Kagoda Agriculture Ltd: Another BOT scandal

I think that the newspaper article meant to refer to a shelf company rather than to a shell company. Whereas a shelf company is a registered company with no assets and no liabilities, a shell company is a nonentity (it does not exist; there is no such thing).

It is entirely possible that public funds have been stolen in this way every year, and perhaps many times each year. As Choveki correctly observes, you need collusion between fat cats in government and at the BoT for these kinds of astronomical embezzlements. Now we know why we are poor while our leaders are filthy rich! They have been stealing almost all our money!
 
DUHHHHHHHHHHHHHHHH mamaaaaaaaaaaaaaa...wakati wengine hata kigari huna wenzio wana magari na maduka kibao...wanakwenda DUBAI, UK, US kuchugua mizigo..kumbe jamaa wamechota pesa HARAMU...Ewe M/Mungu tuoneshe wezi na MAFISADI WAZIWAZI.._AMEEN....HUKUMU yao SIMPLE kufilisiwa wao na Familia zao na Marafiki zao wa KARIBU...
 
MKJJ nikipata..tutafaidi wa-tz wote...tuwe na fair play ktk kutafuta riziki...mambo ya short cut yanatuumiza watafuta HAKI
 
Mkjj Ukitaka Ujue Tz Imeoza, Ajiriwa Na Kampuni Au Shirika Lolote Tz, Then Uone, Kila Mmoja Anafikiria Kuiba Ili Apata Utajiri Wa Haraka...mtu Mwingine Hata Mfuko Ukauke...mwaka 2000 Nilikuwa Ktk Get Collection Pale Sabasaba..namna Watu Wanavyokwiba Utashangaa, Na Ukiwa Askari Kudhibiti Wengine Wanaweza Kukuua..mie Moyoni Nikafikiri Ikiwa Kazi Ya Siku 10 Ndio Hivi, Je Full Employement, Ukaanza Kuwawekea Ngumu Watu Wasiibe Si Watakuua...we Need A Lot 2b Done Kaka....putin Anasema..."the Situation Is Not Convincing And There Is No Sign Of Life"
 
Inawezekana vigogo wa serikalini hawahusiki lakini vigogo wa BOT ndio waliamua kuchukua chao mapema.Na upo uwezekano viongozi ndio walikula kwa kutumia kampuni sasa Balali yanamkuta kwa ewala yake ili aendelee kuwa governor.

Kubwa ambalo limenigusa mimi ni kwanini governor Balali hakutaka kushughulikia watu kama hawa.Na ndio hapa tunapokuwa na mashaka na watu kama akina Balali.
Accountability na responsibility haifanyi kazi.Governor yuko accountable kwa Bunge au kwa Rais.Hivyo kama ni kwa Rais Bunge halina namna.Governor awe accountable kwa Bunge na kwa Wananchi hasa inapotokea vitu kama hivi wanatakiwa watoe ufafanuzi kwanini hawakufanya hivi kwasababu hii.
Nawasilisha.
 
Dada Asha, apart from Noni there is one Liyumba who seem to be a person of interest. He had some significant role especially when there was vacancy in Deputy Governor's position (after the departure of Mbaye).
MKJJ, Chuma's wish is mine too, and hopefully many other Bongolanders.
 
How come nothing happens when the big boys steal? People in the minor league are punished by either the government or by mob justice when they are caught dipping their hands into anything. Those of us that have been around for a while know, on the other hand, that senior bureaucrats and politicians have been stealing us blind right from the time of Mwalimu.

What happened to the people that paid large sums of money for a fake ferry, siphoned off huge amounts of our money via ATC operations, etc, way back in the time of Mwalimu's Presidency? If your answer is nothing then you do not understand our system well. The correct answer is that they got promoted! We know them!

What kind of justice do Tanzanian mobs follow? Why do they lynch those that steal five hundred shillings and vote into office those that steal five hundred billion shillings? When will mob justice turn from the hunger-driven petty thief and deal with the well-fed thieves that cause the hunger?
 
Jamani, hivi tunajifanya hatujui kuwa Kuhusu hii Kampuni? Au hii kampuni ni tofauti na ile ya "Dr" Chrisant Majiyatanga Mzindakaya, Mbunge wa Kwela CCM?
 
Kampuni iliyochotewa bil. 40/= Benki Kuu haina ofisi popote !!

• ‘Iliyeyuka’ baada ya ufisadi huo

MWANDISHI WETU
Dar es Salaam


KAMPUNI binafsi iliyosajiliwa kwa anwani ya Dar es Salaam na kuchotewa shilingi bilioni 40/= baada ya muda mfupi haina ofisi mjini Dar es Salaam na anwani iliyoandikwa katika daftari la usajili ni ya udanganyifu.

Kampuni hiyo iitwayo Kagoda Agriculture Limited, ililipwa mabilioni hayo ya fedha za walipa kodi mwaka 2005. Pesa hizo zilikuwa katika Dola za Marekani milioni 30.8 ambazo thamani yake ni sawa na bilioni 40/=.

Uchunguzi wa THISDAY dada wa KULIKONI umebainisha kwamba anwani ilIyotajwa katika usajili wa kampuni hiyo - Kitalu namba 87 eneo la viwanda la Kipawa, Wilaya ya Temeke - ni ya uongo kwani hakuna kitalu kama hicho katika ramani kuu ya Jiji la Dar es Salaam.

Habari za uhakika za uchunguzi toka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, zinatuthibitishia kwamba hakuna kitalu kama hicho popote.

“Ninasikitika hatuna kitalu chenye namba hiyo kwenye orodha katikaa Ofisi ya Usajili wa Viwanja,” ofisa mwandamizi wa Wizara ya Ardhi alisema alipoombwa kusema kuhusu suala hilo.

Uchunguzi umethibitisha kwamba kampuni ya Kagoda haikuwahi kuwa na ofisi popote na kwamba hata Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) haikuwahi kupokea malipo yoyote ya kodi kutokana na malipo ya mabilioni ya biashara isiyoeleweka.

Cha ajabu zaidi katika usajili wa kampuni hiyo ni majina ya wanahisa waliosajili kampuni hiyo ambao hawafahamiki kabisa. Majina yao ni John Kyomuhendo (hisa 40) na Francis William (hisa 60), ambao wote wana anwani moja (S. L. P. 80154, Dar es Salaam) na kutajwa kama wakazi wa Dar es Salaam.

Vyanzo vya habari vya kuaminika vimesema Kyomuhendo anafanya kazi na kampuni moja ya ujenzi maeneo ya Kipawa na anadhaniwa kutumia jina la udanganyifu kuficha utambulisho wake halisi.

Taarifa katika rekodi za Serikali zinaonesha kwamba Francis William alisajili kampuni ya Kagoda Septemba 29, 2005, na kupewa cheti cha usajili namba 54040. Shahidi wake katika usajili ametajwa kwa jina la Benjamin Mwangonda ambaye ni mhasibu wa kampuni iitwayo Khatco Management Limited.

Majukumu ya kampuni yanatajwa kuwa ni: “Kufanya biashara ya kilimo na ukulima wa aina mbalimbali ya mazao ya kilimo kwa ajili ya chakula au biashara, ufugaji na maziwa. Pia itazalisha kuku, bata, bata-mzinga, kutengeneza jibini, na mbogamboga za majani kwa ajili na kuuza nje ya nchi.

Kagoda Agriculture Limited imesajiliwa pia kwa ajili ya “kuuza nyama, mayai, kuku, vyakula vya kuku, madawa ya kuku, na vifaa vya kufugia kuku; kuuza nje maua; na kujenga nyumba mashambani vyumba vya kupoozesha na barabara.”

Imebainika katika ukaguzi wa kihasibu kwamba kampuni hiyo ilichotewa mabilioni ya fedha zikiwa katika dola kutoka Benki Kuu ikiwa ni mtiririko wa ufisadi kabambe ndani ya Benki Kuu.

Maofisa kadhaa waandamizi wa Benki Kuu wanatuhumiwa kushiriki katika njama hizo za ufisadi.

Kwa mujibu wa taarifa za wakaguzi wa hesabu wa kampuni ya Deloitte & Touche mwaka jana, ufisadi huo ulifanyika kwa mbinu kabambe za kughushi nyaraka mbalimbali Benki Kuu ambayo ni muhimu zaidi katika Sekta ya Fedha na Uchumi hapa Tanzania.

Kama ilivyokwishaandikwa katika matoleo ya awali ya KULIKONI na dada yake THISDAY, Kagoda Agriculture Limited, ililipwa na Benki Kuu fedha hizo (dola 30,732,658.82) kutekeleza majukumu 12 ya miradi ambayo haifahamiki vizuri lakini inayohusu “wafadhili”, “wahisani” au “wakopeshaji” muhimu wa Serikali.

Kampuni ya Deloitte & Touche, ambayo hadi mwaka jana ilikuwa ndio mkaguzi wa ndani wa hesabu za Benki Kuu inasadikiwa kuingia mgogoro kuhusu madeni na malipo ya Benki Kuu katika akaunti namba 99915091 01.

Wakati wa ukaguzi wa hesabu za kihasibu katika kipindi kilichoishia mwaka Juni 30, 2006, akaunti hii ilikuwa na fedha kiasi bilioni 131.95/-.

Kwa kufuatilia maneno yaliyo katika nyaraka ya kurasa nne kutoka Deloitte & Touche kwenda kwa Gavana wa Benki Kuu, Dk. Daudi Ballali, yenye tarehe Septemba 04, 2006, kuna maelezo yanayoonesha kasoro katika malipo ya fedha kwa Kagoda Agriculture Limited kama ifuatavyo:

• Kuna makubaliano 12 ya majukumu ya kutekelezwa kati ya Septemba 10, 2005 na Novemba 05, 2005. Muda huo hapo juu ni mfupi mno kwa kulipa wadai 12 mbalimbali dunia nzima.

• Makubaliano yote yalitiwa saini mjini Dar es Salaam mbele ya ofisa mmoja aitwaye B.M. Sanze, ambaye ni wakili wa Mahakama Kuu.

• Makubaliano matano yalifikiwa kwa kutiwa saini Oktoba 19, 2005 wakati makubaliano manne yaliwekwa saini Oktoba 18, 2005. Hii inaonesha kwamba wadai wa nje walisafiri na kuwahi kuweka saini zao katika makubaliano hayo katika muda wa siku moja. Uchunguzi katika Idara za Uhamiaji unaweza kubainisha kama jambo hili liliwezekana lakini akili za kawaida zinakataa uwezekano huo.

• Kuna makubaliano mawili ya majukumu yaliyofikiwa kwa saini Oktoba 18 (2005) yakihusu kampuni mbili za Kijerumani (Lindeteves J Export BV na Hoechst) kuhusu malipo ya Euro 1,164,402.76. Hata hivyo tarakimu zilikosewa na Benki Kuu ilindika barua kwa Kagoda Agriculture Limited kuelezeka kwamba malipo yatathiminiwe kwa fedha ya Kijerumani - Deutsche Marks. Barua hiyo hiyo ilishauri kutolewa kwa kiasi cha 8,196,673,600.53/- kwa Kagoda Agriculture Limited. Hatimaye wadai (Kagoda) waliwasilisha makubaliano mapya ya majukumu yenye tarehe Novemba 03, 2005 – siku mbili tu baada yta kuarifiwa.

• Tumebaini sio kawaida na tuna mashaka makubwa kwamba wadai wa fedha wa nje wanaweza kufanya makosa ya kujichanganya hadi kusahau na kuweka saini katika makubaliano yenye aina ya fedha tofauti na wanazostahili kulipwa (Euro badala ya Deutsche Marks). Juu ya hapo inaonesha udhaifu mkubwa kwa Benki Kuu kushindwa kufanya uchunguzi baada ya kubaini kasoro katika suala hilo. Badala yake Benki Kuu hiyo hiyo ikaendelea na mchakato wa kutoa malipo makubwa kiasi cha bilioni 8.2/- kwa wadai (kampuni tata ya Kagoda). Pia inashangaza ni vipi wakurugenzi wa Kagoda waliweza kurudi ghafla nchini katika kipindi cha siku mbili tu na kushughulikia marekebisho ya ghafla ya makubaliano. Hapo napo panahitaji uchunguzi katika Idara ya Uhamiaji kubaini safari za maofisa hao zilivyofanikishwa sambamba na matukio yaliyopo.

• Makubaliano yote 12 ya majukumu yanaonekana kuwa na lugha na maneno ya aina moja katika wadai wote wa kigeni. Hili sio jambo la kawaida kwani kampuni zisiohusiana haziwezi kutumia lugha inayofanana katika nyaraka zake.

• Hakuna makubaliano yoyote ya majukumu hayo 12 yaliyo katika karatasi zenye nembo za kampuni husika, hakuna anwani za kampuni husika au wawakilishi wake.

• Makubaliano yote yametiwa saini kurasa ya mwisho na wawakilishi wa wadai 12 wa dunia nzima. Hili sio jambo la kawaida kwani nyaraka za kisheria huwa zinakuwa na sahihi kila kurasa.

• Mihuri ya moto (seal) katika nyaraka zote 12 inaonesha kwamba inafanana na ya Kagoda Agriculture Limited. Uchunguzi umethibitisha kwamba watengenezaji wa mihuri yote 12 wanaweza kuwa “msanii” mmoja katika mbinu za kughushi.

• Kampuni tatu: Fiat Veicoli Industriali (kampuni ya Kitaliano), Valmet (Kampuni ya Marekani), na Adriano Gardella S.P.A (Kampuni ya Kitaliano ) zina mihuri ya moto inayofanana kabisa licha ya mikataba kuonesha kwamba zinatofautiana.

• Makubaliano ya Valmet, ambayo ni kampuni ya Marekani ni dola 2,398,439.96 lakini mkataba umesainiwa na Patrick Kevin, ambaye wadhifa wake katika kampuni hiyo ni “mhasibu.” Hii inashangaza kwamba makubaliano muhimu na ya gharama kubwa namna hiyo yatafikiwa na “mhasibu” katika kampuni.

• Mkataba wa Daimler Benz AG umesainiwa na mkurugenzi aitwaye Christopher Williams. Cha ajabu saini inaonesha herufi W. Christopher.

• Kampuni kadhaa zilizotia mkataba zilikwisha fungwa au kufutwa kama kampuni katika orodha ya usajili wa kampuni tarehe za zinazooneshwa katika mikataba. Hiyo ni kwa mujibu wa uchunguzi wa kampuni ya Deloitte & Touche.

• Kwa mfano, Hoechst AG ilishabadilishwa kuwa Aventis mwaka 1999. Daimler Benz AG nayo ilishabadilishwa kuwa Daimler Chrysler AG mwaka 1998. Fiat Veicoli Industriali halikadhalika ilishabadilishwa kuwa Industrial Vehicle Corporation (IVECO) January Mosi, 1975. Vilevile Mirrlees Blackstone iligeuzwa jina kuwa MAN B&W Diesel Limited kutoka Machi 2002, wakati Valmet ilibalidishwa kuwa Metso Paper toka Mei 10, 2000. Sasa inashangaza kabisa majina ya zamani ya makampuni haya kutumika katika mikataba inayohusu mamilioni ya fedha mwaka 2005.

• Hakuna majina ya kampuni zilizopatikana katika majedwali zinazoitwa NS Boma na Lindeteves J. Export BV.

• Simu zilizopigwa katika ofisi za makampuni yaliyotajwa katika mkataba zimerudisha majibu kwamba hazifahami lolote kuhusu majina ya wawakilishi waliotia saini mikataba na Benki Kuu isiyoeleweka. Simu zimepigwa moja kwa moja Valmet (hivi sasa Metso Paper) nchini Marekani, Mirrlees Blackstone (hivi sasa Man B&W Diesel Limited) ya Uingereza na Daimler Benz AG (hivi sasa Daimler Chrysler) huko Marekani na majibu yakarudi kwamba wahusika wakuu hawajui lolote kuhusu mikataba na Benki Kuu ya Tanzania.

Barua kwa Gavana Ballali, kutoka kwa Samuel Sithole wa Deloitte & Touche nchini Afrika Kusini inasema wazi kwamba “matumizi ya majina ya zamani ya kampuni na kasi ya ufanikishaji wa makubaliano na mikataba inathibitisha wazi kuwepo kwa ufisadi uliohusu maofisa waandamizi wa Benki Kuu ya Tanzania.”

Kampuni ya Deloitte & Touche ilielezea pia mashaka yake kuhusu jinsi kampuni ya Kagoda, ilivyoundwa Septemba 29, 2005, na kuweza kulipwa “dola milioni 30.8 katika kipindi cha wiki tano hadi sita tu ya kuundwa kwake.”

“Hatuna taarifa zozote kuhusu uchunguzi wowote uliofanywa na Benki kuu kuhusu kampuni hiyo. Ni vigumu pia kukubali kuwa kampuni hizo ziliweza kuingia mkataba wa malipo ya dola milioni 30 na wadai mbalimbali nchini Ujerumani, Italia, Yugoslavia, Uingereza, Ufaransa, Marekani na Japan kwa kipindi kifupi,” inasema sehemu ya waraka huo.

Wakaguzi hao wa hesabu walimshauri Dk. Ballali kufanya ukaguzi wa haraka na wa kina na kusimamisha ajira za maofisa kadhaa wakati wa uchunguzi kuepuka kuharibiwa ushahidi wa nyaraka katika mafaili muhimu.

Hata hivyo hadi leo hakuna ofisa wa Benki Kuu aliyesimamishwa ajira yake hadi sasa kuhusiana na suala hilo. Hivi sasa kampuni mpya ya Massawe Ernst & Young, imepewa zabuni kukagua upya hesabu za kihasibu ndani ya Benki Kuu kwa mwaka 2005/06.

Hata hivyo taarifa za uchunguzi mpya bado ni siri ya Serikali licha ya taarifa za wazi kwamba umekamilika.
 
JAmani, hivi tunajifanya hatujui kuwa Kuhusu hii Kampuni? Au hii kampuni ni tofauti na ile ya "Dr" Chrisant Majiyatanga Mzindakaya, Mbunge wa Kwela CCM?

Hii Kagoda sio ya fisadi Mzindakaya; ni ya mfalme wa mafisadi- Rostam Aziz. Jamani mpaka leo hamjanieleza naweza kumpataje nimshike kwenye ule ufisadi mwingine.

Asha
 
Hii Kagoda sio ya fisadi Mzindakaya; ni ya mfalme wa mafisadi- Rostam Aziz. Jamani mpaka leo hamjanieleza naweza kumpataje nimshike kwenye ule ufisadi mwingine.

Asha
Asha
Heri ya mwaka mpya,2008 anza kufikiri positive na stop dealing with Gossips,unauthibitisho gani kua owner wa KAGODA ni Rostam Aziz,nachojifunza most of ur contributions hapa JF ni based na Gossips,Njo na Facts so that wote tuweze kujua unachdai.

Nachosikitika today bado kuna watu watu wanaongea bila facts na kutaka tuamini mawazo yao.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
 
Asha
Heri ya mwaka mpya,2008 anza kufikiri positive na stop dealing with Gossips,unauthibitisho gani kua owner wa KAGODA ni Rostam Aziz,nachojifunza most of ur contributions hapa JF ni based na Gossips,Njo na Facts so that wote tuweze kujua unachdai.

Nachosikitika today bado kuna watu watu wanaongea bila facts na kutaka tuamini mawazo yao.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

With all due respects,naomba unisaidie, utajuaje facts kwenye world-wide-web? Ukizingatia huu ni wakati wa Photoshop etc?
 
With all due respects,naomba unisaidie, utajuaje facts kwenye world-wide-web? Ukizingatia huu ni wakati wa Photoshop etc?
Fundi Mchundo

Ingekua kweli kua huwezi kujua facts then we can not make decission duniani,Facts zinapatikana thats why tuna fanya maamuzi,what i meant hapa uanposema kampuni X owner ni Y then unatueleza kua una uthibitisho through BRELA kama kulikoni ilichofanya wame enda extra mile kutafuta Directors n.k sasa nachojiuliza why mtu anakuja na just habari za Redio Mbao and anataka tuamini and all of us tujadili Gossips,i belive its time JF we should not incourage these ideas angalia hoja ya asha anataka tumsaidie aweze kumfikia Rostam toa Advert ktk magazeti.
 
Fundi Mchundo

Ingekua kweli kua huwezi kujua facts then we can not make decission duniani,Facts zinapatikana thats why tuna fanya maamuzi,what i meant hapa uanposema kampuni X owner ni Y then unatueleza kua una uthibitisho through BRELA kama kulikoni ilichofanya wame enda extra mile kutafuta Directors n.k sasa nachojiuliza why mtu anakuja na just habari za Redio Mbao and anataka tuamini and all of us tujadili Gossips,i belive its time JF we should not incourage these ideas angalia hoja ya asha anataka tumsaidie aweze kumfikia Rostam toa Advert ktk magazeti.

Hatufanyi maamuzi based kwenye yanayojiri kwenye www. Mimi ninavyoona hapa ni mahali ambapo KILA kitu kinaweza kujadiliwa na FACTS zinathibitishwa nje ya hizi fora. Hapa ni catalyst, ni changamoto na ni kwa anayetembelea kuamua kuamini linalojadiliwa au la. Sasa kama dada Asha anataka kumfuatilia Rostam, si mwache afanye hivyo?

Kama ni gossips na inuendos zinazomsukuma naamini Bw. Rostam anauwezo kabisa wa kuhimili mashambulizi na kuweka wazi ukweli ulipo. Ni kwa kubadilishana mawazo bila kujali kama ni pumba, gossips n.k. ndiyo ukweli unaweza kupatikana. Kila mtu ana access na hapa mahali na anapoona ukweli unapindwa hakuna anayemzuia kukanusha.

Si heri wanayazungumza hapa na si kwenye klabu za pombe, beauty salons etc. ambapo mara nyingi watu wanachukua kama gospel truth bila hata kudai authentication? Hapa, at least, unapingwa ukionekana umepotoka na ishu inaangaliwa from all angles. Ni haki ya Asha kufanya alivyofanya kama vile ilivyo haki yako kumchallenge. Ndivyo inavyotakiwa.
 
Nimeshaongelea Bank kuu ya Tanzania kutokuwa independent kunaicost nchi. Bank kuu nyingi duniani zimeanza kujitoa kutoka serikalini na kuwa vyombo vya kujitegemea huku serikali ikiwa kama msimamizi. Utaona Japan Central Bank, European Union Central bank and many other successful central banks are intependent.

Bank kuu ya Tanzania ni branch ya serikali, so inakuwa na new maamuzi kila panapofanyika new election au kubadilishwa kwa cabinent ya mawaziri. Economic goals most of the time are long time goals, sasa kama kila miaka miwili mitatu wanakuja watu wapya ambao wana influance katika bank kuu then wanachange all strategy kutokana na their own personal desires, then we are not going to build strong economy.

Bank kuu ya Tanzania nadhani inakazi nyingi sana kwa sababu ni branch ya serikali. Kama bank kuu inatapewa uhuru wake, then bank kuu ita deal na main three things zenye direct influance to economy. To control reserv requirement of all financial institutions, to control interest rate and lastly, to provide Discound rate (lending of last resort). This are three main things which have direct effect to money supply. Hizi ni kazi tatu zenye effect katika money supply, kazi zingine kama kuchapisha pesa, kuaccept checks na n.k zitaendelea kuwepo.

Sasa baada ya Bank kuu kuwa independ hatutaona tena bank kuu inatoa latter of credits, sababu hiyo ni kazi ya bank za kawaida, hatutaona bank kuu imeusishwa na bajeti sababu hiyo ni kazi ya wizara ya fedha, hatutasikia bank kuu imewakopesha sijui Richmond sababu hiyo ni kazi ya wizara ya fedha kupitia Adhina au kupitia banks.

Kumbuka kwamba mwanasiasa yoyote lengo lake ni kushinda uchagizi unafuata. So, mwanasiasa anafocus short plan na sio long plan, kumuachia mwana siasa huyo kuwa na maamuzi makuu ya kichumi peke yake ni wenda wazimu. Federal Bank of US learn this since 1913, Bank of Japan learn this after 1998 big economic slap, Bank Europre knows about this, the only bank which doesnt understand ni bank kuu, ambayo ipo pale kuwalinda vigogo na sio kuchanyata uchumi wa Tanzania kwa watanzania.
 
Mtanzania.. point nzuri sana.. tatizo Benki Kuu ikiondolewa serikalini huoni kama tutakuwa tumekata mrija mkubwa wa sisi kunyonywa? sasa unafikiri watawala watanyanyonya wapi?
 
Back
Top Bottom