Kagame ndani ya Congo, sisi kiherehere cha nini?

Ukweli hiki ni kiherehere. Tanzania inakwenda DRC kutetea na kulinda raslimali za Congo? Kweli? au nayo inapora?

Soma Post Yangu Mkuu Nimeandika Kila Kitu na Nimejibu Baadhi Ya Maswali Yako. Nakushukuru Pia Kwa Kuwa Critical ktk Hili. Nimefurahi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Itakuwa Kikwete ana maslahi binafsi na hii operation ya kongo, kama kweli anasaidia kuwepo na aman katika nchi za Africa basi apeleke jeshi SOMALIA aone mziki wake.

Mkuu Ulipoamkia Leo Naomba Uwe Unalala Hapo Kila Siku. Umenipa Raha Na Kuifanya Asubuhi Yangu Kuwa Nzuri na Yenye Furaha. Akhsante Kwa Post Yako Hii Na Hakika Sasa Wayahudi Weusi Tunaanza Kuongezeka Nchini Tanzania. Watanzania Wa Leo Siyo Wa Jana Kwani Wanajua Pumba na Mchele.
 

Full of TITO and GIGO.................................!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 


Bila shaka wewe ni kizazi cha facebook,madhara ya kutopita NATIONAL SERVICE,
Fikra zako ni finyu sana,usiongee mambo ambayo una uelewa nayo,nenda kasome kwanza.
 

Wewe ina elekea unachojua sana humu duniani,ni kutumia facebook tu,unawezaje kuongea pumba kiasi hicho,nina wasiwasi hata kama elimu ya darasa la saba umemaliza,
 
Ati?!!!!
 

kwa taarifa yako kagame ni mtutsi-extremist. kwake yeye waafrika wote tofauti na watutsi ni watumwa, akija Tanzania sijui utasemaje.
 

eti wayahudi,.....sema mende!
 
haya ndio majitoto ya haramu ya Kinyaruanda yaliyohifadhiwa Tz. sina hata la kucomment namuona mwehu tu
 

wewe utafaidika nini? Mbona hamna heshima na nchi jirani!?
 



Yaani shukurani yao ni kuja kufanya utapeli na uwizi kwa kushirikiana Mafisadi mifano iko mingi
Hizi ni za South Afrika ebu pima hizi ndiyo zawadi wanayoweza kutupatia


1.NBC
2.NET Group solution
3. ATC
4.............
5............

 

Huyo Mnyarwanda aliminywa kimya kimya na intelijensia ya jeshi,Aliyemmaliza ni mwanamama mwanausalama wa jeshi aliyepewa jukumu la kumfuatilia mara baada ya kushtukiwa nyendo zake.
 

Unaelewa maana ya uzalendo wewe?
 
hoja yako haina mashiko.ukumbuke kwamba leo ni congo kesho itakula kwetu.ni muhimu kwa jeshi letu kwenda kuwasaidia ndugu zetu wakongo kwani kinyume na hapo kesho hawa wanyarwanda watatugeukia sisi.nashangazwa sana na kauli hii potofu kwa huyu jamaa yetu.ujue vision ya mwalimu nyerere ni kuona afrika nzima kuwa huru.wakongo wakiwa na amani hata sisi tutakuwa na amani lakini kongo isipokuwa na amani hata sisi watanzania amani yetu itakuwa mashakani.kagame akileta ujeuri ni lazima apigwe.huwezi kupeleka askari wake kwenda kuiba mali za wakongo,hii haikubaliki.watanzania tuwe wazalendo.nashangaa sana vijana wa sasa hivi wa kitanzania hawana uzalendo na nchi yao.vijana wengi hawaenda jeshini hata hawajui madhara ya vita hivyo wana wanabwabwaja tu
 
Mkuu inabidi ikumbuke hatukuenda sisi kwa matakwa yetu, tumeenda kupitia UN, kupitia UN lleo congo kuna majeshi zaidi ya nchi kumi. Tulienda pamoja na Malawi na South afrika lakini sijawahi kusikia hawa jamaa wengine wakigombana mabungeni mwao. Hii ni kawaida somalia wapo burundi na uganda, CAR ufaransa, rwanda na majeshi ya nchi kibao. Sielewi kwa nini sisi tunaongea saana kuhusu congo. Leo wakitokea M20 tanzania itabidi kama sisi un itume majeshi nchini kufanya kile tuachokifanya congo,
Hoja yangu sisi tusiwachanganye wanajeshi wetu na siasa. Mambo ya UN tuwaachie UN, sisi tukomae kuimarisha uchumi kupitia majirani. Pamoja na kushutumiwa kuiba mali ya congo, rwanda bado ni nchi inayoongoza kwa kupokea misaada africa. Ushauri wangu Nchi iachane na siasa za chuki na majirani, tuangalie jinsi tunavyowez kuwatumia kukua kiuchumi. Tuna safari ndefu jamani.
 
Wewe ndio mchafu unajua kuna vijana wetu wanakufa huko wanaacha watoto na wajane kwa ajili ya mali za wacongo zinatusaidia nini?

ndio kazi waliochagua kupigania taifa hili,kingine kaa ukijua kuwa amani ndani ya congo ndio amani ndani ya taifa hili,kwasababu akili yako ni yakushu=ikiwa huwezi kujua hili matusi ndo ulio fundishwa klakini sio kutoa tathimini za kweli
 
Wewe ndo mpuuzi sisi kupeleka jeshi Congo tunanufaika na nini zaidi ya vijana wetu kuawa huko na kuacha yatima kwanini Wacongo wameshindwa kujilinda,kwanini Marekani hakupeleka jeshi lake.

Yaan wewe unaweza muona jirani yako kavamiwa na uwezo wa kumsaidia unao halafu unaangalia tu.

Huo unaitwa uoga. Halafu na huyo kagame mnaemtetea ametutukana watanzania

Wewe utakuwa na matatizo mtu anakutukana wewe unamchekea, mwisho wa siku atakushika m@tak0

Halafu sisi wote ni watanzania (ila sina uhakika na wewe) pamoja na mapungufu yote tuliyonayo lakini katika suala la utaifa kama hili lazima tuwe wamoja kulinda heshima ya taifa letu
 
Tuna maslahi kubwa sana na Kongo, unajua ni asilimia ngapi ya Mizigo ya nje ya Kongo mashariki inapita kutumia bandari ya Dar es Salaam? Nenda Kasanga ziwa Tanganyika ndio utajua tunamaslahi gani na Kongo.
 
Uzalendo upi unaoujua ina maana kuipigania Congo ni Uzalendo????

Nakuuliza hivi wewe kama jirani yako anavamiwa (tena na mtu ambaye amewahi kukutusi) utajifungia tu ndan kwako bila hata kumsaidia??

Huo unaitwa uoga tena wa kike basi

Nyinyi vijana wa siku hizi mna matatizo sana, hivi unafikiri kina nyerere na nkrumah wangekuwa na mawazo mfu kama yako leo hii africa ingekuwaje?

Suala hapa ni ukombozi na si vinginevyo, na huo ndo uzalendo wa kweli, Africa ni yetu wote kwa hiyo hata kuipigania congo pia ni kuonesha uzalendo kwani wote ni waafrica.

AFRICA UNITE
 

endeleeni kujidanganya..
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…