Kaibiwa hivi hivi!!

Kaibiwa hivi hivi!!

Vituka

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2011
Posts
2,268
Reaction score
1,267
Walipewa mchongo kuwa kuna mhindi mmoja anaenda bureau de change kubadili mijihela ya kutosha. Jamaa wakamlia timing, wakiwa na noah yao, vipande vya watu kama watatu hivi mitaa ya kariakoo. Wakawa kama wanashoot movie, wengine wana mi kamera na wengine kama wanaigiza. Wakati huo mhindi wa watu kaingia bureau kubadili hela hana hili wala lile na yeye alijua jamaa wanashoot movie!

Yule sijui ndo producer alipoona tu mhindi wa watu anatoka mule bureau akasema ' Action!' wale vipande vya wababa wakampiga loba mhindi wa watu masikini! Huku jamaa wenye makamera wakichukua lile tukio kama movie! Mhindi wa watu anakiga kelele jamani naibiwaa mwenzenu! Watu wanaangalia tu wakijua jamaa wanashoot movie! Mara producer akasema 'cut' jamaa weshamwingiza mhindi kwenye noah, haoooo wakatimka nae! wakachukua chao wakamuacha kakodoa macho! Chezea njaa za wabogo wewe!!
 
Lols, si ya kucheka haya..lkn km movie ya bongo Dar es salaam
 
Back
Top Bottom