Kagame tells Kikwete "I will hit you......"

Status
Not open for further replies.
RUTAJUMBUKIRWA, simplemind,

..mbona Kabila anazungumza na M23 ambayo baadhi ya makamanda wanatuhuma za mauaji dhidi ya wananchi wa DRC?

..hata hivyo Kagame hajashauriwa azungumze na FDLR walioshiriki genocide, ameshauriwa azungumze na wale ambao hawana tuhuma za mauaji.

..
 
Last edited by a moderator:
Nakusupport,now its not a time to start confrontation with our enemies.remember vita ya uganda tulishinda kwa sababu wananchi wa uganda walikuwa wanafichua maficho ya jeshi lao.
Pia inaweza ikawa njia kwa wasioitakia mema nchi kupata mwanya.remember vita huanzishwa mezani na kumalizikia mezani but waathirika ni wananchi mnaoshabikia sa hv na ndugu zetu tutaowapoteza vitani.
I urge to tanzanian government not to sit down and find the peaceful solution for this conflict.
Dah, mbona hueleweki sasa, msimamo wako ni upi? Mimi nafikiri simplemind yupo sawa kwamba wananchi hivi sasa wamepoteza imani na majeshi yetu. Badala ya majeshi kuendelea kuwa rafiki wa watu, ndiyo hayo yanatumika hivi sasa kupiga na kuumza watu huko Mtwara na hata Arusha. Hivi ikianza vita, wananchi hawatawaunga mkono maadui kama walivyofanya waganda wakati wa vita na Tanzania? Mimi naunga mkono wazo la kwamba huu si wakati muafaka kufikiria vita. Maana huo uzalendo tunaotaka wananchi waonyeshe ndiyo huo unadhulumiwa na serikali. Kwa hakika usitegemee wananchi wa Arusha wanaopigwa mabomu na polisi watakuwa upande wa polisi. Definitely watawasupport maadui. Lets not even dream about war kwa sasa.
 
i think kuna hidden mater ambayo haijawekwa wazi between the two. JK kuongelea peace making ndio hasira zote hizo, Kagame tuliza hasira utakufa siku si zako, wewe nunaaaaaaaaaaaaa, ongeaaaaaaaaaaaaaaa, JK atakuchekea tu na mwisho wa siku utapasuka. tuache na raisi wetu tumemzoea wenyewe.
 
Kwani tatizo ni nini hapa? Sipendi uongozi wa Jakaya kwa vipindi vyote akiwa madarakani kama Rais wa Tanzania. lakini, kutukanwa na kanchi kadogo kama Rwanda is disgusting!! Kisa Jakaya ametaka peace talks and negotiations kwa nchi zile zilizo katika vita ndani ya maziwa makuu.

Jeuri ya kagame ya kupigana vita vya mstuni, anataka kutuletea sie? Hii haikubaliki hata kidogo...

uko sahihi mkuu,yaani mi nashangaa JK anasubiri nini maana wakati jeshi liko likizo kwa miaka mingi sana mpaka wanapewa kazi ya kulinda mikutano ya vyama vya siasa.
Amesahau ile kauli a mchonga meno kwa nduli?
 
Nimesoma wadau....imenisikitisha sana. kwani kagame ni nani mpaka atutishe hivyo na wembamba wake!
 
Kwani nani anajua mkutano wao kule Uganda? Hawa jamaa wameona uchumi unaweza kuanza kuibuka kwetu na wao wanategemea sisi kama soko kwa hiyo wamekubaliana si ajabu Kagame alianzishe halafu M-7, na Kenyatta wamuunge mkono na hiyo ndo itakuwa M23 ya kweli. Ukiweka na wenzetu wa zenji kujitoa katika muungano, nakwambia hiyo gas ya Mtwara itaisha tukiwa bado tunapambana na M23 hao. Usidhani ni wajinga wanajua kuwa wana-support ya ndani ya majeshi yetu maana kama Kinana kesha kuwa mkuu wake kama waziri unatarajia nini wengine. Uh mi pananiogopesha labda ndo maana tumeanza mapema JKT ili tupeleke baits kabla ya kujua nguvu ya adui.

My take: Kagame has no right to insult our president because of his advise on how to deal with internal conflicts in Rwanda. He has the right to choose the advise or deny it full stop. In my view that is the line you should not cross if you are mentally okey, otherwise 'an idiot'! JK never forced Kagame to negotiate, he gave an alternative method to deal with Rwandan Problem and JK is not the President of Rwanda so cannot decide for the Rwandans. It is Kagame and fellow Rwandans who can draw their roadmap toward PEACE.

Hasira zote najua ni kwa sababu ya Tz kupeleka majeshi kule kuangalia nini kinafanyika mpakani mwa Rwanda na DRC...na huu ndo ulikuwa ulaji wao wa kusafirisha maiti kumbe ni jeneza la dhahabu...kisha kuuze na kujenga Kigali. Huu nao pia ni Ubeberu wa weusi kwa weusi. Mi sioni kwa nini M7 na Bwana Kagame wanakuwa wakaribu kwa Marekani kuliko DRC!!! Jihadhari nawe Uhuru Kenyatta utajatuletea ya Charles Njonjo na EAC mwaka 1977! Eti hata damu yake ukichanja ilikuwa ni ya kiingereza...nyambafu mkubwa huyo...na hawa jamaa nao wanataka kuturudisha huko.
 
.....nachoweza sema hapa ni kuwa ushindi kwenye medani za kijeshi, hautegemei ukubwa wa nchi (eneo la mraba) bali ni zana bora za kisasa, uzalendo, na dhamira ya dhati ktk mapambano.....sina hakika na nguvu/uwezo wa Rwanda/Kagame, lakini pia ninashaka kama uwezo wetu ni uleule wa 1979/80 kwani vita haina macho na siku zote huwa haina droo/sare na "udogo wa ndimu mchuzi waungwaa".
 
Suala ni kuwa makini sana huyu mtu kama kakomaa kusemasema hivi jua kuna something behind him kinachomfanya arudierudie kauri zake,na anapoona rais wetu kimya anajua anamwogopa
 
Kagame kuua maadui zake wa interhamwe ambao wamechukua silaha wanapigana nae ni kitu gani kwako? mbona raisi wako yeye anaua wapinzani wake wa kisiasa ambao hata kisu hawajawahi kumshikia??!!!

yani ukiwa mtoto wa nje ya ndoa ni tatizo kubwa sana pole .
 
Rwanda kwa eneo lake ni ndogo kuliko mkoa wa Kilimanjaro ambao ni mdogo kuliko mikoa yote Tanzania. Tutamkanyaga kama kifaranga cha kuku akithubutu! Asidhani kuwa Tanzania ni kama Congo!

Mkuu; Tafadhali usifikirie kitoto,fikiria kiutu uzima.
Kuwa na eneo kubwa au kuwa na jeshi kubwa siyo kipomo cha kushinda vita.
kupigana na nchi ndogo si kipimo cha kushinda vita.Mharau mwiba mguu huota tende!!!!!!!
 
Hili liwe fundisho JK usiwe unaandikiwa kila kitu, wewe huwa unasema akili ya kwaambiwa changanya na yako. we kila unachoambiwa na kuandikiwa unakubali tu, Hongera sana Kagame.
NYIE WATUSTI MNA SHIDA GANI NA TANZANIA? alichowashauri Mh Kikwete kama hamkitaki sio lazima mkifuate. Haya maneno yote ni yanini? Anyway, you are known as HUMAN BLOOD THIRSTY PEOPLE, then go ahead killing innocent people in DRC; but be informed that, GOD will repay you in HIS due time!
 
akili yako inatosha kwenye kifuniko cha soda tu wala huyajui mambo mengi ya vyombo vyetu vya dola unaongea bila hata ya fact na ukiona mtu anaizalau mpaka nchi yake anachuki binafsi na watu walioko madarakani wala huna lolote.
wee nawe una matatizo sana, sasa wewe unajivuna una jeshi ambalo unalitumia kudhibitia wamachinga na wananchi wa Mtwara. Jamani lets be sincere, hata kama tuna uwezo mkubwa wa vita, huu si wakati wa hata kuifikiria tu ukizingatia hali yetu ya kiuchumi ilivyo mbaya. Tanzania ni nchi ambayo bado ina utegemezi mkubwa sana kifedha kuliko majirani zetu wa Afrika mashariki, na mbaya zaidi mahusiano kati ya jeshi na wananchi si mazuri, hiyo vita itatugharimu. Hebu tuende taratibu, kufikiria vita hivi sasa, ni kuisaliti nchi.
 
Watanzania gani hao? Maana Watanzania wako wengi tofauti tofauti, wengine wanamuunga mkono Kagame.

Sasa hiyo generalization ya "Watanzania this" "Watanzania that" ndiyo inaweza kuwa ku simplify hii habari kuwa unazi kama wa Simba na Yanga kuliko kingine chochote.
 
Asante kwa kunikosoa ni makosa ya kiuandishi tu.
But msimamo ni kwamba,vita sio suluhisho bali ni kuongeza matatizo,tutatumia pesa nyingi,tutapoteza ndugu zetu tunaowapenda na kuwategemea,na hali ya uchumi itadorora zaidi.

Dah, mbona hueleweki sasa, msimamo wako ni upi? Mimi nafikiri simplemind yupo sawa kwamba wananchi hivi sasa wamepoteza imani na majeshi yetu. Badala ya majeshi kuendelea kuwa rafiki wa watu, ndiyo hayo yanatumika hivi sasa kupiga na kuumza watu huko Malawi, hivi ikianza vita, wananchi hawatawaunga mkono maadui kama walivyofanya waganda wakati wa vita na Tanzania? Mimi naunga mkono wazo la kwamba huu si wakati muafaka kufikiria vita. Maana huo uzalendo tunaotaka wananchi waonyeshe ndiyo huo unadhulumiwa na serikali. Kwa hakika usitegemee wananchi wa Arusha wanaopigwa mabomu na polisi watakuwa upande wa polisi. Definitely watawasupport maadui. Lets not even dream about war kwa sasa.
 
ebu tusimchafue rais wetu kwasababu ya upuuzi wa kagame,huyu ni mfia maji,anajitapatapa..how can kagame hit jakaya
 
Johnsecond,

..sasa kosa la Tanzania ni nini mpaka Kagame amtukane Raisi wetu?

..hivi hushangai jinsi jambo hili lilivyowaunganisha wa-Tz hapa JF?

..Kabila anazungumza na M23 ingawa baadhi ya makamanda wa kikundi hicho wana tuhuma za mauaji ya kimbari dhidi ya wananchi wa DRC.

..Kagame ameshauriwa, na JK na tena nchi za SADC, kuzungumza na waasi wa FDLR. ameshauriwa azungumze na wale tu ambao hawakushiriki ktk genocide. tatizo liko wapi hapo??
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom