Barabara ya Geita kwenda Bukoli Kupitia Buyagu na Kamena mbona GGM wameitelekeza?

nizakale

JF-Expert Member
Oct 23, 2019
4,029
2,902
Hii barabara tajwa hapo juu ilijengwa na mgodi wa dhahabu wa GGM ili kurahisisha usafirishaji wa mizigo yao kuja Geita. Aidha, ilibadilika ikawa mkombozi wa wananchi hata kwa mabus ya kutoka Geita- Bukoli - Kahama Hadi Dar es Salaam.

Kwa masikitiko makubwa kwa sasa barabara hii imetelekezwa haipitiki na haifanyiwi tena ukarabati. Sijui uongozi wa juu wa mkoa wa Geita wana taarifa hii ? Na kama Wana taarifa wana mpango Gani juu ya ukarabati wa barabara hii ? Maana Kuna taarifa ambayo siyo rasmi kwamba kwa sasa GGM wanapitishia mizigo yao Kupitia barabara ya Geita- Bwanga- Runzewe ambayo ni ya lami ila ni ya kuzunguka sana unapokwemda Kahama na mikoa mingine !

Hivi wabunge wa Geita hasa Kanyasu na yule wa Busanda hawalioni tatizo hili ? Kwa nini wasiombe GGM wakaendelea kuifanyia matengenezo barabara hii pendwa ? Kwa kweli hali hii inakatisha tamaa sana kwamba mkoa wenye utajiri wa madini kama Geita miundo mbinu yake ni ya hovyo namna hii. Ukiachilia mbali tatizo hili Kuna Ule mpango wa kujenga barabara ya lami ya Geita- Bukoli - Kahama umekuwa wimbo Toka enzi za Mzee Kikwete Kila siku tunaambiwa upembuzi yakinifu unafanyika !

Huo upembuzi miaka 20 haujakamilika tu ? Baadaye tukaambiwa kipande Cha Kakola Kahama mgodi wa Barrick umetoa fedha kwa ajili ya ujenzi huo lakini mpaka leo kimya.

Je, kipande Cha Geita kwenda Kakola Kuna mpango upi ?
 
Mzee hii nchi ukifikiri sana unaweza kuishia kuwa Gaidi ni vile tu hatukupewe roho za kiarabu na hakika hii nchi ingekuwa imeshakatika Vipande vipande!

Ukipita barabara ya Geita Kahama kama wewe ni mkazi wa ukanda huo na uwe unajua mapato yanayochangia kwenye serikali kuu lazima uumie roho!

Huwa naitukana serikali kwa kila tusi nikipita hiyo barabara

Lakini hitimisho kabisa ni kwamba Geita haijawahi kuwa na Mbunge inawachumia tumbo pekee

Ukimtoa Joseph Musukuma Geita haina Mbunge kabisa!
 
Hayati si alikuwa wa Geita au?
 
Back
Top Bottom