Wanafunzi 9 wa shule ya msingi Kihinga mkoani Kagera kusini magharibi mwa Tanzania wamefariki dunia na wengine zaidi ya 25 wamejeruhiwa baada ya kulipukiwa na bomu.
Kamanda wa polisi wa mkoa, Augustine Orom huo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na tayari wananchi wamejitokeza kuchangia damu kwa ajili ya kuwasaidia majeruhi.
Kwa mujibu wa Dokta Mariagoreth Fredrick ambaye ni mganga mkuu hosipitali ya Rurenge, amethibitisha kupokea miili hiyo na majeruhi ambao baadhi wako katika hali mbaya na tayari wanapatiwa matibabu.
"Tulionao hali ya sio nzuri. Wengine wameumia matumbo, wengine wamechanika bandama, wengine wamevunjika miguu, wengine vichwa vimepata maijraha, wengine wameumia macho." Dokta Mariagoreth ameiambia BBC.
Inaelezwa kwamba kabla ya kulipukiwa na kifaa hicho kinachoarifiwa kuwa ni bomu, wanafunzi hao walikuwa wanakichezea.
Wadau,
Habari Kutoka Mkoani Kagera Zinaeleza Kuwa Wanafunzi Watano Wa Shule Ya Msingi Kihinga Wamefariki Na Wengine 18 Kujeruhiwa Baada Ya Kulipukiwa Na Bomu Mapema Leo.Shule Hiyo Ipo Mkoani Kagera Wilayani Ngara Na Wahanga Hao Walikuwa Wakikichezea Kifaa Hicho Kabla Ya Kulipukiwa.
Chanzo: Gazeti Mwananchi
Kwa Mujibu Wa BBC Waliofariki Hadi Sasa Ni 6 Wakati Waliojeruhiwa Ni Zaidi Ya 25.
Zoezi La Uchangiaji Damu Linaendelea Kuwasaidia Manusura Wa Mlipuko Huo.
Karibuni
So far walofariki wamefikia 6 na like 40 ni majeruhi na wengine hali zao siyo nzuri. Baadhi ya Wanafunzi wa shule za RHEC, St Alfred Rulenge na St Joseph Mbuba wamejitolea damu ktika hosp. ya Kristo Mfalme Rulenge.
Chanzo inasadikiwa kuwa ni bomu la mkono lililookotwa na mwanafunzi ktk shule ya Msingi Kihinga (mpakani mwa Tz na Burundi) kutoka kwenye sehemu ya kukusanyia vyuma chakavu!
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.