CHUO KIKUU CHA DODOMA CHASAINI MKATABA WA UJENZI WA KAMPASI NJOMBE NA KAMPUNI YA DIMETOCLASA REALHOPE LTD
Viongozi mbalimbali wakiongozwa na Prof. Rwekaza Mukandala, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), wamefika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe kwa ajili ya kushuhudia tukio muhimu la utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa majengo ya Kampasi ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) mkoani Njombe.
Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi wa ngazi mbalimbali ambapo walipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka.
Katika tukio hilo, Chuo Kikuu cha Dodoma kimesaini rasmi mkataba wa ujenzi wa Kampasi ya UDOM Njombe na Kampuni ya Dimetoclasa Realhope Limited, ambayo ndiyo mkandarasi atakayetekeleza mradi huo mkubwa wa kitaifa. Picha ya tukio inaonesha wawakilishi wa UDOM na kampuni hiyo wakipeana mikono kwa furaha baada ya kutiwa saini mkataba, ikiwa ni ishara ya ushirikiano rasmi ulioanzishwa kwa lengo la kukuza elimu ya juu nchini. Mhe. Mtaka alieleza kuwa mradi huo utakuwa kichocheo cha ukuaji wa uchumi na maendeleo ya kijamii kwa wananchi wa Mkoa wa Njombe.