Kahama VS Njombe/Mafinga

Mbeya cc kwa Sasa imejaa jiografia imewabana Kuna haja mashamba ya KILIMO uyole wahamishe vipimishwe viwe VIWANJA

 
Hawa wababaishaji mbona fujian hexngwang wa maganga matitu kaenda haraka Sana na amelipa FIDIA mwenyewe hapo serikali inajichelewesha yenyewe
Amelipa fidia mwenyewe au ni Serikali imelipa?
 
MKUU WA MKOA WA NJOMBE AMEMPONGEZA MZEE MTEWELE KWA UWEKEZAJI WA HOSPITALI MPYA NJOMBE

NJOMBE MJINI – Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, ametembelea hospitali mpya ya Mtewele iliyopo katika eneo la Block X, Njombe Mjini, na kushuhudia uwekezaji mkubwa uliotekelezwa na Mzee Mtewele.

Katika mazungumzo na Mzee Mtewele, Mhe. Mtaka amempongeza kwa kuamua kuwekeza mradi mkubwa nyumbani Njombe, akibainisha kuwa kukamilika kwa hospitali hii kutawawezesha wananchi wa Mkoa wa Njombe na hata wale kutoka maeneo mengine kupata huduma bora za afya kwa urahisi. β€œHii ni hatua muhimu inayoongeza upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi na inaonyesha jitihada za kweli za maendeleo,” alisema Mhe. Mtaka.

Kwa upande wake, Mzee Mtewele alimshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kutembelea mradi wa ujenzi wa hospitali na kuonyesha ushirikiano katika kuhakikisha jitihada za kuboresha sekta ya afya zinathaminiwa na serikali pamoja na wananchi.

Hospitali ya Mtewele ni mradi mkubwa wa kimfumo unaoashiria maendeleo katika sekta ya afya, huku ikitoa matumaini makubwa kwa wananchi wa Njombe kupata huduma za matibabu za kisasa na kwa gharama nafuu.
 
Utekelezaji wa wazo lamkoa wa njombe kuwa na mji wa VIWANDA na BIASHARA wadau wameunga Sana mkono uwekezaji unapamba moto sector mbalimbali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…