Threesixteen Himself
JF-Expert Member
- Feb 12, 2013
- 8,223
- 7,993
Anandika Chilumba (yule mpiga zumari wa JPM)
Matamshi aliyoyatoa Ndugu Rais leo hapa Unguja sikuyatarajia yatoke kwenye kinywa cha mkuu wa nchi, Haya yanamwagia mafuta kwenye moto.
Suala kama la pensheni au matibabu ya mtu aliyewahi kuwa Kiongozi ni la kisheria siyo hiyari ya mtu, Yaan hata umfumanie na mkeo Sheria inakutaka usaini na apewe. Mengine mmalizane wenyewe.
Na kwa kuwa Tumesema siasa zimeisha Basi tujitahidi kuzimaliza kweli, sare za vyama, vijembe na maneno ya ngebe kwenye mikutano ya serikali inawagawa raia.
Siku zijazo wasio wana CCM wanaweza kuacha kuhudhuria mikutano ya Kiongozi mkuu wa nchi kwa sababu wanajihisi wanyonge na wakiwa.
Tuzungumze Maendeleo, kufanya kazi na kubadili maisha yetu, hawa Wakosoaji na wapinzani watakuwepo daima, kuwashambulia katika jukwaa lililolipiwa kodi na watu wote ikiwemo wao si jambo la kiungwana.
Msema kweli ni mpenzi wa Mungu, Hotuba za Ndugu Rais katika ziara yake visiwani hazijanivutia wala kusisimua. Zimeiacha Zanzibar katika mtafaruku ule ule au mkubwa zaidi.
☝☝☝☝
Waswahili husema _"kenge huwa hasikiagi hadi damu imtoke masikioni"_. Masikio ya Chilumba yameanza kuonesha dalili za damu
!
!
Unasema wasihudhurie? umesahau ule waraka wa wafanyakazi wa tanesco? kwanza wakaambiwa wafike ofisini kwa ajili ya kuandikwa majina na ndipo waelekee uwanjani, agizo. Na nasikia maboti yalihusika kutoa watu unguja kupeleka pemba.