KAFULILA aeleze alipata wapi Shahada ya "BBA" na Mwaka gani

KAFULILA aeleze alipata wapi Shahada ya "BBA" na Mwaka gani

kwani sifa ya kugombea ubunge unatakiwa kuwa na degree ngapi?
 
Unadhani wadau wote wana contact zake au wana muda wa kumfuatilia? Wewe uliyeleta taarifa hizi ndio uthibitishe amedanganya vipi?
 
kama kweli huyu bwana mdogo kaghushi elimu basi ni aibu.......
 
Kwa jinsi jamaa zake kafulila wanavyo mshambulia mtoa mada naanza kuamini huyu jamaa ameweka mada ya ukweli. Kama huyo kafulila anasoma huu uzi aje ajibu tuhuma au awatumie nyinyi mnaotoa mapovu kumtetea kujibu tuhuma. Lakini kwa mwenendo wa watoa maoni naamini kweli jamaa kafoji nyeti
 
Mwandiga mtajiita majina yote ya Kigoma kama,Mwanga,Kibirizi,Ruiche,Uvinza,Bangwe,Kazuramimba,Gwarama,Manyovu yaani majina yote lakini,kudanganya ni kudanganya tu,tena kwa kughushi nyaraka ni kosa kubwa,ila hoja ya msingi ni namna mleta mada alivyoiweka inatia mashaka na kila nnikisoma majina ya walio-comment naona ni watu kutoka kwa wala ugali wa lowe,ukiangalia wengine hata post zao ni kuanzia matatizo ya Kafulila yalipoanza,sasa napata picha ya kwamba huenda ni namna ya kujaribu kumchafua,na hata hivyo umaarufu wa Kafulila haukuletwa na elimu yake ni utumishi kwa umma,sasa kama hoja ni kulidanganya bunge ni kosa lakini ifahamike kwamba hata jeshini au TISS ambako kuna wale ma-LY,yaani la saba haimanishi kuwa huko kuna ruksa ya kudanganya,usije ukataka kuonyesha ubunge ni muhimu sana kuliko kitu kingine,je Kakobe nae atasemaje?cha msingi ni nyini kuwathibitishia wana JF uongo wa Kafulila kama mna taarifa in detail.ila narudia tena nina mashaka na tuhuma hizi
 
Ni bora uwe malaya wa kiume kuliko shoga wa kiume na huku ndan una mke mwenye hamu lakini we unahamu na wenzio zaidi
kazi ipo jf
 
Kama kafoji ashitakiwe kama wahalifu wengine msitetee wahalifu
 
Tatizo hapa ni kwa nini hili suala linaibuliwa kipindi hiki ambapo kafulila kapata matatizo katika chama chake. Hapa hatujadili mambo ya hisia, a.k.a chuki binafsi, majungu. Tuletee hoja zenye mashiko.
 
kwani sifa ya kugombea ubunge unatakiwa kuwa na degree ngapi?

Unahitajika kuwa na degree zifuatazo:

1) Kujishinda mwenyewe, ili usiwaibie watz rasilimali kidogo zilizoachwa na mafisadi;
2)Kutambua kuwa wapiga kura ndo waajiri wako, hivyo una-ahidi kuishi pamoja nao na kupata mawazo ya kero zao kila wakati; na siyo kuwa pamoja nao mwaka wa 4.5 ukiwaunanyemelea kuchaguliwa tena;
3) Ufisadi kwako uwe kama kum-tizama mama mkwe sehemu nyeti;
4) Mwenye dhamira hai - unasema unacho maanisha na unatenda hivyo hivyo - tehe tehe, maisha bora kwa ......; ili hali wengine wanatama jana, wanafunzi wamekaa chini, mwalim kakopwa miezi 12 na dktr kakopwa miezi 6 wakati msinziaji pale mjengoni anavuta Sh 200K/day;

Ongeza zingine kwa kadri inavyofaa
 
Kama Kafulila alidanganya kuhusu elimu yake; mtaoa mada alikuwa na wakati muafaka; kumwekea pingamizi Kafulila kwenye tume ya uchaguzi, wakati akigombea ubunge.Si vimbaya kuhoji elimu ya mtu unapoitilia shaka,au kama unauhakika na unachokisema. Na hapa ieleweke Kafulila hakulidanganya Bunge; kazi ya bunge si kuhakiki elimu au vyeti vya wabunge;bali ni Tume ya uchaguzi ndiyo yenye wajibu huo kupitia kila fomu ya mgombea. Mimi hapa ndipo inaponipa shida, kwani aliogobea nao hawakuliona hili la elimu ya Kafulila na kuliwekea pingamizi??
 
Acha ungese wewe mtoto wa kiume hao wenye elimu mf mkandara prof,dr dr dr dr kikwe.te,dr mkulo,dr mbilinyi,dr hosea,chenge,lowasa,rostam,dr bana wamelifikisha wapi hili taifa? Kadanganya nchimbi udoctor mbona bado yupo? Sie hatuangalii elimu tunataka kuona kalifanyia nin hili taifa? Elimu yake haitotusaidia kwani wanaoendesha nchi hawana elimu kabisa mf J4 kishimba nenda kaulize ,pia kuna mb mwanza wa ccm ana elimu ya std ii lkn hata aje prof asimame nae kwenye ubunge ashindi:;

Haya nenda kwa mbatia ukachukue posho yako
 
Acha ungese wewe mtoto wa kiume hao wenye elimu mf mkandara prof,dr dr dr dr kikwe.te,dr mkulo,dr mbilinyi,dr hosea,chenge,lowasa,rostam,dr bana wamelifikisha wapi hili taifa? Kadanganya nchimbi udoctor mbona bado yupo? Sie hatuangalii elimu tunataka kuona kalifanyia nin hili taifa? Elimu yake haitotusaidia kwani wanaoendesha nchi hawana elimu kabisa mf J4 kishimba nenda kaulize ,pia kuna mb mwanza wa ccm ana elimu ya std ii lkn hata aje prof asimame nae kwenye ubunge ashindi:;

Haya nenda kwa mbatia ukachukue posho yako
Ungekuwa basi ningekufunga kizibiti mwendo!
 
tunataka atueleze aliipata wapi? hata machali ana haki ya kuhoji iwapo anaelewa kuwa kafulila kalidanganya bunge kuhusu elimu yake?hoja ya msingi ni kafulila atueleze alisoma wapi na lini? kwa kuwa ni kfulila maneno kama ya chuki yameanza,ila kwa lukuvi, nchimbi,mkulo wakihojiwa elimu zao na kuitwa mafisadi wa elimu safi. Atueleze ilipata wapi hiyo BBA

Mkuu mnataka na nani? Sema ninataka! Patriote amekukumbusha hapo juu kwamba tumia umoja sio wingi! Kitu kingine umetanguliza jaziba badala ya hoja! Hapa tunajadili hoja na sio jaziba za mtu!!
 
Pole kaka,ebu weka na wewe elimu yako kwanza,maana kuna taarifa kwamba na wewe elimu yako ni ya Upendo Center una certificate ya ushonaji.
 
Hii mada ni ya muhimu sana ningeomba Mods waihamishie kwenye hoja nzito .Naona vijana wa kafulila leo wameidaka hoja mapema na tena juu juu ili kuipotezea.Suala hata kama yeye ni mbunge wa upinzani ama hoja imechelewa kuletwa ,bado mtoa hoja ana hoja yenye mashiko.Kwa nini adanganye kuhusu Elimu yake?. Kafulila anajulikana kwa uwezo wake wa kujenga hoja japo ana mapungufu yake ila hili la kughushi elimu kama ni kweli siungani na wanaomtetea. TENA NI VYEMA SANA KWA WATU AMBAO WANALITAKIA MEMA TAIFA HILI NA USTAWI WA SIASA SAFI WAKALIKEMEA HILI . KAMA HAWA AMBAO WANAIZOMEA SERIKALI KWA UCHAFU ULIYOPO,HALAFU WAO SIO WASAFI TAIFA LINAELEKEA WAPI?
 
elimu yake ina mustakhbali gani na taifa letu?
kwani waliosoma na ni wanasiasa wamelifanyia nn taifa zaidi ya kulifisadi?
kabla ya kumhukumu kafulila tujiulize hilo
wapo kina dr nchi......mbi,dr ka...ma....la,mheshimiwa sana lu...kuviiiuuu na wengineo waliosoma vyuo vya kusadikika mbona hatuwasemi?
tuangalie wamelifanfia nn taifa kwani tushazoea kudanganywa kila kukicha.
 
jamaa si angekomaa tu aikamate hiyo BBA.Matatizo yameanza sasa.Hivi inawezekana kwa Tanzania,mbunge kuvuliwa ubunge kwa kosa la kudanganya elimu yake?
Mkuu kuna Mbunge alikuwa anaitwa Kihiyo wa Temeke alivuliwa ubunge kwa kosa hilo
 
Mleta hoja ana hoja, tumekuwa tukipigia kelele ufisadi wa elimu hasa kwa upande wa chama tawala kwa nini tuutee unapofanywa na upande wa upinzani? Ufisadi ni ufisadi tu haijalishi unafanywa na nani. Mleta hoja kasema Kafulila hakumaliza BBA yake pale UDSM, kama kuna mtu anajua kamaliza mwaka gani au sehemu nyingine amjibu, lakini kumwambia kuwa ana wivu hakuondoi tuhuma hiyo.
 
Back
Top Bottom