Ni mwendo wa VIWANDA eneo hili igawa๐๐๐ MKUU WA WILAYA YA MBARALI APONGEZA UJENZI WA KIWANDA CHA PLASTIKI UNAOENDELEA MBARALI
Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mhe. Kanali Maulid Hassan Surumbu siku ya leo tarehe 03.06.2025 ameambatana na Maafisa Biashara na Viwanda pamoja na Afisa Mazingira wa Wialya ya Mbarali ametembelea Mradi mkubwa wa kiwanda cha Plastiki unaeondelea kijengwa katika kata ya Lugelele kijiji cha Igomelo kitongoji cha Nyanyanjo.
" Niwashukuru sana Uongozi wa kampuni ya RJ MUSA CONSTRUCTION kwa kubuni mradi huu na kuona inafaa kuuleta nyumbani"
" Mradi huu utaenda kupunguza changamoto ya Ajira kwa vijana wetu wa Mbarali, Mkoa wa Mbeya na hata nje ya Mkoa wa Mbeya" Aliongeza Kanali Maulid
"Wilaya ya Mbarali ina miradi zaidi ya 26 kwenye Sekta ya Maji na inahitaji mabomba mengi, nina imani mtawasaidia watakapohitaji"
" Uwepo wa kiwanda hiki Mkoa wa Mbeya, utaenda kupunguza gharama kubwa zinazotumika za kuagiza mabomba nje ya Nchi au Nje ya Mkoa na Miradi itakuwa inakamilika kwa wakati" Kanali Maulid
Kiwanda hicho cha Plastiki kinajengwa katika Kata ya Lugelele na kinatarajia kukamilika Mwezi Agosti, 2025.