Afrika iko tayari kwa ajili ya Rais mmoja

Afrika iko tayari kwa ajili ya Rais mmoja

Joined
May 3, 2019
Posts
53
Reaction score
145
AFRIKA IKO TAYARI KWA AJILI YA RAIS MMOJA.

Leo 13:15pm,14/07/2019.

Ahsante kwa kunitakia heri ya siku yangu ya kuzaliwa,Nami nachukua nafasi hii kuwasimulia ushindi wa hadithi kuu ya Afrika,ndoto njema iliyootwa na Wazee wetu Kwame Nkrumah na Julius Nyerere juu ya kuliunganisha bara la Afrika kuwa moja chini ya Rais mmoja ili kuleta sauti moja ya usimamizi wa maliasili nyingi zinazopatikana katika bara la Afrika.

Afrika sasa imekomaa Viongozi wapya wanazaliwa,Viongozi wenye fikra na maono kama ya Julius Nyerere na Kwame Nkrumah.Uwaonapo Viongozi hao katika Afrika,inakupa picha kuwa huu ni wakati mpya wa kutimiza ahadi ya waasisi wetu Julius Nyerere na Kwame Nkrumah,

Ila tu wakati huu,haitakuwa tena Kwame Nkrumah na Julius Nyerere watakaoamua mustakabali wa Afrika. Badala yake itakuwa Viongozi wa sasa wa Afrika kama John Magufuli,Paul Kagame,Cyril Ramaphosa,Uhuru Kenyatta,Mohamed Buhari,Nana Akufo Addo na pengine George Weah,

Na juu ya yote itakuwa vijana—kizazi kipya kilichojawa na uthubutu na vipawa na nguvu na matumaini—ambao wanaweza kudai mustakabali wa Bara zima la Afrika ambao tuliukosa katika kizazi cha baba zetu ambapo Mabepari Wazungu hawakutupa nafasi kamwe.

Miaka hamsini iliyopita mhubiri mmoja kijana aliyeitwa Martin Luther King, alisafiri toka Marekani kuja hapa Afrika, kushuhudia bendera ya Uingereza ikiteremka na bendera ya nchi kama Ghana ikipanda juu ya Bunge na Bendera ya Tanganyika ikipandishwa juu ya Mlima Kilimanjaro,

Hii ilikuwa baada ya maandamano ya watu weusi mjini Washington lakini kabla ya mafanikio ya harakati za kupigania haki za kiraia katika nchi ya Marekani,

Dakta King alipokuwa Afrika aliulizwa jinsi alivyojisikia kushuhudia kuzaliwa kwa mataifa mapya hapa Afrika. Na akasema “Inafufua imani yangu katika ushindi wa mwisho wa haki." Ndoto ya Martin Luther ilikuwa ikielekea kutimia.

Uhuru ni urithi wetu na Umoja ni nguvu zetu. Sasa, ni wajibu wetu kujenga juu ya msingi wa uhuru na Umoja. Na tukifanya hivyo, tutatazama nyuma miaka ya baadaye kutoka leo,na kusema huu ni wakati ambapo ahadi ilitimia—huu ni wakati ambapo ustawi ulibuniwa; uchungu ulishindwa; na enzi za maendeleo zilianza. Huu unaweza kuwa wakati ambapo tunashuhudia tena ushindi wa kiuchumi.

-Afrika iko tayari kujinyakulia mustakabali mpya wa Muungano wa Mataifa ya Afrika.

Tulihitaji muamko wa kisaikolojia juu uangalizi mkamilifu wa maliasili zetu ili ziweze kunufaisha bara la Afrika na si bara lingine,imefanyika hivi licha ya hali ngumu ya zamani,

Tumepata nguvu kutoka kwa urithi wetu wa Kiafrika.Sasa tuna taasisi imara na utashi imara,Sasa tuna viongozi wenye maono ya Afrika kujitegemea kwa kila kitu,Rais John Magufuli na Rais Paul Kagame wanaweza kutimiza ndoto za Afrika kujitegemea kutokana na wingi wa rasilimali ilizonazo,

Tunaweza kuwa na Bank kubwa ya Afrika itayotoa mikopo kwa nchi za Afrika,tuna madini ya dhahabu,Almasi katika nusu ya bara la Afrika na Tanzanite katika nchi ya Tanzania,tunaweza kuijenga Afrika kuwa kama Ulaya kwa kutumia dhahabu,almasi na Tanzanite tu,tukiachilia mbali rasilimali nyingine zilizojaa katika bara la Afrika.

-Afrika yenye Utajiri wa Mali asili.

Bara lina utajiri wa mali asili. Na kuanzia wajasiriamali wadogo hadi wakulima,na Wafanyabiashara wameonyesha uwezo na kupania kuunda fursa zao wenyewe. Lakini tabia za kale pia lazima zivunjwe. Kutegemea bidhaa—au zao moja linalouzwa nje ya nchi-- kunarundika utajiri mikononi mwa wachache, na kuwaacha watu wengi wakiwa masikini wa kutupwa.

-Kauli mbiu ya Ujenzi wa miundo mbinu ya nishati na Ujenzi wa Viwanda.

Kwa mfano wa Korea Kusini hadi Singapore, historia inaonyesha kwamba nchi hustawi zinapowekeza katika watu wao na miundombinu; tunapoendeleza viwanda mbalimbali vya uuzaji wa bidhaa nje ya nchi, kuunda kundi la wafanyakazi wenye ujuzi, na kuumba nafasi kwa biashara ndogo ndogo na za kati, na zinazobuni kazi,hii itakuwa hatua kubwa kwa watu wa Afrika kupata ujira wa kuendesha maisha yao.

Afrika ineanza kupanua ustawi kupitia ushirikiano wa umma na makundi ya kibinafsi ambao unawekeza katika barabara bora na umeme na hili tunaweza kuliona Tanzania,ikiwa ni juhudi za Rais John Magufuli,Ujenzi wa uwezo unaowafundisha watu kukuza biashara, huduma za kifedha zinazofikia sehemu maskini na zile za mashambani.

Hili ni kwa ajili ya maslahi mapana ya Tanzania na bara la Afrika,kwa kuwa watu wanaponyanyuliwa kutoka kwenye ufukara na utajiri kuundwa Afrika, masoko mapya yatafunguka kwa bidhaa zetu na wazungu watanunua vitu vilivyochakatwa na kutengenezwa katika bara la Afrika.

Afrika tunaweza,kama tuliweza basi tunaweza kuifanya tena Afrika kuwa Great Again, Nchi kama vile Tanzania na Kenya, ambazo zilikuwa na uchumi mkubwa kwa mtu mmoja mmoja kuliko Korea Kusini na Korea Kaskazini kwenye miaka ya sitini,hivi sasa zimepitwa vibaya sana.

Katika sehemu kubwa ya Afrika matumaini ya kizazi cha baba zetu Julius Nyerere na Kwame Nkrumah yamegeuka kuwa ubeuzi, hata kukatisha tamaa lakini tunao kizazi kipya chenye ndoto na maono sawa ya Kwame Nkrumah na Julius Nyerere, Vijana hao ni Rais John Magufuli na Rais Paul Kagame.

-Tunahitaji kuijenga Afrika yetu wenyewe.

Hakuna nchi itakayoumba utajiri ikiwa viongozi wake wanatumia uchumi kujitajirisha wenyewe, au polisi wanaweza kununuliwa na walanguzi wa madawa ya kulevya.

Hakuna biashara yoyote inayotaka kuwekeza mahali ambapo Viongozi wasio waadilifu wanajichukulia asilimia 20 hivi hivi au mkuu wa Mamlaka ya Forodha ni mla rushwa. Hakuna mtu yeyote anayetaka kuishi katika jumuiya ambako utawala wa kisheria unageuzwa kuwa utawala wa hongo.

Katika karne ya 21, taasisi zenye uwezo, zinazotegemewa, na zilizo wazi ndizo ufunguo wa mafanikio -- mabunge yaliyo imara na majeshi ya polisi yaliyo maaminifu; mahakimu na waandishi wa habari walio huru; sekta ya kibinafsi iliyochangamka na jumuiya ya kiraia. Hivi ni vitu vinavyoipa demokrasia uhai, kwa sababu ndivyo vitu vyenye maana katika maisha ya watu.

-Historia inaibeba Afrika kama nguvu ya maendeleo duniani.

Tumeona waafrika wakiijenga Marekani,tumeona rasilimali za Afrika zikiijenga Ulaya,tumeona Afrika ikisaidia uchumi wa bara la Hindi,Tumeona maendeleo ambayo yamefanyika na kumekuwepo na maendeleo mengi katika sehemu kadhaa za Dunia,hii inathibitisha Afrika kuwa nguvu ya Maendeleo duniani,lakini kwa nini Afrika yenyewe haiendelei au kwa nini nguvu hizo hazitumiki kuendeleza bara la Afrika na matokeo yake tunangoja tuwe soko la bidhaa zenye asili yetu zikinakshiwa Ulaya,Marekani na Asia na kuletwa kuuzwa Afrika!?

-Changamoto zinazoikumba bara la Afrika.

Bila shaka tunajua kwamba si hadithi nzuri kuiona sura ya Afrika ambayo mara nyingi mno inapuuzwa na ulimwengu ambapo yanaonekana tu maafa au mahitaji ya hisani.

Afrika imejibidisha kuiweka demokrasia katika mizizi imara, kukiwepo mabadiliko ya utawala kwa amani hata katika uchaguzi ulioshindaniwa vikali,tunaweza kuitolea mfano nchi ya Ghana na Tanzania.

Utakapotembelea Tanzania na Ghana utakuta utawala ulioboreka na jamii inayoibuka ya kiungwana, uchumi wa Afrika kwa nchi hizi umeonyesha kima cha kuvutia cha ustawi katika jamii.

-Afrika si bara la vita bali bara la Amani hata kabla ya kuligawa bara hili.

Afrika si karagosi wa bara lililokumbwa na vita. Lakini kwa Waafrika wengi mno, migogoro imekuwa sehemu ya maisha, ikidumu kama vile jua. Tunaweza kuinyooshea kidole Ulaya na Marekani lakini bado kuna vita ya kugombea ardhi na maliasili. Na bado ni rahisi mno kwa wale wasio na dhamiri kuchochea jumuiya nzima kupigana miongoni mwa imani na makabila.

-Afrika si bara la Vifo na Magonjwa.

Takwimu zinaonyesha watu wengi zaidi wanaishi kwa uzalishaji wakiwa na vvu/ukimwi hasa kusini mwa jangwa la sahara,wengi wanapata dawa zinazohitajika. Lakini wengi mno bado wanakufa kutokana na magonjwa ambayo hayapaswi kuwaua. Watoto wanapouawa kwa sababu ya kuumwa na mbu, na akina mama wanakufa wakati wa Fuji fungus, ndipo tunatambua kwamba lazima maendeleo yafanyike,lazima Afrika tuchukue hatua ya kulinda uzao wetu sisi wenyewe pasipo kuwasubiri wazungu.

Madaktari na manesi wengi wa Afrika inaeleweka huenda nchi za ng’ambo, au hufanyia kazi programu zinazopambana na ugonjwa mmoja tu.

Hii inaunda pengo katika matunzo na baths za kimsingi za kuzuia magonjwa. Wakati huo huo, Waafrika binafsi lazima wafanye maamuzi ya kuwajibika yanayozuia kuenea kwa magonjwa, huku wakiendeleza huduma za afya katika jumuiya na nchi zao.

Waafrika tunapaswa kuitunza thamani ya kila mtoto katika Darfur na heshima ya kila mwanamke nchini Congo. Hakuna imani au utamaduni unaohalalisha maovu wanayotendewa. Sisi sote lazima tujitahidi kutafuta amani na usalama unaohitajika kwa ajili ya maendeleo.Hii ndilo tunalopaswa kupigania ili kuifanya Afrika kuwa mahali salama zaidi.

Nimalizie kwa kusema,Afrika imekomaa sasa na Viongozi wapya wamezaliwa. Huu ni wakati mpya wa ahadi.Haitakuwa tena Ulaya au Amerika kutuamulia mambo juu ya mustakabali wetu Afrika.Ni wakati wa kuitimiza hadithi kuu na ndoto njema iliyootwa na Wazee wetu Kwame Nkrumah na Julius Nyerere. Mungu ibariki Afrika,Mungu wabariki watu wa Afrika.

Nikiishia hapa,Mimi ni,
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854.
 
Muongo huwa anaongea maneno mengi sana.

Na no za simu umeweka uli wakutambue ni nani kabsa!

Umesahau kuwa africa sasa inatafunwa na hiki kizazi kipya cha kujipendekez. Akiamungu kama wakoloni wangekutana na hiki kizazi kama chako, tungekuwa tunatawaliwa mpaka leo.
 
Ni hadithi za kufikirika zaidi kuliko ukweli.
 
Bado sana baso sana. Afrika imegawanyika sana. Itachukua miaka mingi sana
 
Sababu kubwa ya kuungana na kua Rais moja si hoja...kama kupunguza umasikini kwa nchi moja imewashinda na nchi ikiwa moja sijui mtatawalaje wakati kila kukicha mnagombania madaraka
 
Na uhoro wa madaraka wa viongozi wa Afrika pamoja na kupinduana kila uchwao wataweza kuungana na kuwa nchi moja?achilia mbali afrika mashariki waliko shindwa kuwa na nchi moja yenye kuongozwa na Rais moja,Zanzibar yenyewe ambayo ni kama wilaya moja wameshindwa kuwa na muungano wa kweli wenye nchi moja,inayoongozwa na Rais mmoja,kwa sababu ya uroho wa madaraka kila mtu anataka awe rais nchini kwake.
 
Kuhusu bara la Africa kuunganika na kuwa kitu kimoja kwanye sector zote nyeti... bado sana...

Nchi za magharibi hawawezi kukubali kuruhusu hilo litokee na wanafanya hujuma za aina zote na kila njia jambo kama hilo lisitokee...

Ndiyo maana kila anapotekea kiongozi imara mwenye msimamo barafani Africa lazima aangushuwe kwa namna moja au nyingine...


Cc: mahondaw
 
Siku tukiweza kujitoa kwenye hiki kitanzi ndiyo mwanzo wa Maendeleo yetu endelevu.Swali ni je,tuanzie wapi?
Kuhusu bara la Africa kuunganika na kuwa kitu kimoja kwanye sector zote nyeti... bado sana...

Nchi za magharibi hawawezi kukubali kuruhusu hilo litokee na wanafanya hujuma za aina zote na kila njia jambo kama hilo lisitokee...

Ndiyo maana kila anapotekea kiongozi imara mwenye msimamo barafani Africa lazima aangushuwe kwa namna moja au nyingine...


Cc: mahondaw
 
John huyu huyu wa chattle? Hivi wewe ulikwenda shule kusomea ujinga?
 
Unaota mchana wewe, Afrika ipi ya kuwa na rais mmoja? Nani anakubali kupoteza kwa ajili ya mwenzake? Sikia kina JPM, Kagame, Mseveni, Nkurunzinza wanachofanya pale mtu anapoonekana kuhatarisha ulaji wao. Kwa taarifa yako hata East Africa kuwa na rais mmoja haiwezekani kamwe
 
 
Huo utafiti umefanyia chumbani kwako na kwa kuwa kuna uhuru wa kuwaza utakavyo basi ndoto yako itumike ndani ya mipaka ya chumba chako!
 
Africa sasa ikiungana inamana rais atakuwa mmoja tu alafu wapendwa wetu marais waliobaki waende wapi? Utawapa kazi gani? hiyo sahau mkuu. Na Benki kuu iwe moja alafu wafanyakazi wa nchi zingine kwenye benki kuu zao waende wapi? Nchi gani itakubali kupoteza identity yake kama Bendera, utambulisho wa pesa yake n.k. Hiki labda kitatokea YESU akikalibia kurudi.
 
Wafaransa hawawezi kukubali..maisha Yao yanategemea makoloni yote ya Afrika
 
Mind set za watawala wanaojenga na kupendelea miradi ya kila aina vijiji wilaya na mkoa waliitoka hawa ndio wa kuungana kweli ?
 
Muongo huwa anaongea maneno mengi sana.

Na no za simu umeweka uli wakutambue ni nani kabsa!

Umesahau kuwa africa sasa inatafunwa na hiki kizazi kipya cha kujipendekez. Akiamungu kama wakoloni wangekutana na hiki kizazi kama chako, tungekuwa tunatawaliwa mpaka leo.
Bara la afrika haliwezi kusimama lenyewe maana hata uchumi wake unakuwa determined na trends za huko kwingine.
 
Back
Top Bottom