Kabrasha: Jiko la kuoka wafu (cremation)

Siku hizi Vichwa avilipuki. Hspl uvipasua hili kuangalia sababu ya kifo. Au utobolewa na jamaa kuondoa kishindo
 
wachomeee mzeee.....hivi ni kweli ukichomwa duniani, mbinguni ndo huchomwi tena sheik mshana
 
Ovens kama hizi zilikuwepo kwenye Nazi Concentration na death camps kama sobibor,treblinka,auchwitz birkenau na majdanek kwa ajili ya wayahudi na watu wengine waliokuwa wanauwawa kwenye gas chambers.
images.jpg
 
wachomeee mzeee.....hivi ni kweli ukichomwa duniani, mbinguni ndo huchomwi tena sheik mshana
[emoji23][emoji23][emoji23]moto uko palepale[emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91]
 
Akapeleka majivu mgombani ili ndizi zikiita ziwe na chembechembe za mkewe amkule kama matoke
Huwa naandaa mbavu zangu kabisa kila nikutanapo na mchango wako jamvini [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hawa wanao chomwa ukwepa lile rungu.. wanalo sema ndugu zetu kwamba ukizikwa malaika anakuja na rungu kuku surubu umo kaburini
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji848]
 
Kuna rafiki yake Bi Mkubwa ni jamii ya wahindi wamehifadhi jivu za ukoo wao kidogo tu. Yaani wamesave land kubwa balaa
 
Nimetimiza ahadi ya kuleta mada husika. Mada ya uzoefu wa kuchoma wafu moto hadi wateketee kabisa na kubaki majivu.

Kuchoma moto maiti ni aina mojawapo ya mazishi.

Mazishi mengine ni

- Kuzika ardhini
- Kutupa mwili porini na kuwa chakula cha wanyama
- Kuweka mwili juu ya kichanja maalum karibu na makazi ili ndege wapate kula
- Kuweka mwili kwenye chumba maalum, kwenye majabali nknk (viongozi na watu maarufu)
- Kutumbukiza mwili kwenye pipa la tindikali
Nk

Mimi nimeshiriki kikamilifu kwenye haya mazishi ya kuchoma moto na nimewabanika wengi tu kwenye miaka yangu sita ya huduma

Kinachofanyika ni hiki. Taratibu zote hufuatwa toka mochwari mpaka kumremba marehemu tayari kwa kuagwa.

Baada ya hapo kifuatacho ni kuelekea makaburini kwenye jengo la kuchomea.
Mara nyingi mwili unapotolewa mochwari hupelekwa mpaka eneo la kuagia ukiwa mtupu bila nguo zaidi ya mashuka yale ya mochwari. Lakini ukiwa tayari umeshatengenezwa vema
Watu wa mochwari huukabidhi kwa ndugu na ndugu nao huukabidhi kwa wazikaji (mimi) hapa mwili unakuwa kwenye chumba maalum (inategemea na uwezo) wengine hufanyia nyumbani wengine ukumbini.

Huko kwenye chumba maalum ndugu watakupa nguo na chochote cha kumvisha marehemu. Ukishamaliza kumvisha na kumremba, mwili hutolewa na kuwekwa sehemu rasmi ya kuagiwa.

Shughuli ya kuagwa ikishaisha msafara wa kuelekea makaburini huanza.

Huko makaburini kuna sehemu kuu tatu muhimu
- Ukumbi wa ibada ya mwisho
- Jiko la kuchomea mwili (tanuru la gesi)
- Makaburi (yako kama vile vyumba ya mabox ya barua posta

Pale ukumbini jeneza huwekwa juu ya kichanja chenye sliders ambazo huenda moja kwa moja mpaka kwenye tanuru.

Hapa ndugu wanaopenda kumuona marehemu kwa mara ya mwisho kabisa huruhusiwa kufanya hivyo

Baada ya hapo jeneza husukumwa na kuingia sehemu ambapo pametenganishwa na kitambaa cheupe.Hapa hubaki mchomaji (mimi) na watu wake ambapo kwa mahitaji ya ndugu mnamvua marehemu vitu vya thamani nk.

Wakati huu tanuri maalum la gesi lenye nyuzi joto zinazofikia 1000 linakuwa tayari limeshawashwa. Kipindi hiki cha kumuandaa marehemu kwa ajili ya kumbutua ukumbi wote huwa kimya kabisa.

Shughuli fupi ya kumuandaa ikishaisha mchomaji (mimi sasa) hubonyeza switch maalum ambapo sliders huupeleka mwili kwenye tanuru kichwa kikiwa kimetangulia.. Kichwa kinapogusa tu mlango wa tanuru kuna taa nyekundu huwaka na king'ora cha ukiwa hulia kwa sauti ya chini kidogo

Basi hapo mwili utaingia wote na kile kimlango kujifunga kwa nyuma.... Dakika tano nyingi mnasikia kishindo cha kichwa kupasuka. Hapo taa ile nyekundu huzima, king'ora hukoma na kinachosikika sasa ni sauti za vilio vya ndugu, jamaa na marafiki huku wakitawanyika.

Dakika kati ya kumi na ishirini baadae kutegemeana na setting za moto mwili unakuwa umeungua na kuteketea kabisa na kubaki jivu. Jivu hupita sehemu maalum ya kupozwa. Baada ya hapo hutiwa kwenye kisanduku maalum (kaburi) chenye
Jina kamili la marehemu
Tarehe ya kuzaliwa
Tarehe ya kufa
Neno la faraja

Kufikia hapa mazishi yanakuwa yamekamilika na ndugu kuoneshwa kaburi la ndugu yao lilipo (kuna namba za makaburi) kisha kukabidhiwa funguo za kaburi na nguo ama vitu vingine kama vipo.
Umefika wakati mwili wa binadamu uteketezwe badala ya kuzikwa kaburini?

9 Agosti 2019

Mshirikishe mwenzako

Image captionTanuru la mafuta ya dizeli la kuchoma wafu

Kuuchoma mwili wa binadamu baada kifo limekuwa ni jambo la kawaida kwa miaka mwingi miongoni mwa jamii za India na Nepal ambapo mchakato huu umekua ukifanyika mahala palipo wazi na utamaduni wa tangu enzi za kale . Kuanzia karne ya Starting in the 19 , uchomaji wa maiti ulianza kutekelezwa katika maeneo mengine ya dunia .

Hata hivyo katika nyakati hizi , mchakato wa kuchoma maiti umekuwa ukifanyika kwenye matanuru au mahala pa faragha palipofungwa palipotengwa maalumu kwa ajili ya shughuli hiyo.

Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa la watu idadi ya wa maeneo ya Afrika mashariki ambao wamechaguwa kuchomwa kwa miili yao kama njia ya kuihifadhi miili yao baada ya kifo badala ya njia ya kawaida ya kuzikwa kaburini.

Marekani, Uingereza zatilia shaka 'haki za raia kisheria' TanzaniaMsimu mpya, kuna jipya?Ni hatari kwa wanawake kufukiza sehemu zao za siri

Katika miezi ya hivi karibuni, kumeibua hisia tofauti katika eneo la Afrika Mashariki hususan nchini Kenya kuhusu kuchomwa kwa maiti baada ya mtu kufariki.

Wale wanaounga mkono uteketezwaji wa maiti wanasema mfumo huo wa mazishi ni wa kisasa na unapunguza gharama ikilinganishwa na maiti inapozikwa.

Image captionMshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel na mwanamazingira wa Kenya Profesa Wangari Maathai alichakua kuhifadhi mwili wake kwa kuuteketeza kwa moto

Kwa upande mwingine, wanaopinga wanadai kwamba utamaduni wa kuteketeza maiti ni wa kigeni unaoenda kinyume na mila na desturi za Kiafrika.

Chimbuko la mjadala huu ni kuteketezwa kwa miili ya watu mashuhuri ; aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi Safaricom, Robert "Bob" Collymore, na mbunge wa upinzani Ken Okoth.

Wakenya wengine mashuhuri ambao miili yao ilitekekezwa kwa moto ni aliyekuwa mshindi wa tuzo ya Nobel na mwana mazingira Profesa Wangari Mathaialiyefariki mwaka wa 2011 na aliyekuwa kiongozi wa upinzani nchini Kenneth Matiba.

Mwili wa aliyekuwa askofu mkuu wa kanisa la Kianglikana nchini Kenya pia ulichomwa mwaka wa 2005.

Image captionMwili wa Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi Safaricom, Robert "Bob" Collymore hivi karibuni pia ulichomwaJe mchakato wa kuuchoma mwili ni upi?

Kuna aina mbili za kuuchoma mwili wa binadamu, kulingana na Bwana Patel, afisa katika kituo cha kuchoma miili cha kariokor mjini Nairobi Kenya. ''Mwili ukifika hapa kwenye kituo chetu ndugu huchagua ni vipi mwili utachomwa, tuko na mashine na tuna kuni mnachagua kulingana na utashi wenu'', ameiambia BBC Bwana Harish Patel.

Kuchoma mwili kwa njia ya mafuta ya dizeli:

Kulinganza na Bwana Patel kuna mashine maalum zinazoweza kulinganishwa na tanuru ambapo mwili huingizwa ndani na kuchomwa kwa muda wa saa tatu hadi utakapoteketea kabisa na kuwa jivu. ''Tunauingiza mwili ndani ya mashine na kuchomea mwili ukiwa ndani ya jeneza kama ulivyoletwa hatubadilishi kitu. Mtu mmoja wa familia huchaguliwa ili awashe umeme anawasha na kisha tunasubiri mpaka saa tatu ziishe ili mwili uwe umeungua kabisa''.

Image captionTanuru la kuni la kuchoma maiti

Baada ya saa tatu mifupa ya marehemu huwa bado haijaungua ndani ya mashine hiyo na mifupa huondolewa kwenye mashine ya kuchoma mwili na kuwekwa kwenye mashine nyingine maalumu inayofanya kazi ya kusaga mifupa ya marehemu na kuifanya kuwa majivu, anasema Bwana Patel.

Ni kwa nini maiti huchomwa kuliko kuzikwa?Image captionMashine hii hutumiwa kuteketeza mifupa ya mwili wa maiti baada ya mwili kuchomwa na moto ndani ya tanuru na dizeli au kwa kuni

Kuchoma mwili kwa njia ya kuni:

Katika mchakato wa uchomaji wa mwili wa binadamu kwa njia ya kuni, mwili huwekwa kwenye kifaa cha chuma kilichotengenezwa mithili ya kichanja cha kuanika vyombo kisha rundo la kuni hupangwa juu na chini ya mwili, na kisha mwili hupakwa mafuta ya siagi na ufuta ili kuwezesha joto la moto kuuteketeza mwili kwa haraka.

Image captionMafuta ya samuli

Kulingana na Bwana Harish Patel gharama ya kuuchoma mwili wa binadamu iwe kwa njia ya dizeli au kuni ni dola 400 za kimarekani.

Image captionKuni huwekwa juu na chini ya kichanja cha kumchomea maiti huku maiti akiwekwa kati katika ya kuni

Historia fupi ya kuchomwa maiti:

Kuteketeza maiti kama sehemu ya mfumo wa mazishi kumefanyika tangu jadi zaidi ya miaka 10,000 iliyopita.Nchini China miili imekuwa ikiteketeza kuanzia miaka 8000BC yaani -kabla kuzaliwa kwa Yesu Kristo.Huko Ugiriki, uteketezaji maiti umekuwa ukifanyika tangu mwaka 480BC na nchini Sweeden desturi hiyo imekuwepo tangu jadi na kukomesha yapata miaka 1,000 iliyopita baada ya dini ya Ukristo kuingia huko.Baada ya injili ya Kristo kuenezwa barani Ulaya, desturi hiyo ilififia kwani Wakristo waliitaja kuwa kinyume na maadili ya dini.Afisa Mtendaji Mkuu wa Safaricom aaga duniaAdhabu ya kifo kutekelezwa tena MarekaniUtam
 
Nimetimiza ahadi ya kuleta mada husika. Mada ya uzoefu wa kuchoma wafu moto hadi wateketee kabisa na kubaki majivu.

Kuchoma moto maiti ni aina mojawapo ya mazishi.

Mazishi mengine ni

- Kuzika ardhini
- Kutupa mwili porini na kuwa chakula cha wanyama
- Kuweka mwili juu ya kichanja maalum karibu na makazi ili ndege wapate kula
- Kuweka mwili kwenye chumba maalum, kwenye majabali nknk (viongozi na watu maarufu)
- Kutumbukiza mwili kwenye pipa la tindikali
Nk

Mimi nimeshiriki kikamilifu kwenye haya mazishi ya kuchoma moto na nimewabanika wengi tu kwenye miaka yangu sita ya huduma

Kinachofanyika ni hiki. Taratibu zote hufuatwa toka mochwari mpaka kumremba marehemu tayari kwa kuagwa.

Baada ya hapo kifuatacho ni kuelekea makaburini kwenye jengo la kuchomea.
Mara nyingi mwili unapotolewa mochwari hupelekwa mpaka eneo la kuagia ukiwa mtupu bila nguo zaidi ya mashuka yale ya mochwari. Lakini ukiwa tayari umeshatengenezwa vema
Watu wa mochwari huukabidhi kwa ndugu na ndugu nao huukabidhi kwa wazikaji (mimi) hapa mwili unakuwa kwenye chumba maalum (inategemea na uwezo) wengine hufanyia nyumbani wengine ukumbini.

Huko kwenye chumba maalum ndugu watakupa nguo na chochote cha kumvisha marehemu. Ukishamaliza kumvisha na kumremba, mwili hutolewa na kuwekwa sehemu rasmi ya kuagiwa.

Shughuli ya kuagwa ikishaisha msafara wa kuelekea makaburini huanza.

Huko makaburini kuna sehemu kuu tatu muhimu
- Ukumbi wa ibada ya mwisho
- Jiko la kuchomea mwili (tanuru la gesi)
- Makaburi (yako kama vile vyumba ya mabox ya barua posta

Pale ukumbini jeneza huwekwa juu ya kichanja chenye sliders ambazo huenda moja kwa moja mpaka kwenye tanuru.

Hapa ndugu wanaopenda kumuona marehemu kwa mara ya mwisho kabisa huruhusiwa kufanya hivyo

Baada ya hapo jeneza husukumwa na kuingia sehemu ambapo pametenganishwa na kitambaa cheupe.Hapa hubaki mchomaji (mimi) na watu wake ambapo kwa mahitaji ya ndugu mnamvua marehemu vitu vya thamani nk.

Wakati huu tanuri maalum la gesi lenye nyuzi joto zinazofikia 1000 linakuwa tayari limeshawashwa. Kipindi hiki cha kumuandaa marehemu kwa ajili ya kumbutua ukumbi wote huwa kimya kabisa.

Shughuli fupi ya kumuandaa ikishaisha mchomaji (mimi sasa) hubonyeza switch maalum ambapo sliders huupeleka mwili kwenye tanuru kichwa kikiwa kimetangulia.. Kichwa kinapogusa tu mlango wa tanuru kuna taa nyekundu huwaka na king'ora cha ukiwa hulia kwa sauti ya chini kidogo

Basi hapo mwili utaingia wote na kile kimlango kujifunga kwa nyuma.... Dakika tano nyingi mnasikia kishindo cha kichwa kupasuka. Hapo taa ile nyekundu huzima, king'ora hukoma na kinachosikika sasa ni sauti za vilio vya ndugu, jamaa na marafiki huku wakitawanyika.

Dakika kati ya kumi na ishirini baadae kutegemeana na setting za moto mwili unakuwa umeungua na kuteketea kabisa na kubaki jivu. Jivu hupita sehemu maalum ya kupozwa. Baada ya hapo hutiwa kwenye kisanduku maalum (kaburi) chenye
Jina kamili la marehemu
Tarehe ya kuzaliwa
Tarehe ya kufa
Neno la faraja

Kufikia hapa mazishi yanakuwa yamekamilika na ndugu kuoneshwa kaburi la ndugu yao lilipo (kuna namba za makaburi) kisha kukabidhiwa funguo za kaburi na nguo ama vitu vingine kama vipo.
 
Nimetimiza ahadi ya kuleta mada husika. Mada ya uzoefu wa kuchoma wafu moto hadi wateketee kabisa na kubaki majivu.

Kuchoma moto maiti ni aina mojawapo ya mazishi.

Mazishi mengine ni

- Kuzika ardhini
- Kutupa mwili porini na kuwa chakula cha wanyama
- Kuweka mwili juu ya kichanja maalum karibu na makazi ili ndege wapate kula
- Kuweka mwili kwenye chumba maalum, kwenye majabali nknk (viongozi na watu maarufu)
- Kutumbukiza mwili kwenye pipa la tindikali
Nk

Mimi nimeshiriki kikamilifu kwenye haya mazishi ya kuchoma moto na nimewabanika wengi tu kwenye miaka yangu sita ya huduma

Kinachofanyika ni hiki. Taratibu zote hufuatwa toka mochwari mpaka kumremba marehemu tayari kwa kuagwa.

Baada ya hapo kifuatacho ni kuelekea makaburini kwenye jengo la kuchomea.
Mara nyingi mwili unapotolewa mochwari hupelekwa mpaka eneo la kuagia ukiwa mtupu bila nguo zaidi ya mashuka yale ya mochwari. Lakini ukiwa tayari umeshatengenezwa vema
Watu wa mochwari huukabidhi kwa ndugu na ndugu nao huukabidhi kwa wazikaji (mimi) hapa mwili unakuwa kwenye chumba maalum (inategemea na uwezo) wengine hufanyia nyumbani wengine ukumbini.

Huko kwenye chumba maalum ndugu watakupa nguo na chochote cha kumvisha marehemu. Ukishamaliza kumvisha na kumremba, mwili hutolewa na kuwekwa sehemu rasmi ya kuagiwa.

Shughuli ya kuagwa ikishaisha msafara wa kuelekea makaburini huanza.

Huko makaburini kuna sehemu kuu tatu muhimu
- Ukumbi wa ibada ya mwisho
- Jiko la kuchomea mwili (tanuru la gesi)
- Makaburi (yako kama vile vyumba ya mabox ya barua posta

Pale ukumbini jeneza huwekwa juu ya kichanja chenye sliders ambazo huenda moja kwa moja mpaka kwenye tanuru.

Hapa ndugu wanaopenda kumuona marehemu kwa mara ya mwisho kabisa huruhusiwa kufanya hivyo

Baada ya hapo jeneza husukumwa na kuingia sehemu ambapo pametenganishwa na kitambaa cheupe.Hapa hubaki mchomaji (mimi) na watu wake ambapo kwa mahitaji ya ndugu mnamvua marehemu vitu vya thamani nk.

Wakati huu tanuri maalum la gesi lenye nyuzi joto zinazofikia 1000 linakuwa tayari limeshawashwa. Kipindi hiki cha kumuandaa marehemu kwa ajili ya kumbutua ukumbi wote huwa kimya kabisa.

Shughuli fupi ya kumuandaa ikishaisha mchomaji (mimi sasa) hubonyeza switch maalum ambapo sliders huupeleka mwili kwenye tanuru kichwa kikiwa kimetangulia.. Kichwa kinapogusa tu mlango wa tanuru kuna taa nyekundu huwaka na king'ora cha ukiwa hulia kwa sauti ya chini kidogo

Basi hapo mwili utaingia wote na kile kimlango kujifunga kwa nyuma.... Dakika tano nyingi mnasikia kishindo cha kichwa kupasuka. Hapo taa ile nyekundu huzima, king'ora hukoma na kinachosikika sasa ni sauti za vilio vya ndugu, jamaa na marafiki huku wakitawanyika.

Dakika kati ya kumi na ishirini baadae kutegemeana na setting za moto mwili unakuwa umeungua na kuteketea kabisa na kubaki jivu. Jivu hupita sehemu maalum ya kupozwa. Baada ya hapo hutiwa kwenye kisanduku maalum (kaburi) chenye
Jina kamili la marehemu
Tarehe ya kuzaliwa
Tarehe ya kufa
Neno la faraja

Kufikia hapa mazishi yanakuwa yamekamilika na ndugu kuoneshwa kaburi la ndugu yao lilipo (kuna namba za makaburi) kisha kukabidhiwa funguo za kaburi na nguo ama vitu vingine kama vipo.
Hapo kwenye kichwa kupasuka hadi nimetetemeka
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom