KADA CCM: Rais Magufuli ameacha mtafaruku Zanzibar

KADA CCM: Rais Magufuli ameacha mtafaruku Zanzibar

Nilishasemaga huyu mtu atoe kazi yakuandikiwa hotuba yy anatiririka tu vinavyomjia kichwani..
 
Huyu malaika me sijawahi kumuelewa kwenye hotuba zake hata siku moja sijui anapatwa na matatizo gani awapo jukwaani anaweza kuongea a alafu at the same time akapingana nalo directly au indirectly.

Mwanza alisema anataka watu wote walipe kodi stahiki wakati huohuo anawafundisha wananchi namna ya kukwepa kodi kwa kusafirisha gunia mojamoja la mpunga kwa pikipiki badala ya kupakia kwenye Fuso zima na kulipishwa kodi kubwa aiseeee.

Huko Zanzibar amesema tuache siasa za uhasama uchaguzi umekwisha tujenge nchi wakati huohuo anamshangaa Shein kwa kusain karatasi za Maalim na kumsifia Jecha kweliii???


Huku Dar napo alisema wazee wamelitafuna taifa na wametuchakachua vya kutosha sanaa at the same time anawaambia mmefanya kazi nzuri laleni usingizi mtamu nitawalinda hakuna wa kuwagusa like serious.

Hapo ndio nikajua kumbe nilikua sawa kumpa Lowassa kura yangu.
 
Ivi Magu alienda kuwaunganisha Wazanzibari kweli ?

RAIS: hakuna mpinzani atatia mguu katika serikali yangu..
(sio kauli ya kibaguzi? lakini kwani Mrema vepe ?au kamsahau ?)

RAIS: huyo aliekataa kisima chake kutumiwa na watu wa chama fulani, mngemtumbukiza kisimani..

Na je aliekataa wapinzani kuingia kwenye serikali yake ?

RAIS: huwezi kukataa mkono wangu halafu nisaini stahiki zako..

Na je waliomzomea Mbeya, ndio atawatenga ?
 
Hivi ni lazima kiongozi wa kiserikali afanyapo ziara akusanye watu na kuwahutubia?
 
Rais mpenda kujenga Ukuta badala ya kujenga madaraja.........labda ana ajenda yake anaanda mazingira ngoja tuone,Mungu naomba unipe uhai nishuhudie mengi!!!
Hapa Kazi Tu!!!!
 
...wengine wanahubiri muungano...yeye anahubiri utengamano...so sad...alafu anakataza wenzake wasifanye mikutano(hata ya ndani)..wakati mikutano yake inajaa rangi za kijani....huku ni kuhubiri utengamano kwa kiwango cha kutisha....na visasi sasa anavisema kabisa bila kuficha...unahubiri kumnyima kiongozi mwenzako stahiki yake aliyofanyia kazi!...nawe ni kiongozi mkuu!...haya ni anayosema wazi....je yale anayofanyia mahasimu wake wa kisiasa bila kuyasema si majanga!
 
Magufuli lazima waambie ukweli,Hongera raid kwa kukemea uovu
 
Rais yupo sahihi hotuba mzima ndo mmeona Hilo mbona suala la maendeleo ya viwanda hamseni Na kukataza watu kununiana Na kuchomeana karafuu
Ya viwanda tumempuuza maana ni porojo tuu hana uelewa na hilo labda aweke mawazo yake butu pembeni awaachie wataalam wamshauri na kufanya kazi

Tatizo la huyu mungu wenu ni kujiona ana akili sana kuliko watanzania wote,sijui ni ushamba wa asili

Tatizo lingine ni kujiona akilini yuko makini sana kwa kutoa hotuba inayomjia kwa wakati huo,tulikwisha sema aandae hotuba awe anasoma haya yote makorokocho hatayasema hadharani atakua kaficha upuuzi huu ndani kwake

Kwa kweli tunawajibu wa kuombea hawa viongozi kama kuna misukumo ya kipepo ndani yao inayowafanya kuzungumza lolote bila kupima basi wawekwe huru
 
Tatizo lililopo ni wapinzani kupenda kubembelezwa kitu ambacho Magu hawezi na hapa ni lazima wanyooke tu.
 
'Huyo aliekataa watu wa Chama fulani kuchota Maji kwny kisima chake mngemtumbukiza kwny hicho hicho kisima'- Chatto's Boy!
 
AKA PRODUCER MAANA KILA KONA TUNASIKIA BEAT ZAKE MITHILI YA MAYBACK.HII SERIKALI NI MFANO WA STUDIO KWA BEATS PRODUCTION.....
 
Back
Top Bottom