Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,473
- 13,629
Unaweza kudai unampenda sana Rais na hutaki kwa namna yoyote ile atukanwe au akosolewe. Hayo mapenzi yako unayoyasema mbele ya kamera, hakuna anayeweza kuyapima wala kuyathibitisha.
Unatengeneza aina fulani za siasa ambazo kwa bahati mbaya hujui madhara yake yanaweza kuwa makubwa kiasi gani.
Kwa taarifa yako ni kwamba ile radio ya kule Rwanda ambayo ilichochea maasi, haikuwa ikiendeshwa kwa gharama kubwa. Sawa sawa na gharama za utoaji wako wa habari.
Gharama za kufikisha ujumbe ni ndogo lakini madhara ya ujumbe wa radio ile yalikuwa ni vifo vya watu zaidi ya watu laki nane wasio na hatia yoyote ile. Kaka mkubwa Cyprian wenye mapenzi na ufanisi wa kazi anazofanya mheshimiwa JPM ni wengi.
Bahati mbaya kati ya hao hao team JPM wapo ambao wanakwazika na ujumbe wako, wapo ambao wanawaheshimu wazee ambao unapowataja majina ni kama vile unawazungumzia wanafunzi mliomaliza la saba au kidato cha sita pamoja.
Haipendezi kukuona kila baada ya siku chache ukijibizana na watu, huku mkiwa mnakejeliana na kutukanana, hii ni cheap politic, haiwezi kuwa na tija itakayodumu kwa miaka mingi kuanzia leo.
Nakutakia mwaka 2019 wenye mafanikio, lakini anza kwanza kwa kubadili approach ambayo inakufanya utengeneze maadui kumi na rafiki moja kila unaporusha hewani video clip mpya.