Kabrasha: Jiko la kuoka wafu (cremation)

Kabrasha: Jiko la kuoka wafu (cremation)

Mimi huwa nawaza tu, sijui haya mawazo huwa nayatoa wapi, eti huwa nawaza kwa mfano mtu uzikwe harafu gafla upate fahamu ukiwa ndani ya jeneza, hilo joto lake sijui litakuwaje, nazani utakufa kifo kibaya zaidi[emoji23][emoji23]
Hatari zaidi ipo kwa wanaozika kiislamu yani yule mtu hawezi hata kujisogeza maana anafungwa miguuni, kiunoni yani mfano amefufuka hawezi kutoka maana wanachonga kaburi saizi ya mtu hawezi toka asilani
 
Ila wanavyochoma Japan imekaa vizuri sana unawekwa kwenye jeneza linaloungua wanabonyeza mashine mwili unaingia ndani taratiibu
 
Somo zuri sana, kila kazi ina process hadi kufikia level au uzoefu fulani, mkuu wewe ulianza moja kwa moja kuchoma watu au ulianza kuhudumu sehemu nyingine mfano mortuary
Ni kazi zilizoenda kwa pamoja ila experience ya kwanza ilikuwa kuchoma
 
Inaungua mpaka inakuwa majivu kabisa
Nielewavyo Mimi siyo kila particle ya mwili inapoteketezwa hugeuka kuwa jivu,mifupa huungua na baadhi hubaki kama particles ndogo ndogo na kubwa.
Kuteketea na kuwa jivu kamili kunahitaji muda na joto zaidi ukilinganisha na muda unaotumika kwenye tambiko la uchomaji
 
Nielewavyo Mimi siyo kila particle ya mwili inapoteketezwa hugeuka kuwa jivu,mifupa huungua na baadhi hubaki kama particles ndogo ndogo na kubwa.
Kuteketea na kuwa jivu kamili kunahitaji muda na joto zaidi ukilinganisha na muda unaotumika kwenye tambiko la uchomaji
Ok hebu tuone picha hii ya maiti iliyokwisha kuwa jivu
1b521ea52d82b8c4b0df41760a085139.jpeg
 
Nimetimiza ahadi ya kuleta mada husika. Mada ya uzoefu wa kuchoma wafu moto hadi wateketee kabisa na kubaki majivu.

Kuchoma moto maiti ni aina mojawapo ya mazishi.

Mazishi mengine ni

- Kuzika ardhini
- Kutupa mwili porini na kuwa chakula cha wanyama
- Kuweka mwili juu ya kichanja maalum karibu na makazi ili ndege wapate kula
- Kuweka mwili kwenye chumba maalum, kwenye majabali nknk (viongozi na watu maarufu)
- Kutumbukiza mwili kwenye pipa la tindikali
Nk

Mimi nimeshiriki kikamilifu kwenye haya mazishi ya kuchoma moto na nimewabanika wengi tu kwenye miaka yangu sita ya huduma

Kinachofanyika ni hiki. Taratibu zote hufuatwa toka mochwari mpaka kumremba marehemu tayari kwa kuagwa.

Baada ya hapo kifuatacho ni kuelekea makaburini kwenye jengo la kuchomea.
Mara nyingi mwili unapotolewa mochwari hupelekwa mpaka eneo la kuagia ukiwa mtupu bila nguo zaidi ya mashuka yale ya mochwari. Lakini ukiwa tayari umeshatengenezwa vema
Watu wa mochwari huukabidhi kwa ndugu na ndugu nao huukabidhi kwa wazikaji (mimi) hapa mwili unakuwa kwenye chumba maalum (inategemea na uwezo) wengine hufanyia nyumbani wengine ukumbini.

Huko kwenye chumba maalum ndugu watakupa nguo na chochote cha kumvisha marehemu. Ukishamaliza kumvisha na kumremba, mwili hutolewa na kuwekwa sehemu rasmi ya kuagiwa.

Shughuli ya kuagwa ikishaisha msafara wa kuelekea makaburini huanza.

Huko makaburini kuna sehemu kuu tatu muhimu
- Ukumbi wa ibada ya mwisho
- Jiko la kuchomea mwili (tanuru la gesi)
- Makaburi (yako kama vile vyumba ya mabox ya barua posta

Pale ukumbini jeneza huwekwa juu ya kichanja chenye sliders ambazo huenda moja kwa moja mpaka kwenye tanuru.

Hapa ndugu wanaopenda kumuona marehemu kwa mara ya mwisho kabisa huruhusiwa kufanya hivyo

Baada ya hapo jeneza husukumwa na kuingia sehemu ambapo pametenganishwa na kitambaa cheupe.Hapa hubaki mchomaji (mimi) na watu wake ambapo kwa mahitaji ya ndugu mnamvua marehemu vitu vya thamani nk.

Wakati huu tanuri maalum la gesi lenye nyuzi joto zinazofikia 1000 linakuwa tayari limeshawashwa. Kipindi hiki cha kumuandaa marehemu kwa ajili ya kumbutua ukumbi wote huwa kimya kabisa.

Shughuli fupi ya kumuandaa ikishaisha mchomaji (mimi sasa) hubonyeza switch maalum ambapo sliders huupeleka mwili kwenye tanuru kichwa kikiwa kimetangulia.. Kichwa kinapogusa tu mlango wa tanuru kuna taa nyekundu huwaka na king'ora cha ukiwa hulia kwa sauti ya chini kidogo

Basi hapo mwili utaingia wote na kile kimlango kujifunga kwa nyuma.... Dakika tano nyingi mnasikia kishindo cha kichwa kupasuka. Hapo taa ile nyekundu huzima, king'ora hukoma na kinachosikika sasa ni sauti za vilio vya ndugu, jamaa na marafiki huku wakitawanyika.

Dakika kati ya kumi na ishirini baadae kutegemeana na setting za moto mwili unakuwa umeungua na kuteketea kabisa na kubaki jivu. Jivu hupita sehemu maalum ya kupozwa. Baada ya hapo hutiwa kwenye kisanduku maalum (kaburi) chenye
Jina kamili la marehemu
Tarehe ya kuzaliwa
Tarehe ya kufa
Neno la faraja

Kufikia hapa mazishi yanakuwa yamekamilika na ndugu kuoneshwa kaburi la ndugu yao lilipo (kuna namba za makaburi) kisha kukabidhiwa funguo za kaburi na nguo ama vitu vingine kama vipo.
Mzee Mshana jr uwe una ni tag basi ukiweka mada zako tafadhali.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom