Kabrasha: Jiko la kuoka wafu (cremation)

Kabrasha: Jiko la kuoka wafu (cremation)

Hayo makaburi ni kwa muda hlf wanapisha wengine ama inakuwaje? Vyumba hvyo havijai majagi ya majivu au vinajengwa vipya kila vikijaa?
Ni ya milele kadiri wamiliki wanavyolipia.. Kunakuwa na ongezeko la makaburi mapya....
Yale makaburi baada ya muda watu huachana nayo na kuondoka na majivu yao
 
Brother hivi Kuna kitu kinakutisha dunia hii kweli ???... Maana experience zako ni mtihani
[emoji3][emoji3][emoji3] natishika na walio hai... Mioyo yao ni kiza kinene na imebeba siri kubwa
 
Naona Uchomaji Inaonekana Picture Ya Mwisho Mwili Hutoa Mafuta Mengi Sana Kama Shwain Vile
Kwa kuwa moto ni mkali sana kitendo cha kutoa mafuta wala harufu yoyote nafikiri kinakuwa hamna maana mwili unateketea kwa haraka sana
 
Acha kujidanganya ndugu. roho ikitoka sio mwisho wa maisha yako. Kuna maisha baada ya kufa. Tena unayaanza pale pale ulipo lala ukiwa umekufa.
Yote yana yofanyika unayasikia. na kama ni mtu mbaya utapata adhabu hapo hapo ulipo. Watakusikia watoto wachanga na wanyama pekee kelele zako.
Ndio maana binti yangu wa wiki mbili anahangaika kama kuna vitu anaviona
 
Sema mada imekaa kigoogle zaidi huku maswali yakijibiwa kijanja janja tu
 
Nimetimiza ahadi ya kuleta mada husika. Mada ya uzoefu wa kuchoma wafu moto hadi wateketee kabisa na kubaki majivu.

Kuchoma moto maiti ni aina mojawapo ya mazishi.

Mazishi mengine ni

- Kuzika ardhini
- Kutupa mwili porini na kuwa chakula cha wanyama
- Kuweka mwili juu ya kichanja maalum karibu na makazi ili ndege wapate kula
- Kuweka mwili kwenye chumba maalum, kwenye majabali nknk (viongozi na watu maarufu)
- Kutumbukiza mwili kwenye pipa la tindikali
Nk

Mimi nimeshiriki kikamilifu kwenye haya mazishi ya kuchoma moto na nimewabanika wengi tu kwenye miaka yangu sita ya huduma

Kinachofanyika ni hiki. Taratibu zote hufuatwa toka mochwari mpaka kumremba marehemu tayari kwa kuagwa.

Baada ya hapo kifuatacho ni kuelekea makaburini kwenye jengo la kuchomea.
Mara nyingi mwili unapotolewa mochwari hupelekwa mpaka eneo la kuagia ukiwa mtupu bila nguo zaidi ya mashuka yale ya mochwari. Lakini ukiwa tayari umeshatengenezwa vema
Watu wa mochwari huukabidhi kwa ndugu na ndugu nao huukabidhi kwa wazikaji (mimi) hapa mwili unakuwa kwenye chumba maalum (inategemea na uwezo) wengine hufanyia nyumbani wengine ukumbini.

Huko kwenye chumba maalum ndugu watakupa nguo na chochote cha kumvisha marehemu. Ukishamaliza kumvisha na kumremba, mwili hutolewa na kuwekwa sehemu rasmi ya kuagiwa.

Shughuli ya kuagwa ikishaisha msafara wa kuelekea makaburini huanza.

Huko makaburini kuna sehemu kuu tatu muhimu
- Ukumbi wa ibada ya mwisho
- Jiko la kuchomea mwili (tanuru la gesi)
- Makaburi (yako kama vile vyumba ya mabox ya barua posta

Pale ukumbini jeneza huwekwa juu ya kichanja chenye sliders ambazo huenda moja kwa moja mpaka kwenye tanuru.

Hapa ndugu wanaopenda kumuona marehemu kwa mara ya mwisho kabisa huruhusiwa kufanya hivyo

Baada ya hapo jeneza husukumwa na kuingia sehemu ambapo pametenganishwa na kitambaa cheupe.Hapa hubaki mchomaji (mimi) na watu wake ambapo kwa mahitaji ya ndugu mnamvua marehemu vitu vya thamani nk.

Wakati huu tanuri maalum la gesi lenye nyuzi joto zinazofikia 1000 linakuwa tayari limeshawashwa. Kipindi hiki cha kumuandaa marehemu kwa ajili ya kumbutua ukumbi wote huwa kimya kabisa.

Shughuli fupi ya kumuandaa ikishaisha mchomaji (mimi sasa) hubonyeza switch maalum ambapo sliders huupeleka mwili kwenye tanuru kichwa kikiwa kimetangulia.. Kichwa kinapogusa tu mlango wa tanuru kuna taa nyekundu huwaka na king'ora cha ukiwa hulia kwa sauti ya chini kidogo

Basi hapo mwili utaingia wote na kile kimlango kujifunga kwa nyuma.... Dakika tano nyingi mnasikia kishindo cha kichwa kupasuka. Hapo taa ile nyekundu huzima, king'ora hukoma na kinachosikika sasa ni sauti za vilio vya ndugu, jamaa na marafiki huku wakitawanyika.

Dakika kati ya kumi na ishirini baadae kutegemeana na setting za moto mwili unakuwa umeungua na kuteketea kabisa na kubaki jivu. Jivu hupita sehemu maalum ya kupozwa. Baada ya hapo hutiwa kwenye kisanduku maalum (kaburi) chenye
Jina kamili la marehemu
Tarehe ya kuzaliwa
Tarehe ya kufa
Neno la faraja

Kufikia hapa mazishi yanakuwa yamekamilika na ndugu kuoneshwa kaburi la ndugu yao lilipo (kuna namba za makaburi) kisha kukabidhiwa funguo za kaburi na nguo ama vitu vingine kama vipo.
 
Nafikiri crematorium center ya Koriokoor, Nairobi-Kenya ni ya kisasa ndipo alipofanyiwa maziko Robert Collymore, former CEO, Safaricom.
 
Ila haya ndiyo mazishi mazuri kuliko kuzika. Ni vizuri jamii zianze kutumia njia hii rafiki kwa mazingira
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom