Sisi tunakusanya fedha kila pande ya dunia ndani na nje wewe inafutahia wanaokuja kuchekua fedha na kwenda kula raha Paris.Kwangu lilomuhimu ni lile linarudisha pesa.Issue ya wasanii wa nje ni hasara kwa Taifa tu.Jiulize wanarekani wakati wa fiesta walikomba USD ngapi TZ na nchi ilipata nini?
Dah hizi akili zilizozoea show za Gigy money ni shida kwelikweli, kwa taarifa yako huyo msanii kuja tu kufanya shughuli hapa bongo tayari serikali inapiga pesa,
Pili, huyo msanii analetwa na kulipwa na kampuni binafsi kibiashara ili kukuza na kutangaza brand yao,
Tatu, katika tamasha kubwa la msanii mkubwa watu huwa wengi na hutumia bidhaa mbalimbali kwa kiwango cha juu sana, mfano bia hunywewa kwa kiasi kikubwa sana na hapo serikali inapiga pesa make kila chupa ya bia ina pesa ya serikali.
Nne, hawa wasanii huwa wanapost kwenye account zao za mitandao ya kijamii kuhusu shughuli zao mbalimbali, mfano Jay Z alipokuja bongo alipost kuhusu uzuri wa bongo, hata alipohojiwa na wanahabari wa huko kwao alizungumzia pia sifa nzuri za Tanzania, hivyo basi aliitangaza Tanzania na pengine Kuna watu walikuja TZ kupitia yeye.
Tano, wananchi kupata burudani, namaanisha burudani kama burudani yaani, sio hizo burudani zenu za huko kusini za akina Amber Lulu. Mtu kuburudika ni faida sio hasara, na ukizingatia watu wa huku tuna hela sio kama nyie huko na ndo maana hawaji huko.
Kwa hiyo hapo serikali kwa niaba ya nchi inapata, wafanyabiashara wanapata, msanii anapata, host anapata, Mwananchi anapata.