Nimegundua mwanamke wangu alizaa na aliyekua mpangaji wangu

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
40,388
98,868
Habari wakuu,

Kuna mdada mmoja ni fundi chereheni, ana mtoto mmoja, tuna mahusiano mwaka wa pili huu sasa ila naweza kuyaita mahusiano yetu ni ya msimu (seasonal relationship).

Nilishawahi kuleta uzi wake humu, huu na nikaelezea vema kabisa jinsi gan mahusiano yangu yetu yalivo ya msimu.

Sasa Baada ya mama J kujinunisha kila mara, nikampuuza na zamu ikahamia kwa fundi cherehani. Karibia wiki 3 nzima haipiti siku 2 sijaenda kwake alikojenga. Tunafanya ya kufanya, namhudumia kiasi chake, anashkuru na wote tunafurahi sana.

Sasa wikendi Moja usiku mida ya saa 2 kasoro nikiwa naenda kwake,Kuna sehem Kuna pagale huwa nakunja Kona ya mwisho kabla ya kuingia kwenye uwanja wake ni kama mita 100 TU mbele unakua unaiona nyumba yake ile pale.

Sasa siku hiyo nimefika nikakuta Not kubwa na vipande kadhaa vya bati na mbao vimeziba njia (mchana wake walikua wanapua ile nyumba), ikanibd kusimama kuvisogeza vyote pembeni na kukagua njia nisije kanyaga misumari.

Niko nakagua njia gafla kaja mwanamke wangu mbio mbio anahema, akasema, "Wee, ujue baba V kaja na sasa hivi yuko hapo nyumbani, nakuomba sana we nenda tu tutaonana kesho".

Duh! Moyo ukastuka, nikatamani kukataa kurudi ila nikamkubalia tu na nikamjibu "Sawa". Nikageuza pale pale na kurudi nilikotokea huku nawaza ni kipi kilichomfanya awe na hofu vile wakati alishanambia baba mtoto walishaachana, hamhudumii mtoto na pale kajenga mwenyewe? Hata hivyo, Nikapotezea.

Kwenye mida ya saa 3 na nusu hivi niko njiani naelekea kwangu, akanitumia ujumbe kuwa jamaa keshaondoka niende tena. Nikaona ni Kama vile kanidharau. Nikamjibu tu kuwa "Siwezi tena kuja hapo kwako, nikikuhitaji nitakuita lodge kama zamani. Kilichotokea leo inatosha kupata picha kamili".

Akanipigia na kuanza kujieleza kuwa jamaa alikuja tu kumuona mwanae, hamna lolote zaidi walilofanya. Nikamuuliza kwamba kama ni mzazi mwenzie tu na hawana tena mahusiano aliona shida gani mimi nikifika pale jamaa akiwepo mpaka aje mbio mbio anahema na kunisimamisha?

Akajitetea kuwa aliona inaweza kuwa vurugu pale, maana jamaa yake anawivu sana. Nikamuuliza "Jamaa alete vurugu kwani pale ni nyumbani kwake? Akileta vurugu si ananyooshwa tu, tatizo liko wapi, au nyumba hii ni mali yake wee unanificha ficha tu?"

Nikaongezea, "Ujue nyie wanawake mudda mwingine mna ujinga mwingi sana, usikute jamaa kakujengea nyumba halafu wewe unanidanganya na unanileta hapa tunafanya mapenzi kwenye nyumba yake. Unataka siku moja uskie watu wameuana hapa ndiyo roho yako itasuuzika. Huo Ujinga mimi sitaki, ukweli sifikirii tena kuja hapa kwako."

Alijitetea mengi sana, nikamwambia ili kuja tena hapo lazima kwanza nimjue huyo baba wa mtoto wako ni nani, mambo ya kuishi kwa hofu sitaki.

Akanambia atanambia nikienda tena nyumbani kwake, anayo na picha yake atanionyesha. Nikasema sawa. Nimeenda kwake tumeishia kufanya ya kufanya tu. Kila Nikigusia kuhusu kumjua jamaa au picha yake ananipiga sana chenga na kubadili mada. Nikaona utakua ujinga huu, nikamwambia "Leo ndo mwisho, siji tena hapa".

Baada ya kuona nmekaza msimamo zaidi ya siku 2 siendi kwake. Usiku mmoja niko kwangu, akanipigia na kunambia mbona baba mtoto namjua na nafahamiana naye kabisa? Nikamwambia nitajie jina akalitaja.

Nikamwambia mimi simjui, akajaribu kunielezea ila sikumwelewa. Mke wangu alipotokea ikabidi kukatisha mazungumzo. Nikamwambia tutaendelea kesho. Kesho yake nimeenda kwake, kweli kanionyesha picha ya jamaa.

Kuangalia nikakuta ni jamaa ninayemfahamu kabisa. Nakumbuka alikua ni dreva wa gari za serikali ana mke wake na watoto wawili. Tena aliwahi kuwa mpangaji wangu zamani (sahivi yuko kwake kajenga) na ni mtu wa kabila langu na kila Jumapili ya mwanzo wa mwezi huwa nakutana naye sana kwenye vikao vya kikundi cha umoja wetu wa kikabila. Aisee nikapigwa na butwaa.

Ikabd kumdadisi zaidi walikutana vipi na jamaa mpaka wakazaa pamoja halafu wasiendelee na mahusiano yao, maana jamaa ninavyomjua ana mke tayari na watoto wawili.

Akanielezea kua kipindi hicho jamaa kapanga kwangu, walikua wapenzi alikua anakuja pale na anaondoka, siku moja moja analala pale na ndipo aliponifahamu Mimi kama mwenye nyumba wa bwana wake maana nilikua nakuja Sana kipind Cha ukarabati vyumba vingine vya pembeni nyumba ile.

Nikamwambia "Sikukumbuki kabisa, japo nakumbuka kuna mwanamke nilikua namuona anafua na kufanya usafi kwa jamaa ila sikutilia sana maanani hata sura siikumbuki".

Akanambia kuwa yeye alishanijua tu muda mrefu kuhusu jamaa, walikuja kugombana sana baada ya punde tu kumwambia kuwa ana ujauzito wake, wakawa hawaongei mpaka anajifungua na kwenda kujifungulia kwao. Sasa aliporudi kwa jamaa ili kumuonyesha mtoto wake, anafika pale ndiyo akamkuta mwanamke mwingine.

Alipomtafuta jamaa kwenye simu, jamaa akamwambia pale asikanyage, tena yeye alishaoa mda mrefu, huyo ni mkewe wa ndoa, kipindi hicho wana mahusiano ni nyege tu zilimsukuma wawe pamoja, mkewe alikua mkoani.

Akaona isiwe shari akarudi kwa mama yake na kuendelea kulea mtoto wake. Na ndipo mama yake akampeleka kujifunza ushonaji na mpaka sasa hivi ufundi cherehani ndiyo kazi yake inayomlisha yeye na mwanae.

Akasema siku moja moja jamaa huchangia matunzo ya mwanae na ile juzi alikwenda pale kumuona tu hakuna cha ziada walichofanya. Nikawa nimemuelewa, ila nikajipa nafasi kidogo ya kuyafanyia uchunguzi maneno yake nisije kulishwa matango pori.

Basi Jumapil ya tarehe 2 ndiyo ilikua siku ya kikundi chetu cha kikabila kukutana, na kwasababu bia na story za hapa na pale huwa zinakuepo baada ya vikao. Tulipobaki wanaume tu nikajaribu kuchomekea stori za Michepuko na kuzaa nje kazi yake ya sasa, nione jamaa atachangia vipi ili nijaribu kuunga doti.

Jamaa akawa ni msikilizaji tu huku akishangaa tunaoweza kuchepuka tunawezaje, akasema yeye hajawai kuzaa nje, mambo hayo huwa hawezi kabisa. Serikalini ana mwaka kaachishwa (sababu hakuzisema) sasa hivi anapiga deiwaka kwenye gari kusafirisha nje ya nchi (yaani IT).

Basi kichwan nikajua mengine ni kweli ila huyu mwanamke kuhusu kuzaaa naye kanidanganya. Huenda kweli waliwai kuwa na mahusiano tu, ila kuzaa anamficha wa ukweli aliyezaa nae. Basi nikamwambia "Wee umenidanganya, hujazaa na jamaa. Nimemdadisi sana jamaa hana mambo hayo. Kile kilikua kikao cha wanaume tu, na bia zilikua kichwan lazima tu angefunguka ukweli."

Akasema, "Wee kama huamini, kesho usiku ntamuita hapa. Wakati wa kuondoka jifiche gizani hapo barabarani kwenye kona ndani ya lile pagale utamuona vizuri jamaa anatokea huku kwangu". Nikasema "Sawa"

Kweli kesho yake kanitumia ujumbe kuwa jamaa kafika, nikaanza safari ya kwenda kwake. Nimefika barabarani alikonambia nimsubiri akitoka. Nikaona utakua ujinga huu. Nikaenda mpaka dirishan kwake nikamsikia jamaa yumo ndani anacheza na mwanae.

Ikanibidi nitege sound recorder juu ya vent ya dirisha kwa kutumia kisimu cha tochi. Kisha nikarudi barabarani kwenye pagale jirani kusubiri. Kweli haukupita muda jamaa akatoka, akafika pale kwenye pagale nilikojificha akasimama kwa muda akitizama huku na kule na kubonyeza simu, moyo ukanidunda labda jamaa kaniona.

Haukupita muda bodaboda ikafika, ikambeba, ikageuza na wakaondoka pale. Nikatoka mule kijasho chembamba kinanishuka nikaenda kwa mwanamke na kumwambia kweli ni yeye jamaa nimemuona.

Akataka tufanye mapenzi ila hata ule mzuka wa kufanya naye haukuepo, nikaaga, nikamwachia posho yake na kuondoka. Akafunga mlango akalala. Nilivyofika mbele nikarudi nyuma kuchukua kitochi changu nikasikilize zile voice recordings.

Nimefika kwenye gari nmetulia nimesikiliza vizuri zile recordings nikagundua hawakua na vitu serious walivyoongea mle ndani kuhusu mapenzi. Zaid zaid jamaa alileta midoli na nguo za mwanae na muda mwingi jamaa aliutumia kuongea na simu. Alipomaliza akaacha dawa ya kikohozi ya mwanae, akaaga na akaondoka.

Kiukweli wakuu tangu hapo nimebaki njia panda katika hili, nmekuwa mzito sana kwa huyu mwanamke. Sijui ni lipi sahihi nifanye, ni lipi siyo sahihi nisifanye maana nikiangalia vizur huyu mwanamke anaonyesha kunipenda, kunitii na kuniheshimu sana.

1. Kuna muda nafsi inanambia niendlee na haya mahusino, nafsi nyingine inanambia niyasitishe.

2. Vipi jamaa akija kujua natembea na huyu mzazi mwenzie, na japo hajanitambulisha ila kuna nafsi inanambia hatojiskia vizur?

3. Vipi suala la kuendelea kufanya naye mapenzi pale nyumban kwake? Japo mwanamke ananiaminisha niwe na amani na keshamwambia na jamaa anaelewa yuko kwenye mahusiano mengine ila binafsi nafsi inasita sana pale.

4. Huyu jamaa ni kabila langu, anamjua hadi MKE wangu na familia yangu. Nawaza vipi siku akijua namla mchepuko wake na vipi akienda nisemea kwa mke wangu?

Tushauriane hapa wakuu.
 
Back
Top Bottom