Kainerugaba Msemakweli anatumiwa - Saed Kubenea

nyabhingi

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2010
Messages
14,088
Points
2,000

nyabhingi

JF-Expert Member
Joined Oct 12, 2010
14,088 2,000
Katika makala yake kwenye gazeti la mwanahalisi la septemba 7,2011, Kubenea anasema msema kweli anatumiwa pale anaposema CCM hawakuiba fedha za EPA kwa ajili ya uchaguzi wa 2005 wakati ushahidi upo wazi kuwa fedha zilichotwa kuanzia septemba 2005 kwa maelekezo maalum ya rais mkapa.

Anasema wanaomtumia Msemakweli ni wapambanaji hewa wa ufisadi..Na Saed Kubenea - Imechapwa 07 September 2011

MTU huyu anatumika kuficha ukweli. Ni Kainerugaba Msemakweli. Anasema mabilioni ya shilingi yaliyokwapuliwa na kampuni ya Kagoda Agriculture Limited (KAL), ndani ya Benki Kuu ya taifa (BoT) hayakutumika kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.

Anasema wezi wa Kagoda walichota fedha BoT, Februari 2006, na kwamba uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani ulimalizika Novemba 2005. Yote haya yanaonyesha jinsi Msemakweli, ama anavyotumika bila kujijua, au anavyotumiwa na watu wenye malengo binafsi.

Kile ambacho wengi hawajakifahamu, ni nani anayemtumia Msemakweli. Je, aweza kuwa anatumiwa na Kagoda au anatumiwa na wapinzani wa Kagoda?

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari (Alhamisi iliyopita jijini Dar es Salaam, Msemakweli amekuja na madai mawili makubwa. Kwanza, fedha za Kagoda hazikutumika kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2005. Anasema ushahidi wake ni "nyaraka zinazoonyesha Kagoda iliiba fedha BoT, Februari 2006 na ilizisafirisha nje ya nchi Machi 2006."

Pili, Msemakweli anatetea Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa hakikutumia sehemu ya fedha hizo kuingia madarakani. Hatua hii inaleta maswali mengi kuliko majibu; yakiwa ni pamoja na iwapo Msemakweli anafahamu anachikitenda.

Kwanza, hati ya kiapo ya wakili Bhyidinka Sanze wa kampuni ya mawakili ya Malegesi – Malegesi Law Chambers – ya Dar es Salaam, kwa Kamati ya rais ya kushughulikia wizi kwenye akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), inaeleza fedha za Kagoda ziliibwa ili kufanikisha kampeni za CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.

Sanze anakiri kuwa ni yeye alishuhudia "…mikataba ya Kagoda na makampuni mengine ya nje."

Andishi lake linaeleza kuwa Rostan Aziz, Peter Noni na Bered Malegesi walimthibitishia kuwa Rostam alikuwa kwenye kikao ambako rais mstaafu Benjamin Mkapa alitoa maelekezo kwa Gavana wa BoT, Dk. Daudi Ballali kutoa fedha hizo kwa Rostam kwa ajili ya uchaguzi.

Sanze anasema, "Niliitwa na Bw. Malegesi ofisini kwa Bw. Rostam Aziz…Nilipofika…niliwakuta Bw. Rostam Aziz, Peter Noni (Mkurugenzi Mtendaji wa sasa wa benki ya raslimali) na Bw. Malegesi; wakaniambia fedha hizo zinahitajika kwa ajili ya kugharamia uchaguzi wa CCM na rais wake."

Hili ni andishi ambalo mpaka sasa halijakanwa na serikali, Mkapa, Rostam, Sanze, Meregesi wala Peter Noni.

Je, Msemakweli anayedai amefanya utafiti wa suala hili kwa miaka miwili mfulululizo hajaliona andishi hili? Hakulitafuta? Kama ameliona, kwa nini anataka kuficha ukweli? Kama hakuliona, kwa nini hakuuliza walilonalo?
Kama hakuliona andishi la Sanze, hakulitafuta na hakuuliza walilonalo, anatoa wapi ujasiri wa kusema, "fedha za Kagoda hazikuibwa kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2005?" Anamtumikia nani na nani anataka kumuokoa au kumzamisha?

Kampuni ya Kagoda ilikwapua jumla ya dola za Kimarekani 30,732,658.82 (Sh. 40 bilioni) katika Akanuti ya Madeni ya Nje (EPA), ndani ya BoT.

Fedha hizi ziliibwa kati ya Septemba 2005 na Novemba 2005. Kagoda ilifanikiwa kuchukua fedha BoT na kuzipitisha katika matawi saba ya benki ya CRDB jijini Dar es Salaam kwa mtindo wa "kuingiza na kutoa papo hapo."

Aidha, serikali imekuwa ikijikanyaga kuhusu wizi huu. Aliyekuwa waziri wa fedha, Zakia Meghji aliwaandikia maodita wa kampuni ya Deloitte & Touche ya Afrika Kusini akisema, fedha za Kagoda zilitumika kwa "kazi za usalama wa taifa."

Katika barua yake ya 15 Septemba 2006, Meghji anasema, "Kama unavyofahamu vema, mamlaka ya serikali huwa na siri, vilevile haja ya kugharamia matumizi ya busara.

"Kwa hiyo... malipo ya dola 30,732,658.82 za Marekani yaliyofanywa na BoT kwa Kagoda Agriculture Limited, yaliidhinishwa na serikali kugharamia matumizi yake nyeti na ilikuwa lazima kuchukua hatua hii ya kudumisha usiri huu."

Msemakweli anajichanganya pia katika eneo jingine ambamo anamtaja mmoja wa wafanyabiashara mashuhuri nchini, kwamba ndiye aliyesafirisha fedha hizo Machi 2006.

Lakini nyaraka ambazo amezitumia kupeleka shauri hilo kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), zinaonyesha mfanyabiashara anayemtaja, ameingia mkataba wa kukopeshana fedha na Kagoda 12 Septemba 2005, kipindi ambacho Kagoda yenyewe ilikuwa haijasajiliwa.

Kuna visingizio vingi vimetumika kuhalalisha wizi huu na kutaka kuisafisha CCM. Kwa mfano, mara kadhaa serikali kupitia Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupamnbana na Rushwa nchini (TAKUKURU), Waziri wa Fedha, Mustaph Mkullo, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba na DPP, Eliezer Feleshi wamedai, kwa nyakati tofauti kuwa Kagoda haifahamiki na haijulikani iliko.

Lakini ni Kagoda inayodaiwa kumuondoa nchini aliyekuwa gavana wa BoT, Dk. Daud Ballali. Baadaye serikali ikaeleza, "gavana Ballali ameaga dunia."

Pili, Msemakweli anasema fedha zisingeibwa mwaka 2006 ili kutumika mwaka 2005. Hata kama tukikubaliana na Msemakweli, kwamba fedha ziliibwa benki mwaka 2006, bado huo hauwezi kuwa utetezi.

Je, haiwezekani wezi wa Kagoda wakaipa CCM fedha mwaka 2005 kwa makubaliano kuwa wajilipe mwaka 2006 kwa kutumia EPA?

Nyaraka zinaonyesha kuwa hata kabla kampuni hiyo kusajiliawa, Kagoda tayari ilishachota sehemu ya fedha ilizokwapua.

Kwa mfano, aliyeitwa Meneja Mkuu wa Kagoda, John Kyomuhendo anaonekana akimwandikia Gavana wa BoT tarehe 12 Septemba 2005. Barua nyingine ya Kagoda, ikikumbushia nia ya kuhamisha fedha kutoka BoT iliandikwa tarehe 7 Oktoba 2005.
Naye gavana anajibu mawasiliano hayo kwa barua Kumb. Na. 6054/1355 ya 13 Oktoba 2005 inayofuatwa na barua ya Kagoda ya 20 Oktoba ikielekeza uhamishaji wa fedha kwenda benki.

Maelekezo ni kwamba fedha hizo ziwekwe kwenye akaunti Na. 01J021795700 iliyoko benki ya CRDB tawi la Holland jijini Dar es Salaam.

Barua kutoka Kagoda inayoelekeza jinsi ya kuhamisha zaidi ya Sh. 25 bilioni ilipokelewa na benki siku hiyohiyo ya 20 Oktoba 2005, kuwekwa katika faili na kupewa namba (folio) 7.

Wakati mawasiliano yote yakifanyika, ikiwa ni pamoja na kuchota mabilioni ya shilingi, Kagoda ilikuwa haijasajiliwa. Biashara ilikuwa "mali kauli."

Kagoda ilisajiliwa na Msajili wa Makampuni (sasa wakala wa usajili wa makampuni – BRELA) tarehe 29 Septemba 2005 na kupewa hati Na. 54040, huku wakiwa tayari wamekwapua mabilioni ya shilingi kwa kauli tu.

Pamoja na uhalifu huu wa wazi wa Kagoda, kwa kushirikiana na BoT, ambao ulifahamika kwa wajumbe wa Timu ya Rais na bila shaka kwa rais mwenyewe, Msemakweli anataka kulinda wezi.

Hapa inaonyesha jinsi Msemakweli alivyokuwa tatizo badala ya suluhisho katika sakata la Kagoda. Kisheria, Msemakweli anageuka shahidi tata au shahidi adui, na kwamba vyombo vya – upelelezi (ofisi ya DCI, DPP na TAKUKURU), ni sharti viwe makini naye.

Shahidi anayefunua ukweli na kuufunika hapohapo huwa ana dalili za kutumiwa na wale anaodai kuwa anawashitaki bila yeye kujijua. Msemakweli anajua, kwamba Rais Jakaya Kikwete aliunda Kamati Maalum ya rais ya kufuatilia walioiba benki. Anafahamu Kamati Maalum ya rais ilivyomweleza Rais.

Kwamba baadhi ya wezi waliorudisha fedha na kusamehewa kinyume cha sheria, wanalalamika kutapeliwa kwa kuwa wamelazimika kurudisha hata fedha ambazo walizigawa kwa CCM ili kufanikisha harakati zake za uchaguzi mkuu wa 2005. Miongoni mwao, ni Kagoda Agriculture Limited.

Kama Msemakweli hayafahamu haya, basi hana sababu ya kusema amefanya utatiti. Aseme, "Nimehadithiwa na walionituma." Ikiwa wezi wenyewe wanakiri kurudisha fedha kwa niaba ya Kagoda, Msemakweli anapata wapi ujasiri wa kuisafisha CCM kuwa haikuchukua fedha hizo?

Vilevile, wanaotuhumiwa kuiba fedha kwa mgongo wa Kagoda, wanalalamikiwa na baadhi ya wana-CCM, kwamba hawakuwakilisha fedha yote waliyoiba benki ndani ya
chama. Badala yake, wanadaiwa kutumia fedha hizo kujitajirisha binafsi.

Ni utajiri huo ndio unaotumika kuwanyanyasa wale ambao hawakupata mgawo. Je, madai haya ni ya uongo? Kama ndiyo, mbona ndani ya CCM kumeibuka minyukano isiyoisha, inayotokana na tuhuma za wizi wa fedha hizo, kwamba baadhi ya wanaotuhumiwa kushiriki wanasema zimetumika kuingiza serikali hii madarakani?
Rais Kikwete mwenyewe siyo tu anaamini hivyo, bali mbele ya wananchi anatazamwa kama mtoto wa Kagoda na mjukuu wa EPA.

Hata baadhi ya wananchi wa kawaida, wakiwamo wana-CCM na viongozi wake, wanaamini Kagoda ndiyo iliingiza serikali hii madarakani. Kagoda ndiyo sababisho la minyukano isiyokwisha ndani ya chama.

Aidha, ni kiini cha kuibuka kwa tamthilia mpya ya kujivua gamba na ndiyo sababu ya serikali kuingia katika uchaguzi mdogo wa ubunge jimboni Igunga, miezi 10 baada ya kumalizika uchaguzi mkuu.

Katika mazingira haya, wananchi wamebaki na jambo moja la kuamini. Kwamba ni kweli kuwa Msemakweli ametumwa na waliomtuma wanafahamika. Ni wale waliokuwa mstari wa mbele kujionyesha wanapambana na ufisadi, lakini papohapo wakikumbatia ufisadi wa kisingizio cha kuitetea CCM.

Ndiyo msingi wa madai yake haya. Kwamba "fedha za Kagoda hazikutumiwa kufanikisha mgombea wa CCM kuingia madarakani."

Jambo moja ni muhimu. Hatua ya Msemakweli kutetea CCM, kwamba haikutumia fedha za Kagoda katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, inazidisha kiu ya wananchi kutaka kufahamu Kagoda ni nani na ana uhusiano gani na Msemakweli anayemtetea?

Jingine ambalo wananchi watataka kufahamu kwa kutumia mizani ya Msemakweli, ni serikali inashughulikia vipi "ukweli" aliousema Msemakweli na kuachana na propaganda zake za kuwasafisha wezi.
 

zumbemkuu

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2010
Messages
10,025
Points
2,000

zumbemkuu

JF-Expert Member
Joined Sep 11, 2010
10,025 2,000
ngoja tuendelee kusubiri data! lakini ushahidi wa msemakweli haujaonyesha popote kuwa fedha za kagoda zilitumiwa na CCM, pesa za EPA zimechotwa kwa staili nyingi, inawezekana hizo zilizosaidia CCM ndo hazikupitia kagoda.
 

lifeofmshaba

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2011
Messages
868
Points
195

lifeofmshaba

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2011
868 195
hivi kuna watu wana hati miliki ya nchi hii?
yaani kuna watu hawataki mtu atoe neno lazima watamvamia
kama kubena ana info za kulikoa ili taifa au kumpinga msemakweli kwa data na sio kwa KEEYBOARD na maneno
mengi ya kuungaunga
 

Daniel Anderson

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2011
Messages
877
Points
0

Daniel Anderson

JF-Expert Member
Joined Aug 7, 2011
877 0
Kila post mawazo ni 'anatumiwa' tu! Upupu mwingine wa wachangiaji. Kwani na ninyi mnatumiwa? Nini? Kutoka wapi? Mnapokeaje hizo sijui zawadi mnazotumiwa? Mliomba ndo mkatumiwa?
Sijui ni nini kutumiwa? Msamiati huu kiinglish chake ni kipi? Kama kutumiwa ni vibaya acheni nanyi kutumiwa kabla hamjasema Kubenea na Msemakweli wanatumiwa.
 

only83

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2010
Messages
5,343
Points
2,000

only83

JF-Expert Member
Joined Oct 15, 2010
5,343 2,000
Katika makala yake kwenye gazeti la mwanahalisi la septemba 7,2011, Kubenea anasema msema kweli anatumiwa pale anaposema CCM hawakuiba fedha za EPA kwa ajili ya uchaguzi wa 2005 wakati ushahidi upo wazi kuwa fedha zilichotwa kuanzia septemba 2005 kwa maelekezo maalum ya rais mkapa.

Anasema wanaomtumia Msemakweli ni wapambanaji hewa wa ufisadi..
Jamani mbona mnatuchanganya watanzania......Kwanini wapambanaji mnaanza kuumana wenyewe kwa wenyewe tena.......
 

DSN

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2011
Messages
2,836
Points
1,250

DSN

JF-Expert Member
Joined Feb 2, 2011
2,836 1,250
Kosa la WanaCCM lilikikua ni kuwakubali watu waliojitanabaisha kuwa wana mbinu na mikakati ya kutengenezea pesa kwa ajili ya CCM.Kwa hiyo CCM kama Chama has nothing to do with that dirty game of some few CCM leaders.Hakika tufike sehemu kitanzi hiki ni lazima kiwaangukie watu na sio Taasisi [Institution]

Na Watanzania wengi sana kwa sasa hili swala la EPA wanakubali kupumbuzwa na MAFISADI kulifanya kuwa ni kitaasisi kumbe ni wezi wachache tu ambao kama mchakato ukikaa vyema basi wahusika wafikishwe mahakamani.

Tatizo Watanzania tunajenga utamaduni wa kulewa na kukumbatia kuwa tunatoa lawama za kitaasisi baada ya kuwa tuna lawama za watu binafsi kama watu binafsi.Ndio maana wenzetu walioendelea wao lawama uenda kwa mtu binafsi kama yeye hata kama ilikuwa ni kwa dhamana ya taasisi aliyopewa.

Kuna kiongozi wa kitaifa wa zama hizo alipopewa taarifa ya pesa ilivyokwapuliwa wakati wa EPA,alishika kichwa na kupiga ukete.Lakini walioinjinia mkakati ule ifike sehemu watajwe kwani walipokuwa wanatoa vimemo kwa wahindi na waarabu huyu asikilizwe walitegemea nini?

Wazee ambao wamechafuliwa kwa kashfa hizo za EPA wajitokeza kujisafisha Watanzania kwa kuwa ukweli ukidhihiri uongo ujitenga na nafsi zenu zitakuwa huru na uenda mkapata piece of mind,mkatumia muda huu uliosalia kulea wajukuu zenu kwa amani.
 

Nangetwa

Senior Member
Joined
Feb 9, 2009
Messages
134
Points
170

Nangetwa

Senior Member
Joined Feb 9, 2009
134 170
Ingekuwa vizuri kama Kubenea angesema Msemakweli anatumiwa na nani. Naye alete ushahidi wa jinsi fedha hizo zilivyotumika ili tusome na tucheje hizo data kuliko kusema tu mtu anatumiwa. Siasa za bongo zinakuwa hazina tija hata siku hizi. tunataka ushahidi tu.
 

Shapu

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2008
Messages
2,086
Points
1,500

Shapu

JF-Expert Member
Joined Jan 17, 2008
2,086 1,500
Some other people bana hata siwaelewi..... Isue ni kwamba hela ziliibwa full stop. kwamba zilienda wapi is not an issue coz now tunatakiwa kuwashughulikia wezi.
 

tindikalikali

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2011
Messages
4,868
Points
1,195

tindikalikali

JF-Expert Member
Joined Jan 14, 2011
4,868 1,195
Katika makala yake kwenye gazeti la mwanahalisi la septemba 7,2011, Kubenea anasema msema kweli anatumiwa pale anaposema CCM hawakuiba fedha za EPA kwa ajili ya uchaguzi wa 2005 wakati ushahidi upo wazi kuwa fedha zilichotwa kuanzia septemba 2005 kwa maelekezo maalum ya rais mkapa.

Anasema wanaomtumia Msemakweli ni wapambanaji hewa wa ufisadi..
Kubenea kadai, msemakweli ama hajui asemalo au anatumiwa. Acha kuchakachua habari
 

John Marwa

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Messages
275
Points
0

John Marwa

JF-Expert Member
Joined May 25, 2011
275 0
Katika makala yake kwenye gazeti la mwanahalisi la septemba 7,2011, Kubenea anasema msema kweli anatumiwa pale anaposema CCM hawakuiba fedha za EPA kwa ajili ya uchaguzi wa 2005 wakati ushahidi upo wazi kuwa fedha zilichotwa kuanzia septemba 2005 kwa maelekezo maalum ya rais mkapa.

Anasema wanaomtumia Msemakweli ni wapambanaji hewa wa ufisadi..
Kubenea hajamuelewa Msemakweli! Msemakweli anasema hela ya Kagoda haikutumia kwenye kampeni na CCM! hakusema hela ya EPA! Kuna kampuni ya Deep green ambayo haijulikani ukweli wake labda na sio Kagoda kama alivyosema msemakweli! Mimi nampongeza Msemakweli amekuja na Ushahidi kama kuna mtu mwingine nae ana ushahidi wa kagoda auweke hadhalani ili tujue ukweli ni upi na uongo ni upi? Dr slaa alisema anaushahidi wa kagoda ebu nae auweke wazi!
 

Forum statistics

Threads 1,392,476
Members 528,635
Posts 34,110,158
Top