Kabrasha: Jiko la kuoka wafu (cremation)

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,791
Nimetimiza ahadi ya kuleta mada husika. Mada ya uzoefu wa kuchoma wafu moto hadi wateketee kabisa na kubaki majivu.

Kuchoma moto maiti ni aina mojawapo ya mazishi.

Mazishi mengine ni

- Kuzika ardhini
- Kutupa mwili porini na kuwa chakula cha wanyama
- Kuweka mwili juu ya kichanja maalum karibu na makazi ili ndege wapate kula
- Kuweka mwili kwenye chumba maalum, kwenye majabali nknk (viongozi na watu maarufu)
- Kutumbukiza mwili kwenye pipa la tindikali
Nk

Mimi nimeshiriki kikamilifu kwenye haya mazishi ya kuchoma moto na nimewabanika wengi tu kwenye miaka yangu sita ya huduma

Kinachofanyika ni hiki. Taratibu zote hufuatwa toka mochwari mpaka kumremba marehemu tayari kwa kuagwa.

Baada ya hapo kifuatacho ni kuelekea makaburini kwenye jengo la kuchomea.
Mara nyingi mwili unapotolewa mochwari hupelekwa mpaka eneo la kuagia ukiwa mtupu bila nguo zaidi ya mashuka yale ya mochwari. Lakini ukiwa tayari umeshatengenezwa vema
Watu wa mochwari huukabidhi kwa ndugu na ndugu nao huukabidhi kwa wazikaji (mimi) hapa mwili unakuwa kwenye chumba maalum (inategemea na uwezo) wengine hufanyia nyumbani wengine ukumbini.

Huko kwenye chumba maalum ndugu watakupa nguo na chochote cha kumvisha marehemu. Ukishamaliza kumvisha na kumremba, mwili hutolewa na kuwekwa sehemu rasmi ya kuagiwa.

Shughuli ya kuagwa ikishaisha msafara wa kuelekea makaburini huanza.

Huko makaburini kuna sehemu kuu tatu muhimu
- Ukumbi wa ibada ya mwisho
- Jiko la kuchomea mwili (tanuru la gesi)
- Makaburi (yako kama vile vyumba ya mabox ya barua posta

Pale ukumbini jeneza huwekwa juu ya kichanja chenye sliders ambazo huenda moja kwa moja mpaka kwenye tanuru.

Hapa ndugu wanaopenda kumuona marehemu kwa mara ya mwisho kabisa huruhusiwa kufanya hivyo

Baada ya hapo jeneza husukumwa na kuingia sehemu ambapo pametenganishwa na kitambaa cheupe.Hapa hubaki mchomaji (mimi) na watu wake ambapo kwa mahitaji ya ndugu mnamvua marehemu vitu vya thamani nk.

Wakati huu tanuri maalum la gesi lenye nyuzi joto zinazofikia 1000 linakuwa tayari limeshawashwa. Kipindi hiki cha kumuandaa marehemu kwa ajili ya kumbutua ukumbi wote huwa kimya kabisa.

Shughuli fupi ya kumuandaa ikishaisha mchomaji (mimi sasa) hubonyeza switch maalum ambapo sliders huupeleka mwili kwenye tanuru kichwa kikiwa kimetangulia.. Kichwa kinapogusa tu mlango wa tanuru kuna taa nyekundu huwaka na king'ora cha ukiwa hulia kwa sauti ya chini kidogo

Basi hapo mwili utaingia wote na kile kimlango kujifunga kwa nyuma.... Dakika tano nyingi mnasikia kishindo cha kichwa kupasuka. Hapo taa ile nyekundu huzima, king'ora hukoma na kinachosikika sasa ni sauti za vilio vya ndugu, jamaa na marafiki huku wakitawanyika.

Dakika kati ya kumi na ishirini baadae kutegemeana na setting za moto mwili unakuwa umeungua na kuteketea kabisa na kubaki jivu. Jivu hupita sehemu maalum ya kupozwa. Baada ya hapo hutiwa kwenye kisanduku maalum (kaburi) chenye
Jina kamili la marehemu
Tarehe ya kuzaliwa
Tarehe ya kufa
Neno la faraja

Kufikia hapa mazishi yanakuwa yamekamilika na ndugu kuoneshwa kaburi la ndugu yao lilipo (kuna namba za makaburi) kisha kukabidhiwa funguo za kaburi na nguo ama vitu vingine kama vipo.
 
Sina picha halisi za vile nilikuwa nafanya.. Way back late 90's... Lakini hapa kuna picha chache kwa hisani ya Google
57646830-the-buddhist-thai-cremation-chamber.jpeg
dreams.metroeve_cremation-dreams-meaning-1024x576.jpeg
 
Asubuhi yote hii boss,utaharibubsiki za watu aisee!
Unafanyia wapo hizi shughuli? Mm nimeshuhudia wakichoma bila tanuri la gesi huko ughaibuni.
Nilisubiri kupambazuke sikutaka kupost usiku
Matanuri yapo ya kuni, umeme, makaa na gesi pia.. Kuna matanuri ambayo ni manually operated na kuna automatic... Ya kisasa zaidi... Mimi mengi nilitumia ya kisasa
dreams.metroeve_cremation-dreams-meaning-1024x576.jpeg
Casket-entering-cremation-chamber-680x350.jpeg
 
Baadhi ya ndugu hupenda mpenda wao achomwe mwili bila chochote kingine ili wapate jivu halisi
Wengine hupenda achomwe na kila kitu alichovishwa.. Ukikutana na mchomaji kichwa maji asiye mwaminifu huiba vitu vya thamani
1b521ea52d82b8c4b0df41760a085139.jpeg
 
Ahsante kwa elimu Mshana Jr
Sijui kwanini wengi wanaogopa sana kifo wakati ni kitu hatuwezi kukikwepa na kinapomfika mtu hana jinsi.

Kwa jinsi uhaba wa maeneo ulivyo na ongezeko la watu, hii ingeweza kuwa njia bora kabisa ya kuhifadhiana.

Kwanza inakupa mazoezi ya jehanum..(natania).
 
Back
Top Bottom