engine rock
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 1,389
- 1,418
Hahaaa..kagame style.Magufuli ni mtu wa visasi. Ana roho ya korosho iiyojaa hila na husuda.
Hahaaa..kagame style.Magufuli ni mtu wa visasi. Ana roho ya korosho iiyojaa hila na husuda.
Anandika Chilumba (yule mpiga zumari wa JPM)
Matamshi aliyoyatoa Ndugu Rais leo hapa Unguja sikuyatarajia yatoke kwenye kinywa cha mkuu wa nchi, Haya yanamwagia mafuta kwenye moto.
Suala kama la pensheni au matibabu ya mtu aliyewahi kuwa Kiongozi ni la kisheria siyo hiyari ya mtu, Yaan hata umfumanie na mkeo Sheria inakutaka usaini na apewe. Mengine mmalizane wenyewe.
Na kwa kuwa Tumesema siasa zimeisha Basi tujitahidi kuzimaliza kweli, sare za vyama, vijembe na maneno ya ngebe kwenye mikutano ya serikali inawagawa raia.
Siku zijazo wasio wana CCM wanaweza kuacha kuhudhuria mikutano ya Kiongozi mkuu wa nchi kwa sababu wanajihisi wanyonge na wakiwa.
Tuzungumze Maendeleo, kufanya kazi na kubadili maisha yetu, hawa Wakosoaji na wapinzani watakuwepo daima, kuwashambulia katika jukwaa lililolipiwa kodi na watu wote ikiwemo wao si jambo la kiungwana.
Msema kweli ni mpenzi wa Mungu, Hotuba za Ndugu Rais katika ziara yake visiwani hazijanivutia wala kusisimua. Zimeiacha Zanzibar katika mtafaruku ule ule au mkubwa zaidi.
[emoji121][emoji121][emoji121][emoji121]
Waswahili husema _"kenge huwa hasikiagi hadi damu imtoke masikioni"_. Masikio ya Chilumba yameanza kuonesha dalili za damu
Sio msukuma huyo....ana kabila lake.Jamaa bora asingeenda Zanzibar maana kwenda kwake hakujaleta faida yoyote zaidi ya kuwagawa wazanzibari. Tatizo la hawa watani zangu wasukuma ni ushamba, ila huu ushamba wa huyu jamaa yetu umepitiliza maana badala ya kupungua unaongezeka
Ndio maana kuna usemi unasema kiongozi ni wa kuzaliwa sio wa kutengeneza, kuna watu wameumbwa kuwa kuongozwa ila sio kuwa kiongoziKinachoangaliwa sio kufurahia au kutofurahia bali uhalisia wa kile ulichosema kama kiongozi na hekima iliyomo ndani yake
Nadhani alitaka kueleza ukweli kuwa yeye ni Rais wa tanzania nzima Na anaitawala Zanzibar pia. Hili la kumuambia shein kuwa wakikushinda nineleze. Wenzake walishindwa kuwarudisha katika nafasi yao hao ndugu zetu.kweli kabisa mkuu,rais yupo mstari wa mbele kuligawa taifa
Kweli kabisa tz tunashida ila wengine bado hawajatambuaNdio maana kuna usemi unasema kiongozi ni wa kuzaliwa sio wa kutengeneza, kuna watu wameumbwa kuwa kuongozwa ila sio kuwa kiongozi
Nchi hii tayari ni chafu labda kui dump tuu ndo kilichisaliaMkuu kuna kitu hakipo sawa, lazima tuseme bila kuogopa, zile sio kauli za Raisi wa nchi, tukimwacha aendelee kutoa kauli kama hizi atachafua nchi
Lakini si wingi wote huuUkiwa kiongozi sio lazima wote wafurahia unachosema au unachofanya
hivi hapo Lumumba,huwa unamtolewa ubongo wenu na kupewa mwingine!Ilibidi Seif aambiwe ukweli.....inaonekana huwa mnavutiwa na hotuba za Rais sababu kila kukicha mnamnukuu.....inapendeza sana hii.
katika kosa ambalo watz watakuja kulijutia ni kumchagua huyu bwana,..japo inasemekana alishinda mweny nywele nyeupe