Kagera: Mlipuko wa bomu Wilayani Ngara waua Wanafunzi 05, zaidi ya 45 wamejeruhiwa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,496
9,278
Takribani wanafunzi 3 wameripotiwa kufariki dunia mpaka sasa na wengine kadhaa kujeruhiwa kufuatia mlipuko wa bomu wilayani Ngara.

Diwani wa Kata ya Kibogora wilayani humo, Ndg Adronizi Burindoli ameeleza kuwa jitihada za kuokoa uhai wa majeruhi zinaendelea..

Taarifa zaidi zitafuata...

Mwendelezo:

========



=> Wanafunzi sita wa shule ya msingi Kihinga mkoani Kagera Kaskazini Magharibi mwa Tanzania wamefariki dunia na wengine zaidi ya 25 wamejeruhiwa baada ya kulipukiwa na bomu wakicheza.

Kamanda wa polisi wa mkoa, Augustine Orom huo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na tayari wananchi wamejitokeza kuchangia damu kwa ajili ya kuwasaidia majeruhi.

Kwa mujibu wa Dokta Mariagoreth Fredrick ambaye ni mganga mkuu hosipitali ya Rulenge, amethibitisha kupokea miili hiyo na majeruhi ambao baadhi wako katika hali mbaya na tayari wanapatiwa matibabu.

"Tulionao hali ya sio nzuri. Wengine wameumia matumbo, wengine wamechanika bandama, wengine wamevunjika miguu, wengine vichwa vimepata majeraha, wengine wameumia macho." Dokta Mariagoreth ameiambia BBC.

Inaelezwa kwamba kabla ya kulipukiwa na kifaa hicho kinachoarifiwa kuwa ni bomu, wanafunzi hao walikuwa wanakichezea.

=> Mganga wa Hospitali ya Rulenge wilayani Ngara, Kagera Sister Mariagoreth Fransis amesema wamepokea majeruhi 45 waliotokana na mlipuko unaodhaniwa kuwa ni bomu. Kati ya majeruhi hao, 13 wamejeruhiwa vibaya na wawili wamefariki

ngara1.jpg
Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya msingi Kihinga,iliyopo wilayani Ngara mkoani Kagera walionusurika wakiwa Hospitali ya misheni Rulenge wilayani humo.
ngara2.jpg
ngara3.jpg
ngara4.jpg
Madaktari wa Hospitali ya Mission Rulenge wakiendelea na Matibabu kwa Majeruhi.

Kamanga wa Jeshi la Polosi mkoani Kagera Agustino Olomi amesema chanzo cha wanafunzi hao kujeruhiwa kwa bomu ni zoezi la kuuza vyuma chakavu ambapo mwanafunzi aliliokota na kuja nalo shuleni ili alipeleke kwa mnunuzi na kupewa madaftari.

Hata hivyo Kamanda wa Kikosi cha Kulinda mipaka cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ wilaya ya Ngara ,Meja TR Mutaguzwa amesema Bomu hilo lilikuwa na vipande 36 na lingelipukia ndani ya darasa wangeleta athari zaidi .

=> Kamanda Ollomi amesema kwamba wanafunzi waliopoteza maisha ni:

1. Julian Tarasisi (13)

2. Evart Theonas (12)

3. Edson Bigilimana (12),

4. Miburo Gabriel (12),

5. Tumsifu Ruvugo (8).

Wote wavulana wa Shule ya Msingi Kihinga.


=> Ngara.

Kamanda wa Polisi mkoani Kagera Agustino Ollomi amewataja majina wanafunzi ambao wamefariki dunia kutokana na bomu la kutupwa kwa mkono katika shule ya msingi Kihinga wilaya ya Ngara mkoani Kagera.

Kamanda Ollomi amesema kwamba wanafunzi hao ni Juliana Tarasisi (13) Evart Theonas (12) Edson Bigilimana (12), Miburo Gabriel (12), na Tumsifu Ruvugo (8).

Pia Kamanda huyo amesema mtoto wa sita aliyedhani amefariki alibainika kuwa bado yuko hai na yuko mahututi kwenye chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU).

Amesema mwalimu wa darasa, Policalipo Clemency aliyekuwa darasani wakati wa tukio ni miongoni mwa waliojeruhiwa na kulazwa hospitali.

Akizungumzia tukio hilo, Mwalimu Clemency amesema wakati bomu linaipuka, alikuwa akiandika mtihani wa kusoma ubaoni na kila mwanafunzi alikuwa akiingia na kusoma ili kumwekea alama kwa ajili ya mitihani ya kufunga mwaka.

“Ghafla nilisikia kishindo kikubwa na kuona baadhi ya wanafunzi wakianguka, walipoteza fahamu na wengine kutokwa damu,” amesema Clemency

Mmoja wa wazazi aliyepoteza mtoto katika tukio hilo, Bigimana Kaloli amesema baada ya kusikia kishindo alikimbilia shuleni na kusikia mtoto wake anayeitwa Edson akiwa tayari amefariki na kusema jambo hilo limeipa familia yake simanzi kubwa.

Chanzo: Mwananchi
 
Takribani wanafunzi 3 wameripotiwa kufariki dunia mpaka sasa na wengine kadhaa kujeruhiwa kufuatia mlipuko wa bomu wilayani Ngara.

Diwani wa Kata ya Kibogora wilayani humo, Ndg Adronizi Burindoli ameeleza kuwa jitihada za kuokoa uhai wa majeruhi zinaendelea..

Taarifa zaidi zitafuata...
Wishes to Meet Miss Zomboko.....@ miss Zomboko unaleta taarifa ngumu ngumu na za uhakika
 
Tuzidisheni maombi

Kutakuwa kuna sehemu tunakosea na mungu anaamua kutuadhibu
 
Takribani wanafunzi 3 wameripotiwa kufariki dunia mpaka sasa na wengine kadhaa kujeruhiwa kufuatia mlipuko wa bomu wilayani Ngara.

Diwani wa Kata ya Kibogora wilayani humo, Ndg Adronizi Burindoli ameeleza kuwa jitihada za kuokoa uhai wa majeruhi zinaendelea..

Taarifa zaidi zitafuata...
kwani mkuu yuko wapi?
 
Back
Top Bottom