Kagera: Mlipuko wa bomu Wilayani Ngara waua Wanafunzi 05, zaidi ya 45 wamejeruhiwa

Taarifa kamili tafadhali. Roho za marehemu zipate rehema kwa Mungu zipumzike kwa amani amina.
 
Poleni sana wafiwa wote na majeruhi Mwenyenzi Mungu awape Nguvu na faraja katika kipindi hiki kigumu
 
Takribani wanafunzi 3 wameripotiwa kufariki dunia mpaka sasa na wengine kadhaa kujeruhiwa kufuatia mlipuko wa bomu wilayani Ngara.

Diwani wa Kata ya Kibogora wilayani humo, Ndg Adronizi Burindoli ameeleza kuwa jitihada za kuokoa uhai wa majeruhi zinaendelea..

Taarifa zaidi zitafuata...

Darasani, njiani, shambani, uwanajani au kulikuwa na mkutano?
 
Kibogora ni eneo lililo mpakani kabisa mwa Burundi upande wa wilaya ya Ngozi. Hapa warundi huwa wanafanya kufuru ya kuzurura na silaha zao hatari sana.
 
Back
Top Bottom