Kaitwa Mbowe, wengine mnaenda kufanya nini?

Kaitwa Mbowe, wengine mnaenda kufanya nini?

Mwendesha mashitaka wa kesi hiyo alikuwa J.C.Summerfied na Mwalimu Nyerere alitetewa na mawakili watatu, D.N.Pritt aliyekuwa wakili kiongozi akisaidiwa na Wakili Mahamoud Rattansey na Wakili K.L.Jhavery.

Walalamikaji walikuwa wakoloni wa Kiingereza, Mkuu wa Wilaya ya Musoma na Geita F.B.Weeks na mwingine Mkuu wa Wilaya ya Songea G.T.Scotts. Ilidaiwa kuwa Mwalimu Nyerere aliwakashifu viongozi hao katika mikutano yake ya hadhara na kwa kuandika makala kwenye kigazeti kiitwacho Sauti ya Tanu.

Akiwa mahakamani mwendesha mashitaka ambaye pia alikuwa mkoloni wa Kiingereza alisema: "Julius Kambarage Nyerere unashitakiwa, kwanza kwa kumkashifu DC Weeks wa Musoma katika makala yako ya ''Sauti ya Tanu'' Namba 58 ya tarehe 27 Mei 1958. Pili, Katika gazeti hilohilo ulimkashifu pia DC Scotts wa Songea.

Mwendesha mashitaka akaendelea: "Tatu, unashitakiwa kwa kuwakashifu kwa pamoja maafisa hao wa serikali. Baada ya kusomewa mashitaka mambo yalikuwa hivi:
Mwendesha mashitaka: Ni kweli au hapana
Mwalimu Nyerere: Hapana.

Kesi iliahirishwa hadi Julai 16, 1958 ambapo siku hiyo Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw.J.C.Cole alilazimika kufika mahakamani yeye binafsi. Shitaka la kwanza liliondolewa. Shitaka la pili lilifanyiwa marekebisho.

Katika utetezi wake, Mwalimu Nyerere alikiri kuwa yeye ndiye aliyechapisha gazeti la ''Sauti ya Tanu'' na kwamba maneno yaliyopo kwenye gazeti hilo yanayowahusu wakuu wa wilaya hao aliyaandika akiwa na lengo la kuitaka serikali ya kikoloni itupie macho malalamiko ya watu.

Alisisitiza kuwa chama cha Tanu kilikuwa na wanachama 300,000 na lengo lake lilikuwa ni kupatikana uhuru wa Tanganyika bila kusababisha vurugu.

Hukumu ya kesi hiyo ilitolewa Agosti 13, 1958 na Mwalimu Nyerere alipatikana na hatia ya makosa mawili ya uchochezi kwa kuwaita wakuu wa wilaya, mashetani na maharamia. Hakimu Davies alisema:

"Nimegundua kuwa Nyerere ni mtu mwenye busara nyingi. Ni mtu mwajibikaji katika jamii. Si jambo la kawaida kutoa adhabu ya kifungo kwa makosa kama haya… mimi sitaki kujitenga na desturi hiyo. Namtoza mshitakiwa faini ya shilingi 3,000 au kwenda jela miezi 6. Nampa mshitakiwa muda wa siku mbili kulipa faini hiyo.''

Baada ya hukumu hiyo kutolewa nyimbo na nderemo zilitawala mahakamani hapo, akina mama ambao walikuwa wamezoea kuzingira jengo hilo kufuatilia kesi hiyo kila ilipotajwa, walishangilia kwa msisimko wakiongozwa na Bibi Titi Mohammedi.

Baada ya kupeana mikono na mawakili wake, Nyerere aliingia katika gari kurejea nyumbani kwake Magomeni Mikumi akifuatana na makamu wake wa Tanu, John Rupia na viongozi wengine wa chama.
 
Mliopo Ufipa na kwingineko tupeni updates ikiwa ni pamoja na picha, na kinachoendelea hadi mwisho yale yanayojiri katika maandamano ya wanachadema ya kumsindikiza kamanda Mbowe makao makuu ya polisi.

Vile vile nipeni majibu ya hoja hii; KINA LISSU NA JOPO LAKE LA MAWAKILI, JE NI MAWAKILI WA CHAMA? kama ni mawakili wa chama, mbona hawana desturi ya kuwatetea wanachama katika kesi mbalimbali kama kinA LWAKATARE bali wanaonekana kwenye issue za VIONGOZI WA CHAMA TU? tujadili kwa ustaarabu!
 
mkuu nikumbushe mawakili wa lwakatare
 
Kama wameenda na wengine wewe kinachokuuma ni nini? Kwani rafiki yako huwezi kumsindikizwa akiitwa polisi au mahakamani? Hivi msome hadi level gani ya elimu kuelewa kuwa nchi inahitaji mabadiliko? Masikini wangapi waendelee kuteseka ili ujue tunanyonywa? Yatima na wajane wapi na wapi waendelee kulia vilio vya kusaga meno ili mjue wanateseka? Watoto wa mitaani walale njaa siku ngapi mjue wanastahili keki ya taifa? Tufe na kuumizwa kwa virungu miaka mingapi ili mjue wananchi wa kawaida nasi ni waTanzania? Tuteseke kiasi gani vijana kwa kutafuta ajira mnazogawa kiupendeleo na hamuachii vyeo? Tusomeshe wadogo zetu na watoto wetu mara ngapi wa-resit bila kufaulu ktk uongozi wenu? Tulie mara ngapi tulioajiriwa kwa mishahara midogo tukatupwa vijijini kusiko barabara, maji safi wala nyumba bora za kuishi? Tuteseke kiasi gani waTanzania wa kawaida tunaolipa kodi lukuki nanyi mnazivunia matumboni mwenu? Tufanye nini sisi mnaotulazimisha tusiwe na Tanganyika yetu ili hali Zanzibari yao wanayo? Nyimbo hii ni ya kijana yatima mtu mzima masikini mimi wa Ludewa kuliko na madini mengi, ziwa, ardhi, misitu, milima, mabonde, mito mikubwa hakuna umeme, barabara ya vumbi, umaskini uliokithiri, yatima na wajane tele!!

Naimba mimi......... Ni wimbo tuu........
 
Si vema mtu kujitafutia matatizo bila sababu yeyote. Kuitwa kwa Mbowe makao makuu ya polisi ambao hamjaitwa mnaenda kufanya nini? Ama tuseme kauli ya Mbowe ilikuwa kauli ya Chadema na mawakili wake?

Waandamanaji wa chadema huwa wanabeba visu, nondo na bisibisi mifukoni na kwenye soksi, pia hubeba mapanga kwenye makoti makubwa ili kwenda kupambana na polisi. Hivyo siyo vita ni nini? Ni vema wanachadema kufuata utaratibu, hakuna haja ya kutumia nguvu kujitafutia matatizo.

Mwacheni Mbowe aende kama alivyoitwa, kama atasema alitumwa na chadema na mawakili wake, kila mmoja ataitwa kwa wakati wake.
Vp mdau jana ulilala wapi mbona umeamka na mapovu?Kwani akienda na wafuasi kuna tatizo kwasababu kwenye wito haukusema tena asije na Gari la KUB sababu dereva pia atamsindikiza.Aliambiwa aende kumwona DPP so wacha watu watumie haki yao.Kaja na fuso ya watu hayakuhusu wewe subiri tshirt na khanga za kijani basi
 
Mwenyekiti wa CCM anapokuwa kwenye ziara mbalimbali za kikazi ndani ya nchi na nje ya nchi ndege nzima huwa wanajaa watu wengine ambao siyo marais na wanakuwa hawajaitwa,kazi inayokwenda kufanyika ni ya Rais.Je hao watu wanaoandamana na Rais kwenye kazi zinazo muhusu Rais huwa wanakwenda kufanya nini?.

kwahiyo mbowe ni raisi wa nchi gani?
 
Mbowe ni mwenyekiti wa chama, nyuma ya Mbowe kuna wafuasi kwa mamillion, sasa lazima wajue mnamwitia nini? na nini kitaendelea pale - mbona unakuwa na wasiwasi kama mwizi wa bata.

wakiitwa wanawake nawe unaenda siyo hata kama siyo mwanamke?
 
Mwendesha mashitaka wa kesi hiyo alikuwa J.C.Summerfied na Mwalimu Nyerere alitetewa na mawakili watatu, D.N.Pritt aliyekuwa wakili kiongozi akisaidiwa na Wakili Mahamoud Rattansey na Wakili K.L.Jhavery.

Walalamikaji walikuwa wakoloni wa Kiingereza, Mkuu wa Wilaya ya Musoma na Geita F.B.Weeks na mwingine Mkuu wa Wilaya ya Songea G.T.Scotts. Ilidaiwa kuwa Mwalimu Nyerere aliwakashifu viongozi hao katika mikutano yake ya hadhara na kwa kuandika makala kwenye kigazeti kiitwacho Sauti ya Tanu.

Akiwa mahakamani mwendesha mashitaka ambaye pia alikuwa mkoloni wa Kiingereza alisema: “Julius Kambarage Nyerere unashitakiwa, kwanza kwa kumkashifu DC Weeks wa Musoma katika makala yako ya ‘’Sauti ya Tanu’’ Namba 58 ya tarehe 27 Mei 1958. Pili, Katika gazeti hilohilo ulimkashifu pia DC Scotts wa Songea.

Mwendesha mashitaka akaendelea: “Tatu, unashitakiwa kwa kuwakashifu kwa pamoja maafisa hao wa serikali. Baada ya kusomewa mashitaka mambo yalikuwa hivi:
Mwendesha mashitaka: Ni kweli au hapana
Mwalimu Nyerere: Hapana.

Kesi iliahirishwa hadi Julai 16, 1958 ambapo siku hiyo Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw.J.C.Cole alilazimika kufika mahakamani yeye binafsi. Shitaka la kwanza liliondolewa. Shitaka la pili lilifanyiwa marekebisho.

Katika utetezi wake, Mwalimu Nyerere alikiri kuwa yeye ndiye aliyechapisha gazeti la ‘’Sauti ya Tanu’’ na kwamba maneno yaliyopo kwenye gazeti hilo yanayowahusu wakuu wa wilaya hao aliyaandika akiwa na lengo la kuitaka serikali ya kikoloni itupie macho malalamiko ya watu.

Alisisitiza kuwa chama cha Tanu kilikuwa na wanachama 300,000 na lengo lake lilikuwa ni kupatikana uhuru wa Tanganyika bila kusababisha vurugu.

Hukumu ya kesi hiyo ilitolewa Agosti 13, 1958 na Mwalimu Nyerere alipatikana na hatia ya makosa mawili ya uchochezi kwa kuwaita wakuu wa wilaya, mashetani na maharamia. Hakimu Davies alisema:

“Nimegundua kuwa Nyerere ni mtu mwenye busara nyingi. Ni mtu mwajibikaji katika jamii. Si jambo la kawaida kutoa adhabu ya kifungo kwa makosa kama haya… mimi sitaki kujitenga na desturi hiyo. Namtoza mshitakiwa faini ya shilingi 3,000 au kwenda jela miezi 6. Nampa mshitakiwa muda wa siku mbili kulipa faini hiyo.’’

Baada ya hukumu hiyo kutolewa nyimbo na nderemo zilitawala mahakamani hapo, akina mama ambao walikuwa wamezoea kuzingira jengo hilo kufuatilia kesi hiyo kila ilipotajwa, walishangilia kwa msisimko wakiongozwa na Bibi Titi Mohammedi.

Baada ya kupeana mikono na mawakili wake, Nyerere aliingia katika gari kurejea nyumbani kwake Magomeni Mikumi akifuatana na makamu wake wa Tanu, John Rupia na viongozi wengine wa chama.

habari yako inaweza kuwa muhimu kwangu, nikipata muda nitaisoma inshalla.
 
Si vema mtu kujitafutia matatizo bila sababu yeyote. Kuitwa kwa Mbowe makao makuu ya polisi ambao hamjaitwa mnaenda kufanya nini? Ama tuseme kauli ya Mbowe ilikuwa kauli ya Chadema na mawakili wake?

Waandamanaji wa chadema huwa wanabeba visu, nondo na bisibisi mifukoni na kwenye soksi, pia hubeba mapanga kwenye makoti makubwa ili kwenda kupambana na polisi. Hivyo siyo vita ni nini? Ni vema wanachadema kufuata utaratibu, hakuna haja ya kutumia nguvu kujitafutia matatizo.

Mwacheni Mbowe aende kama alivyoitwa, kama atasema alitumwa na chadema na mawakili wake, kila mmoja ataitwa kwa wakati wake.
Mbona unatetemeka. Polisi wenyeqe mi macho imewatoka..
 
kesi iliishaje? Kama hajatelekezwa!
Hivi FISIEM wanao mawakili wanaotetea wanachama au watanzania maana watanzania wamekuwa na hichi chama toka enzi, aisee kumbe zile story za watanzania kusingiziwa makosa ya jinai za kuozea jela ni uongo!
 
Mbowe ni kiongozi wa watu. Aliyoyasema si yake Bali ni ya watu anaowaongoza na ndiyo maana wako nyuma yake.
 
kupitia hii thread nimeamini watanzania wengi niwa dumavu wa akili.....
 
Back
Top Bottom