Nyote mnashindwa kuelewa: Kubenea hapingi ushahidi wa Msemakweli kuhusu ukwapuaji wa kagoda kutoka BoT ktk akaunti ya EPA, anachopinga ni timing ya uchotaji huo, kwamba kufuatana na Msemakweli ulifanyika baada ya uchaguzi wa 2005.
Kubenea anasema hii si kweli na lengo ake ni kujaribu kumuokoa JK na CCM yake kutoka kwenye ndoano ya Kagoda -- kwamba akina RA hawakupanga kufanya wizi kwa ajili ya kampeni za JK, bali waliiba kivyao na baadaye kuonyesha kwamba ni CCM ndiyo ilipanga na kuwatuma. Sababu yake ni kupata huruma ya serikali ya CCM na hivyo kulinda shingo zao.
Habari nilizopata ni kwamba Msemakweli anatumiwa na Mzee Mengi -- na ndiyo maana vyombo vyake vya habari vilitangaza sana 'ushahidi' wake kuliko vyombo vingine vya habari. Inawezekana Mengi aliombwa na JK ajaribu kumtenganisha yeye (yaani JK + CCM) na uchotaji huo.
Tusisahau kwamba Mengi ni sapota mkubwa sana wa JK na nadra magazeti yake kumhusisha na ufisadi. Anamuona ni rais safi sana -- isipokuwa wasaidizi wake wakuu wakiwemo akina RA na EL ndiyo mafisadi waliokubuhu.
Kubenea kashindwa kuwajua waliomwagia tindikali, hatajua kama Msemakweli anatatumiwa
Nasema hivi haiajlishi kama anatumiwa au la muhimu ni je anchosema kina ukweli au la. Hivi kama huyu anayetuambia kuwa Msemakweli anatumiwa anataka nini - anatumiwa so what??
Nimeusoma uchambuzi wa Kubenea kuhusu MSEMAKWELI na nilichokiona ni kwamba amekurupuka tu hakufanya research yoyote. Inawezekana ameandika uchambuzi huo kwa shinikizo la watu fulani, kama ambavyo naamini Msemakweli naye ametumwa na watu fulani. Kubenea anapaswa kutuliza kichwa kabla ya kuandika makala zake. Of late naona kama anapoteza mwelekeo. Naweza kukubaliana na baadhi ya watu kuwa huenda naye ANATUMIWA.
Agh! Kubenea anaweza kufanya research? ana ubavu huo? mbona mnamwonea yeye ni kasuku akiambiwa jambo ambalo anaona linaweza kuuza gazeti lake anakurupuka nalo.
Gazeti gani, kwa maoni yako, hufanya research? Jamba Leo? kubenea kaweza kufanikisha kitu kimoja: ikifika Jumatano asubuhi moto huwaka ndani ya chupi za wakuu wa serikali ya magamba! bila kubenea sijui nani angejua kwamba magamba ni wizi mtupu! AAAARRRRGGGGHHHHHH! Pu!
Bujibuji anatumiwa confirmed!
<br />Kanerugaba "<i>If you can't</i> beat <i>them</i>, <i>join them"</i>
kubenea au buji?fafanua anatuniwa ki vipi?
Umesomeka mkuu,Tatizo letu watz ni kwamba tumeibiwa sana, sasa wezi wengi tumewafahamu kiasi ambacho sasa tunabishana ni nani kaiba zaidi, nani kaiba wapi, umebakia ushabiki badala ya kuwakamata wezi