KAFULILA aeleze alipata wapi Shahada ya "BBA" na Mwaka gani

asilimia kubwa ya kashfa ya wanasiasa huchomoza wakati wa mivutano kuliko wakati wa amani. kafulila ana kesi ya kujibu hata kama amehumikuwa na chama chake kwa kesi yake ya mwanzo.
 
Great thinkers you should learn to call a spade a spade. You either refute what has been presented or challenge what has been presented but please stop attacking the presenter.
 
jamaa si angekomaa tu aikamate hiyo BBA.Matatizo yameanza sasa.Hivi inawezekana kwa Tanzania,mbunge kuvuliwa ubunge kwa kosa la kudanganya elimu yake?
 
piga ua kafulila hili analo dawa ni kujibu tu tuhuma hizi lakini akijaribu kutumia mbinu za magufuli za kukwepa hoja kwamba ni wabaya wake wanataka kummaliza amekwisha. kama amesoma kweli na kuiweka kwenye tovuti ya bunge siri ni ya nini?
 
mtu anayeiba elimu hawezi kuacha kuiba mali ya taifa hata kama jina lake ni kafulila
 
Wakuu mbona tunakuwa na dabo Standadi?
Au ukihiyo ruhusa kwa wapinzani na dhambi kwa ccm?
Hoja ni hoja tu hata kama imeibuliwa na mbaya wako as long as inamashiko
 
  • Thanks
Reactions: KXY
Eleza ulisoma wapi na kupata shahada ya BBA na kuamua kulidanganya bunge? Kama umeweza kulidanganya bunge, je wananchi umewadanganya mambo mangapi? Lete vyeti tuone, na useme ulisomea chuo gani gani hapa nchini, Malagarasi ameeleza ukweli. Ulisoma wapi? Kwa yeyote anayetaka kuthibitisha haya aende kwenye tovuti ya Bunge "www.bunge.go.tz" kisha afungue profile ya kafulila kwenye kipengele cha elimu yake,utakuta ameripotosha Bunge kuwa yeye ni Graduate wa BBA. Then muulize alisoma chuo gani,na alimaliza mwaka gani hiyo BBA?
 
tunataka atueleze aliipata wapi? hata machali ana haki ya kuhoji iwapo anaelewa kuwa kafulila kalidanganya bunge kuhusu elimu yake?hoja ya msingi ni kafulila atueleze alisoma wapi na lini? kwa kuwa ni kfulila maneno kama ya chuki yameanza,ila kwa lukuvi, nchimbi,mkulo wakihojiwa elimu zao na kuitwa mafisadi wa elimu safi. Atueleze ilipata wapi hiyo BBA

Mavyuo yoooote haya yamejaa dunia mzima leo unauliza alipata wapi BBA? Kama aliipata Nigeria ulitaka akutaarifu wakati anaenda kuichukua? na kama alisoma mtandaoni ulitaka akutangazie? au BBA ni UDSM pekee?
 
Great thinkers you should learn to call a spade a spade. You either refute what has been presented or challenge what has been presented but please stop attacking the presenter.

Mkuu, tatizo ni jinsi alivyowakilisha hoja yake, haihitaji akili kubwa kujua huyu ana bifu na Kafulila, ndiyo maana members humu wanamjibu kimtindo.
 
Bado ninsistiza, atueleze aliipata wapi na vyeti vyake vipo wapi? inaeleweka kuwa mpo wapenzi wa kafulila ambao mliwahi kuwashikia bango mawazili kadhaa kuwa ni mafisadi wa elimu, tunamtaka na jamaa yenu atueleze alisoma na kupata wapi shahada yake ya kwanza katika BBA na siyo kuja kubwabwaja? Atueleze, amezoea kusema uwongo sasa amekamatwa pabaya waziwazi, ktk hili hawezi kukwepa, akanunue vyeti udsm tuone kama anaweza. Aliipata wapi shahada yake? Umma unataka kujua, siyo kusema sema uongo halafu adhani hatujui

this is serious character assasination. Small minds discuss people. I just guess its MACHALI at work
 
Wivu wa kike huu! Hivi wewe Malagarasi ni demu? Confirm basi, unaboa tu! Mnafuatiliana sana! Pambafu
 
Unataka elimu yake ulimlipia Karo? Ubora wa elimu ni utumishi wake kwa Umma sio vyeti(makaratasi)acha ushamba

Haongelei ubora wa utumishi wa umma, anaongelea kulidanganya bunge na dunia kuwa ni degree holder usikurupuke au kudandia treni kwa mbele, soma hoja, jibu hoja. Unakuwa kama wa Facebook!? Utumishi bora hata STD seven wapi safi nenda jeshini, tiss utawakuta. Lakini mbunge kudanganya elimu yake ni aibu!
 
Kafulila kama kweli umejimaliza kisiasa...kwa nini usiwe kama wenzako kina Mbowe na Lema, wao kidato cha nne, hawana shinda na BBA.
Wametulia na elimu zao za mtaani
 
Tunataka mbunifu na mchapakazi vyeti hata wendawazimu wa ddm wanavyo acha kuleta mada za kimbea hapa,anachofanya havihitaji vyeti macho yanatosha
 
Malagarasi umetumwa?umelogwa?umechanganyikiwa?umevuta?umekula mirungi?hujala?umevimbiwa?au una PEPO?
wewe ni sehemu ya matatizo ya watanzania,kama sio gamba basi wewe ni gamba C.
Unasemaje?DKafulila hana BBA?OK fine huoni hata kama una hoja ya msingi itakuwa imeingia doa?kwanini usingekuwa interested na Kafulila kabla hajafukuzwa na NCCR-gamba C leo ndio unatuambia?alipokuwa analibana bunge liliojaa magamba na mafisadi wa elimu kama yeye unavyotaka kutuaminsha ulikuwa wapi?na je hao wenye degree za ukweli kama mkulu wa magogoni amelifanyia nini taifa,kina professor maji marefu nao wamo,Livingstone nae yumo,Makinda nae yumo,Jairo nae yumo ukilinganisha na Kafulila unadhani mwenye elimu kubwa ya kweli kalifanyia nini taifa hili,nami ameitumia vizuri elimu yake?na wewe labda kama hujui bongo hakuna elimu bali kuna vyeti tu ukibisha nitamwaga mboga na ugali,tunajua sana jinsi elimu ya bongo inavyotolewa kwa miaka ya hivi karibuni,unagombana na vyeti mbona hata Kariakoo,Tandika na kwingineko vipo tu?kinachomata ni kile unacho-deliver kwa jamii.
Usijionyeshe wivu na chuki binafsi,mimi wala simtetei Kafulila wala mimi sio NCCR,mimi ni Peoplesss ......Lakini pia sikatai kwamba hawezi kudanganya ninachokataa taarifa hii kuja leo na kwa jinsi dogo huyo-Kafulila alivyokuwa popular kisiasa,kwa nini usingetoa habari hizi mapema?Kuna uwalakini hapa
 
Back
Top Bottom