoaji wako wa habari.

Gharama za kufikisha ujumbe ni ndogo lakini madhara ya ujumbe wa radio ile yalikuwa ni vifo vya watu zaidi ya watu laki nane wasio na hatia yoyote ile. Kaka mkubwa Cyprian wenye mapenzi na ufanisi wa kazi anazofanya mheshimiwa JPM ni wengi.

Bahati mbaya kati ya hao hao team JPM wapo ambao wanakwazika na ujumbe wako, wapo ambao wanawaheshimu wazee ambao unapowataja majina ni kama vile unawazungumzia wanafunzi mliomaliza la saba au kidato cha sita pamoja.

Haipendezi kukuona kila baada ya siku chache ukijibizana na watu, huku mkiwa mnakejeliana na kutukanana, hii ni cheap politic, haiwezi kuwa na tija itakayodumu kwa miaka mingi kuanzia leo.

Nakutakia mwaka 2019 wenye mafanikio, lakini anza kwanza kwa kubadili approach ambayo inakufanya utengeneze maadui kumi na rafiki moja kila unaporusha hewani video clip mpya.
mbona unampa sifa asiyostahili.. ni bora ungemuita kijakazi wa JIWE ungeeleweka
 
Musiba anawadharau watu kwa kuwaandika vibaya,hajui kesho hao anaowadharau watakuwa nani,shauri yake ajue kila lenye mwanzo huwa na mwisho wake.
kuna jamaa mmoja kipindi kilee cha MZEE WA MSOGA aliwahi kumwambia mtu fulani ''SIONGEI NA MMBWA NAONGEA NA MWENYE MMBWA'' baada ya muda kadhaa kupita mwenye mmbwa akasafiri akamuachia MMBWA ulinzi na majukumu yoote ya nyumba ile yawe chini yake. kilichfuatia yule jamaa akapotea kimyakimya sijui yuko wapi...
sasa ngoja mwenye mmbwa arudi upyaa tuone mmbwa ataendelea kubwaka??!!
 
Back
Top Bottom