Kabrasha: Jiko la kuoka wafu (cremation)

Kabrasha: Jiko la kuoka wafu (cremation)

Nimetimiza ahadi ya kuleta mada husika... Mada ya uzoefu wa kuchoma wafu moto hadi wateketee kabisa na kubaki majivu....
Kuchoma moto maiti ni aina mojawapo ya mazishi... Mazishi mengine ni
Kuzika ardhini
Kutupa mwili porini na kuwa chakula cha wanyama
Kuweka mwili juu ya kichanja maalum karibu na makazi ili ndege wapate kula
Kuweka mwili kwenye chumba maalum, kwenye majabali nknk (viongozi na watu maarufu)
Kutumbukiza mwili kwenye pipa la tindikali
Nk

Mimi nimeshiriki kikamilifu kwenye haya mazishi ya kuchoma moto... Na nimewabanika wengi tu kwenye miaka yangu sita ya huduma
Kinachofanyika ni hiki.... Taratibu zote hufuatwa toka mochwari mpaka kumremba marehemu tayari kwa kuagwa... Baada ya hapo kifuatacho ni kuelekea makaburini kwenye jengo la kuchomea
Mara nyingi mwili unapotolewa mochwari hupelekwa mpaka eneo la kuagia ukiwa mtupu bila nguo zaidi ya mashuka yale ya mochwari... Lakini ukiwa tayari umeshatengenezwa vema
Watu wa mochwari huukabidhi kwa ndugu na ndugu nao huukabidhi kwa wazikaji (mimi) hapa mwili unakuwa kwenye chumba maalum (inategemea na uwezo) wengine hufanyia nyumbani wengine ukumbini
Huko kwenye chumba maalum ndugu watakupa nguo na chochote cha kumvisha marehemu.. Ukishamaliza kumvisha na kumremba, mwili hutolewa na kuwekwa sehemu rasmi ya kuagiwa...
Shughuli ya kuagwa ikishaisha msafara wa kuelekea makaburini huanza... Huko makaburini kuna sehemu kuu tatu muhimu
Ukumbi wa ibada ya mwisho
Jiko la kuchomea mwili (tanuru la gesi)
Makaburi (yako kama vile vyumba ya mabox ya barua posta
Pale ukumbini jeneza huwekwa juu ya kichanja chenye sliders ambazo huenda moja kwa moja mpaka kwenye tanuru... Hapa ndugu wanaopenda kumuona marehemu kwa mara ya mwisho kabisa huruhusiwa kufanya hivyo
Baada ya hapo jeneza husukumwa na kuingia sehemu ambapo pametenganishwa na kitambaa cheupe... Hapa hubaki mchomaji (mimi) na watu wake... Ambapo kwa mahitaji ya ndugu mnamvua marehemu vitu vya thamani nk....
Wakati huu tanuri maalum la gesi lenye nyuzi joto zinazofikia 1000 linakuwa tayari limeshawashwa.... Kipindi hiki cha kumuandaa marehemu kwa ajili ya kumbutua ukumbi wote huwa kimya kabisa...
Shughuli fupi ya kumuandaa ikishaisha mchomaji (mimi sasa) hubonyeza switch maalum ambapo sliders huupeleka mwili kwenye tanuru kichwa kikiwa kimetangulia.. Kichwa kinapogusa tu mlango wa tanuru kuna taa nyekundu huwaka na king'ora cha ukiwa hulia kwa sauti ya chini kidogo
Basi hapo mwili utaingia wote na kile kimlango kujifunga kwa nyuma.... Dakika tano nyingi mnasikia kishindo cha kichwa kupasuka.... Hapo taa ile nyekundu huzima, king'ora hukoma na kinachosikika sasa ni sauti za vilio vya ndugu, jamaa na marafiki huku wakitawanyika...

Dakika kati ya kumi na ishirini baadae kutegemeana na setting za moto mwili unakuwa umeungua na kuteketea kabisa na kubaki jivu... Jivu hupita sehemu maalum ya kupozwa... Baada ya hapo hutiwa kwenye kisanduku maalum (kaburi) chenye
Jina kamili la marehemu
Tarehe ya kuzaliwa
Tarehe ya kufa
Neno la faraja
Kufikia hapa mazishi yanakuwa yamekamilika na ndugu kuoneshwa kaburi la ndugu yao lilipo (kuna namba za makaburi) kisha kukabidhiwa funguo za kaburi na nguo ama vitu vingine kama vipo
Somo zuri sana
 
Nasikia wa Israel wanatumia jivu hilo kutengeneza almasi
Baadhi ya ndugu hupenda mpenda wao achomwe mwili bila chochote kingine ili wapate jivu halisi
Wengine hupenda achomwe na kila kitu alichovishwa.. Ukikutana na mchomaji kichwa maji asiye mwaminifu huiba vitu vya thamani View attachment 1158618
 
Hivi huwa ni kwa binadamu tu au kwa viumbe vyote? Yaani nauliza kama mbwa au mifugo mingine inapokufa wanaichoma pia au wanafukia ardhini kama tufanyavyo sisi? Na pia kwa wageni wasiotambulika wanaofia huko kwao nao pia huchomwa au lah! Na wakichomwa (Wageni wasiokua raia) majivu yao hupelekwa wapi na ni nani hugharamia uchomwaji wao?
Good question
 
Kuna jamaa nimepanda nae gari saiv nikitoka kwa Morombo (Arusha) kwenda mjini kati nimeona anaufatilia Sana huu uzi mana nilikuwa nae siti moja kwenye daladala ila akashukia Kona ya Mbauda

Respect sana kwako Mshana Jr. Kwa madini hatari kama haya
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji120][emoji120][emoji120][emoji123][emoji123][emoji106]
 
Nimetimiza ahadi ya kuleta mada husika. Mada ya uzoefu wa kuchoma wafu moto hadi wateketee kabisa na kubaki majivu.

Kuchoma moto maiti ni aina mojawapo ya mazishi.

Mazishi mengine ni

- Kuzika ardhini
- Kutupa mwili porini na kuwa chakula cha wanyama
- Kuweka mwili juu ya kichanja maalum karibu na makazi ili ndege wapate kula
- Kuweka mwili kwenye chumba maalum, kwenye majabali nknk (viongozi na watu maarufu)
- Kutumbukiza mwili kwenye pipa la tindikali
Nk

Mimi nimeshiriki kikamilifu kwenye haya mazishi ya kuchoma moto na nimewabanika wengi tu kwenye miaka yangu sita ya huduma

Kinachofanyika ni hiki. Taratibu zote hufuatwa toka mochwari mpaka kumremba marehemu tayari kwa kuagwa.

Baada ya hapo kifuatacho ni kuelekea makaburini kwenye jengo la kuchomea.
Mara nyingi mwili unapotolewa mochwari hupelekwa mpaka eneo la kuagia ukiwa mtupu bila nguo zaidi ya mashuka yale ya mochwari. Lakini ukiwa tayari umeshatengenezwa vema
Watu wa mochwari huukabidhi kwa ndugu na ndugu nao huukabidhi kwa wazikaji (mimi) hapa mwili unakuwa kwenye chumba maalum (inategemea na uwezo) wengine hufanyia nyumbani wengine ukumbini.

Huko kwenye chumba maalum ndugu watakupa nguo na chochote cha kumvisha marehemu. Ukishamaliza kumvisha na kumremba, mwili hutolewa na kuwekwa sehemu rasmi ya kuagiwa.

Shughuli ya kuagwa ikishaisha msafara wa kuelekea makaburini huanza.

Huko makaburini kuna sehemu kuu tatu muhimu
- Ukumbi wa ibada ya mwisho
- Jiko la kuchomea mwili (tanuru la gesi)
- Makaburi (yako kama vile vyumba ya mabox ya barua posta

Pale ukumbini jeneza huwekwa juu ya kichanja chenye sliders ambazo huenda moja kwa moja mpaka kwenye tanuru.

Hapa ndugu wanaopenda kumuona marehemu kwa mara ya mwisho kabisa huruhusiwa kufanya hivyo

Baada ya hapo jeneza husukumwa na kuingia sehemu ambapo pametenganishwa na kitambaa cheupe.Hapa hubaki mchomaji (mimi) na watu wake ambapo kwa mahitaji ya ndugu mnamvua marehemu vitu vya thamani nk.

Wakati huu tanuri maalum la gesi lenye nyuzi joto zinazofikia 1000 linakuwa tayari limeshawashwa. Kipindi hiki cha kumuandaa marehemu kwa ajili ya kumbutua ukumbi wote huwa kimya kabisa.

Shughuli fupi ya kumuandaa ikishaisha mchomaji (mimi sasa) hubonyeza switch maalum ambapo sliders huupeleka mwili kwenye tanuru kichwa kikiwa kimetangulia.. Kichwa kinapogusa tu mlango wa tanuru kuna taa nyekundu huwaka na king'ora cha ukiwa hulia kwa sauti ya chini kidogo

Basi hapo mwili utaingia wote na kile kimlango kujifunga kwa nyuma.... Dakika tano nyingi mnasikia kishindo cha kichwa kupasuka. Hapo taa ile nyekundu huzima, king'ora hukoma na kinachosikika sasa ni sauti za vilio vya ndugu, jamaa na marafiki huku wakitawanyika.

Dakika kati ya kumi na ishirini baadae kutegemeana na setting za moto mwili unakuwa umeungua na kuteketea kabisa na kubaki jivu. Jivu hupita sehemu maalum ya kupozwa. Baada ya hapo hutiwa kwenye kisanduku maalum (kaburi) chenye
Jina kamili la marehemu
Tarehe ya kuzaliwa
Tarehe ya kufa
Neno la faraja

Kufikia hapa mazishi yanakuwa yamekamilika na ndugu kuoneshwa kaburi la ndugu yao lilipo (kuna namba za makaburi) kisha kukabidhiwa funguo za kaburi na nguo ama vitu vingine kama vipo.
Na mifupa inageuka majivu?
 
Na kupata huduma hiyo ni bure au kuna gharama unatoa?
 
Na kupata huduma hiyo ni bure au kuna gharama unatoa?
Hapana kuna gharama... Ile furnace na yale makaburi ni miradi na uwekezaji wa watu ila kuna familia wao hupenda kuondoka na majivu yao ili wakayamwage mtoni ama wakayahifadhi nyumbani... Hapa gharama zinapungua
 
Hicho kiswahili cha "kuoka wafu" toka lini?
Cremation ndio kuoka?
Halafu wafu ni roho sio mwili ambao ukifa huitwa maiti.
Kuoka ni namna ya kuandaa nyama jikoni, iwe kwa mkaa, oven, au kuni. Toka lini maiti ikaokwa?
Mengine uliyosema watakujibu.
 
Hicho kiswahili cha "kuoka wafu" toka lini?
Cremation ndio kuoka?
Halafu wafu ni roho sio mwili ambao ukifa huitwa maiti.
Kuoka ni namna ya kuandaa nyama jikoni, iwe kwa mkaa, oven, au kuni. Toka lini maiti ikaokwa?
Mengine uliyosema watakujibu.
Nadhani nimeshalitolea ufafanuzi hili kwahiyo ni vema mjadala ukaendelea kuliko kubaki hapa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom