View attachment 2725754Wakikamilisha hii Barabara ya mkenda hadi msumbiji kiukweli itafungua Sana mikoa ya ruvuma na njombe maana gari nyingi za msumbiji
Malawi na south Africa zitapita hii road ni short cut kuliko ya tunduma na kazi ya ujenzi inaanza km 60 na hii imefanya makambako kuwa busy na ujenzi wa viwanda ndani ya mkoa wa njombe na bado mchuchuma na liganga mambo yanazidi kuwa♨️♨️♨️ 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇JE WAJUA SONGEA NDIYO BARABARA YA MKATO KWENDA AFRIKA YA KUSINI
Mkuu wa Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma Mheshimiwa Kapenjama Ndile Mji wa Songea ni njia ya mkato ya kwenda nchini Afrika ya Kusini hivyo kujengwa kwa barabara ya lami kutoka Songea hadi Mkenda mpakani na Msumbiji kunakwenda kuufungua Mkoa wa Ruvuma kimataifa
Mheshimiwa Ndile alikuwa anazungumza na wananchi wa Kata ya Mwengemshindo Manispaa ya Songea ambao wametoa hekari 5000 kwa ajili ya kujenga viwanda vya kisasa hivyo kuwezesha bidhaa zitakazozalishwa kwenye viwanda hivyo kuuzwa nchi za Malawi,Msumbiji na Afrika ya Kusini.
View attachment 2725752