Kahama VS Njombe/Mafinga

Kwa miji yenu ata mkipata tuvimiradi twa nyumba kama hizi lazima uringe, lakini huku tuipost nyumba kama zako unazopost itakuwa ni kujishushia heshima.
Excuses as usual,tukivipata kutoka wapi? Unadhani ni sawa na huko mnakotegemea Serikali?

Wapi Shinyanga na Musoma?
 
Excuses as usual,tukivipata kutoka wapi? Unadhani ni sawa na huko mnakotegemea Serikali?

Wapi Shinyanga na Musoma?
Acha kulinganidha mikoa ya wapambanaji na miko ya ajabu, kawaambie Dar na Dodoma hizo ndio mikoa inayotegemea miradi ya serikali mpaka kwenye makazi ya watu.
 
Labda hujauelewa ule Uzi vizuri.

Wenzetu huwa wanadai kwamba kila kitu kizuri ni chao sisi Tanzania hatuna kitu kizuri cha kuonyesha.

Ule Uzi ni wa evidences. Wao wanasema wanajua kupika na wanakula chakula kizuri kuliko sisi anaweka chakula chake, ukimbishia anakwambia onyesha chako tukione inabidi uweke.

Wanasema wanavaa vizuri na nguo za gharama kwasababu wana uchumi mzur na sisi Watanzania hatuwezi kumudu kuvaa hivyo. Tunawaptove wrong.

Wanasema wana wanawake wazuri eti sisi Watanzania wanawake wetu ni wabaya. Wewe binafsi unaamini hivyo? Tunatuma picha.

Kwahiyo wao wako kimkakati zaidi kuichafua Tanzania na sisi tunawakosoa kila angle ili kuonyesha watu kwamba Tanzania ni nchi nzuri na tuna vitu vizuri.

Elimu hivyo hivyo eti Watz hatujasoma huku wakiweka vyeti vyao vya mchongo lakini wanaumbuliwa. So siyo uzi wa kipuuzi kama unavyodai. Ukiacha uvumi wa uongo ukadumu muda mrefu baadaye ugeuka na kuwa ukweli.

Hapo sijazungumzia utalii,miundombinu,demokrasia n.k. Zingatia kwamba siyo sisi tu kwenye jukwaa ndio tunaufuatilia hata walioko nje wanaufuatilia pia.
 
Pamoja sana me nawakubali.
 
Bado sana, vijengo viwili unavimba asee una matatizo ambayo kwenye jukwaa hili hatuwezi kukusaidia. May be ni Moja ya sehemu yako ya starehe ndiyo maana watu wanakuacha upate burudani kadri akili yako itakavyo
 
Ni mwendo wa mabilioni tuu..
Moja ya Wilaya mbazo zitachangia sana GDP ya Mbeya na per Capita income ni Mbarali.πŸ‘‡
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…