Kahama VS Njombe/Mafinga

Acha upimbi mkuu Njombe ilikidhi viwango vya kuwa TC toka 2005 na ndipo 2007 ikapewa hadhi rasmi.

Jiografia ndio ililazimika kuwa na Tarafa mbili afu ziliwekwa kimkakati Ili tunapokidhi viwango vya Manispaa tusilazimike kuomba Eneo au kuchukua maeneo ya Halmashauri zingine,kwa hiyo waliona akili.

Nyie endeleeni kujikusanya bado mnasafari ndefu Sana,wachuuzi wenzenu Kahama walibebwa na mapato na idadi ya watu sasa sijui hicho kijiji Maskini kitabebwa na nini maana watu wachache na pesa kiduchu.

Sikumbuki kama Njombe TC wakati inapewa hadhi ya Mji ilikuwa na mapato madogo kama ya Makambako,kama ndivyo kueni kwanza sio kupiga makelele baada ya kuota ndevu.
 
Usikalili viwanda vya kilimo tu viwanda ni chachu ya maendeleo eneo husika najua hili Jambo watu wa njombe linawatesa polen tutaendelea kuja kununua mashamba
Viwanda ambavyo vinatumia mitambo na teknolojia zaidi kuliko labour based sivikubali na hafuvihitaji kwa pale Njombe.

Sie tunataka viwanda vya kuongeza thamani ya Mazao yetu ya kilimo.Unakaribishwa Sana kununua mashamba kama muwekezaji utatuongezea pesa
 
Yana wewe ndo hujui ulisemalo hebu fatilia mapato ya 2017 uone mkoa wa njombe Nan alikuwa anaongoaza usijisifu na mapato ya miaka miwili mzee
 
Unajifariji
vumilia tuu nanyi mtafika..hapo awali ilikuwa maandalizi na mapendekezo vigezo vilikuwa bado.Kwa sasa tumekidhi vigezo baada ya sensa mwakani tutakuwa na population rasmi ya serikali ambapo minimum ni watu 150k

Taja wewe vigezo ambavyo unadhani hatujakidhi.. Changamoto ya barabara itatatuliwa na Tactic mwaka ujao yaani saizi wanakamilisha procedures za kiserikali tuu.
 
Makambako idadi ya watu ni kubwa tofauti na njombe wanao kaa vijijin hko hata growth rate makambako ni kubwa kuliko mashambani hko unavotoa point hebu jaribu hata kufatilia mwaka 2002 njombe ilikuwa na watu 40000 wakati makambako ikiwa na watu zaidi 50000 bado mapato makambako ikawa juu Sasa nani alibebwa Kama sio njombe na bado hadi saiz mnataka kubebwa hii itakuwa ndo manispaa ya Kwanza yenye wakaz asilimia 85 ni vijiji
 
Barabara changamoto , umeme changamoto eneo la kiutawa Wala asilimia 85 ni vijiji kitu ambacho makambako ni tofauti tena kubwa mno
 
Kumbuka tactic Kama unafatilia vizur mradi huu utatoa vipaumbele kwenye miji ambayo haikuwemo kwenye mradi wa mwanzo uwe unafatilia mzee happy mlisha jengewa stend , soko , na vibarabara
 
unfortunately hakuna mjinga anaeweza kwenda eti kutalii Makambako hayupo wote watakuja nchi ya ahadi Njombe.

Hiyo mandhari na jiografia ndio vinawaleta sasa.

Pia mwambie huyo Msukuma kwamba Njombe ni mkoa wa kimkakati kwa serikali kwa sababu zifuatazo

1.Uta host mabwawa 4 ya kuzalisha umeme ya Ruhudji,Rumakali,Ruhuhu

2.Utakuwa na migodi mikubwa ya Madini ya chuma na makaa ya mawe Liganga na mchuchuma.

3.Mkoa maalumu wa kufundishia teknolojia za Mazao ya chakula,biashara, mboga mboga na matunda baada ya Arusha ndio maana TARI na TAHA wameweka kambi.Soon tunaanza kulima maua.Hata PM alisema watajenga cold Room pale Songwe Airport maalum kwa bidhaa kutoka Njombe

4.Mkoa maalumu wa kuzalisha Mazao ya miti na bidhaa zake sanjali na wailaya za Mufindi na Kilolo.

5.Ni mkoa wenye nguvukazi ya wachapa kazi

Kwa kuzingatia hayo ndio maana serikali inafungua barabara pande zote zakutoka na kuingia Mkoa wa Njombe tena zinajengwa kwa asphalt na zege tofauti na mikoa mingine mizee.

Cha kukuongezea na wewe ni kwamba shughuli zote hizo zitakuwa centered mkoani yaani mjini Njombe.

Sasa mkoa/Mji kama huu huwezi linganisha na hivyo Vimiji uchwara vya wachuuzi kama Kahama, Makambako, Tunduma nk
 
Unaleta takwimu za historia zitakusaidia nini mkuu at current times.By 2012 Njombe TC kwa mujibu wa sensa ilikuwa na watu 130k sasa hizo takwimu za 2002 zitakusaidia nini wewe?
 
Na kati ya mji wa ovyo nyanda za juu kusini ni njombe eneo kubwa ni mapori huwezi linganisha na miji Kama makambako ambayo eneo kubwa ni makazi unavoingi mipakan ni makazi mwanzo mwisho ila sio njombe ukitoka kibena makazi mwisho nundu hadi ukaukute mpaka wa madaba ni full mapori na vijiji kitu ambacho kwa iringa , mbeya ,songea na tunduma hakipo Yan hiyo itakuwa manispaa ya mapori
 
Na kati ya mji wa ovyo nyanda za juu kusini ni njombe eneo kubwa ni mapori huwezi linganisha na miji Kama makambako ambayo eneo kubwa ni makazi unavoingi mipakan ni makazi mwanzo mwisho ila sio njombe ukitoka kibena makazi mwisho nundu hadi ukaukute mpaka wa madaba ni full mapori na vijiji kitu ambacho kwa iringa , mbeya ,songea na tunduma hakipo Yan hiyo itakuwa manispaa ya mapori
 
Kumbuka tactic Kama unafatilia vizur mradi huu utatoa vipaumbele kwenye miji ambayo haikuwemo kwenye mradi wa mwanzo uwe unafatilia mzee happy mlisha jengewa stend , soko , na vibarabara
Sasa wewe una shida sana mkuu,sasa Njombe ilikuwepo kwenye tactic au? Njombe ilikuwepo kwenye ULGSP na sio TACTIC.Sio tuu kufuatilia mimi ni miko kwenye utekelezaji wa huo mradi.Nenda kwenye tovuti ya Njombe TC ukaangalie hiyo taarifa ya DCC uone Meneja wa TARURA Njombe Mji kasemeje afu urudi kufuta post yako .Wewe ndio hufuatilii sio mimi.

Kwa vigezo vyovyote huwezi jenga barabara kwenye vimiji uchwara ukaacha makao makuu ya Mkoa,bora hata hivyo vi miji uchwara kama Makambako vingekuwa vinazalisha mapesa vingekuwa considered .Ni mwehu tuu ndio anaweza weka kipaombele sehemu ambayo haizalishi akaacha sehemu inayozalisha kama Njombe.
 
Huo huo mji wa hovyo ndio makao makuu ya Mkoa πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ na hayo hayo mapori ndio yanazalisha pesa ya kuzidi,lete point nyingine mkuu.

Miji yote yenye mapori inafanya vizuri sana kwanza ina hali ya hewa nzuri na iko liveable like Mbeya,Arusha,Njombe,Mafinga nk
 
Unaleta takwimu za historia zitakusaidia nini mkuu at current times.By 2012 Njombe TC kwa mujibu wa sensa ilikuwa na watu 130k sasa hizo takwimu za 2002 zitakusaidia nini wewe?
πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„Uelewe mnavyobebwa
 
Cool down uzur want hili Jambo wazir mkuu Alisha lieleza kuwa no wap wataanza na vipaumbele we ni mtekelezaji Kama wengine makao makuu uchwara Kama hayo waache kupambana na miji ya Pesa mzee πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„ na isitoshe makambako haikuwemo kwenye hiyo miradi ila kwa mkoa wa njombe ndo mji wenye barabara za lami km nyingi mkoa wa njombe
 
Barabara changamoto , umeme changamoto eneo la kiutawa Wala asilimia 85 ni vijiji kitu ambacho makambako ni tofauti tena kubwa mno
Changamoto za barabara zitamalizwa next yera via TACTIC,Umeme sio changamoto ya kushindwa kwa Halmashauri ni ishu ya TANESCO na Serikali haituhusu.

Eneo la mipaka kuwa na vijiji au vitongoji sio changamoto linakubalika kisheria na ndio linatumika kwa shughuli za uchumi na uzalishaji kuleta pesa mjini.

Wewe jua tuu before 2025 itakuwa Njombe TC,zile benefits za Manispaa tutaanza kuzipata kama kuongezewa bajeti ya maendeleo na utawala kwenye kila kitu mfano ruzuku ya serikali kuu kuwa 2bln,kupewa bajeti ya lami kila mwaka km 1 nk kwa hiyo tutazidi kuwatimulia vumbi.
 
Na uzuri wa mji wa makambako barabara za centre asilimia 90 wamemaliza saiz wanaanza za pembezoni na km 10 za lami tayar wamepata kinachofuata ni ujenzi tu
 
Hakuna hisani ya PM wala huruma mtapata

Miji ya pesa ndio iko kama hii
hapo chini ?
 
Na uzuri wa mji wa makambako barabara za centre asilimia 90 wamemaliza saiz wanaanza za pembezoni na km 10 za lami tayar wamepata kinachofuata ni ujenzi tu
Hako kamji kaduchu ukijenga km 3 umemaliza Mji wote huwezi linganisha na Njombe ambayo ina mtandao mkubwa wa barabara kuliko hicho kijiji.

Ndio maana hata bajeti ziko tofauti bajeti ya Tarura Njombe TC ni kubwa kuliko ya hicho kijiji chenu,got it
 
Safi πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ huo uloo wenu wa ku force mambo lazima mtandao wa barabara uwe mkubwa ko tegemea makambako kuwa kivingine zaidi ya Sasa maana ndo tunaanza lami pembezoni kwenye uwekezaji mkubwa wa makampuni maana umeme kila Kona upo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…