Kainerugaba Msemakweli anatumiwa - Saed Kubenea

Msema kweli anatumia na CCM na ndio maana alijifanya kutangaza kuwa yeye ni CDM katika maelezo yake wakati kulikuwa hakuna jinsi na namna utambuzi wake kichama ulipaswa kuingia pale, badala kuongea ushahidi alionao na jinsi alivyoupa. zaidi ya hapo akasema RA na Manji anawamudu na haofii kabisa.

Lengo lao ni kutaka kumtenganisha EL na RA ili EL asonge mbele zaidi na ionekana wana makosa tofauti kabisa.
 
ngoja tuendelee kusubiri data! lakini ushahidi wa msemakweli haujaonyesha popote kuwa fedha za kagoda zilitumiwa na CCM, pesa za EPA zimechotwa kwa staili nyingi, inawezekana hizo zilizosaidia CCM ndo hazikupitia kagoda.
Kainerugaba alitoa ushahidi wa KAGODA iliyokuwa inahusishwa kusaidia CCM uchaguzi 2005 . Sasa kama kubenea anao ushahidi wa pesa ya Kagoda kutumika kwenye uchaguzi 2005 basi autoe huo ushahidi hadharani na vilevile ushahidi wa jinsi kainerugaba anavyotumiwa.
Hivi maelekezo ya mkapa yalikuwa yanahusu specifically Kagoda au alitoa maelekezo watumie mfuko wa madeni ya nje EPA?
Huwa najiuliza hivi hawa wanasiasa/wanaharakati/waandishi wa habari huwa wana motive gani wanapokuwa wanauanika ufisadi hadharani maana kila mtu anataka kuonekana yeye ndiyo zaidi ya mwenzake badala ya kushirikiana/kusaidiana kwenye front moja kupambana na ufisadi.
 
Kila binadamu anatumiwa kwa mabaya au mazuri. Cha msingi hiyo pesa irudishwe zisaidie kujenga nchi. Danadana hazishibishi tumbo.
 
Katika makala yake kwenye gazeti la mwanahalisi la septemba 7,2011, Kubenea anasema msema kweli anatumiwa pale anaposema CCM hawakuiba fedha za EPA kwa ajili ya uchaguzi wa 2005 wakati ushahidi upo wazi kuwa fedha zilichotwa kuanzia septemba 2005 kwa maelekezo maalum ya rais mkapa.

Anasema wanaomtumia Msemakweli ni wapambanaji hewa wa ufisadi..
Naungana na Saed Kubenea kwamba Kainerugaba anatumiwa na kundi fulani ndani ya CCM katika kukisafisha chama, ukweli usionakificho ni kwamba Kainerugaba amesema KWELI kama alivyotumwa KUSEMA na wale waliomtuma. Hii haimaanishi kwamba Mkapa hakuhusika la hasha, Mkapa ni mtuhumiwa namba 1 wa Kagoda, Kikwete lazima atakuwa ni mtuhumiwa namba 2 wengine wanafuata.
 
kila mtu aliyekamili hapa duniani anatumiwa kwa namna moja au nyingine.
mf nape anatumiwa na ...........
 
Kubenea holds no bona fides required for his position but was shanghaied into the industry by a desire of grabbing easy mammons. He is, therefore, a complete analphabet when it comes to journalism ethics.
 
hawa ndo wale wanaoropoka tu kujitafutia umaarufu wanatudanganya kila siku. oooh fulani fisadi nina ushahidi kama sio fisadi basi akanishitaki mahakamani! tangu lini mwizi anajitanguliza kitanzini? acheni kutuzingua kama mna ushahidi kuweni na uthubutu kama wa msemakweli na kama mnampinga njooni na data za kutushawishi sio kuropoka tu!
 
Hapa kuna hela za Kagoda,
Na hela za EPA kwa ujumla hivyo tuwe makini katika kuchanganua hili.
Pili si lazima uone kwenyee maandishi hela zikitoka Kagoda zikaenda CCM moja kwa moja bila kua na vituo vya kufutia nyayo,
wala hela kuchotwa BAADA na sio KABLA ya uchaguzi nayo inaweza isiwe kigezo cha kuitoa moja kwa moja Kagoda kwenye CCM,
Inawezekana kuna mahali deni lilikopwa kipindi cha Uchaguzi ndio zilikua zinaenda kurudishwa
Nilitegemea kwa ninavyowafahamu hawa jamaa wawili wangeweza kukutana na kubadilishana taarifa ili kila mmoja wao atoke na habari ambayo haitatuchanganya wala kuchanganyana wao wenyewe.
 
hEBU MWENYE HIYO NAKALA YA MSEMAKWELI EMBU ATUANGUSHIE HAPA TAFADHAAAAALI
 
Kwa kusoma na kuangalia kilichopo nyaraka za Msemakweli ni kweli kathubutu kufanya kile ambacho PCCB na DP walidhani ni kichaka cha kuficha ukweli kwa sababu eti walihitaji kushirikiana na umma kuwatambua waliofanya umafya kwenye hela za EPA.

For sure he has done his part, ametumiwa au kwa msukumo wake binafsi sio suala muhimu kwetu. Kama kuna Mtanzania mwingine anajua zaidi ya yale ambayo msemakweli amewasilisha naye atusaidie kwa kufanya yale ambaye mwenzetu ameyasahau au kuyatoa kwa makusudi au hakuyajua kabisa.
 
Msemakweli kwenye ripoti yake amefafanua na kutoa uthibitisho wa kampuni ya kagoda ilivyochota pesa kutoka BOT, kwa kuwahusisha RA na wenzake. Hakusema kazi iliyokwenda kufanyiwa, kama ni kufanya kampeni za M.k.w.e.r.e au vinginevyo
 
Kubenea kashindwa kuwajua waliomwagia tindikali, hatajua kama Msemakweli anatatumiwa
ni kweli alishindwa kumjua aliyemwagia tindikali, lakini aliwajua waliomtuma aliyemwagia tindika.
 
Katika makala yake kwenye gazeti la mwanahalisi la septemba 7,2011, Kubenea anasema msema kweli anatumiwa pale anaposema CCM hawakuiba fedha za EPA kwa ajili ya uchaguzi wa 2005 wakati ushahidi upo wazi kuwa fedha zilichotwa kuanzia septemba 2005 kwa maelekezo maalum ya rais mkapa.

Anasema wanaomtumia Msemakweli ni wapambanaji hewa wa ufisadi..
mapaparazi mbona hawapendani jamani? Ngoja tuone paparazi mwingine Ngongo ata biase kwa nani
 
Kubenea aache kuendekeza njaa, yeye ndiye anayetumiwa kupotosha ukweli. Msemakweli kapeleka vielelezo kwa DPP, yeye ushahidi kamwonyesha nani? Wasomaji wa kageziti alopewa kusimamia watamuhukumu kwa kulinunua kutokana na kuandika uongo na hatimaye kufa.
 
Back
Top Bottom